DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 551
..huko ndo kukandamiza ki zenj!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maalim azuiwa Zanzibar
na Mohammed Abduralhman
ZIARA ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kutembelea wagonjwa katika hospitali za wilayani Unguja na Pemba imeingia dosari, baada ya kuzuiliwa kutembelea Hospitali ya Mkoa Kaskazini Unguja iliyopo Kivunge.
Hamad juzi alitembelea wagonjwa waliopo majumbani, lakini Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imemzuia kutembelea hospitali hiyo kwa kile kilichoelezwa sababu za kitaalamu.
Ujumbe wa Maalim Seif ulikuwa umeambatana na Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Kaskazini A Unguja, Bakari Makame, Katibu wa jimbo hilo, Khamis Abass na Mbunge wa Viti Maalumu wa CUF, Mwajuma pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani.
Kiongozi huyo amezuiwa kutembelea katika hospitali hiyo na Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge, Mtumwa Ibrahim, ambaye alisema kutokana na sababu za kitaalamu, ujumbe huo hauruhusiwi kutembelea hospitali hiyo. Hata hivyo hakufafanua zaidi.
Alisema ni kweli uongozi wa hospitali ulipokea ombi la ujumbe huo kutaka kuruhusiwa hospitalini kuwajulia hali wagonjwa wanaopatiwa matibabu, lakini kutokana na sababu hizo haikuwezekana.
Kutokana na sababu za kitaalamu haitawezekana kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Kivunge, alisema daktari huyo Dhamana, katika barua yake ya Oktoba 5, mwaka huu.
Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Bimani, alisema CUF imesikitishwa na uamuzi huo, kwa vile umewanyima haki wagonjwa kusalimiwa na kupatiwa msaada.
Bimani, alisema ni jambo la kushangaza wakati Maalim Seif anazuiwa kuwatembelea wagonjwa, wananchi mbalimbali wanaruhusiwa kuwatembelea katika hospitali hiyo hiyo.
Alieleza kuwa tangu ziara ya Maalim Seif kuanza kuwatembelea wagonjwa hospitalini na majumbani, kumekuwa kukijitokeza matatizo mbalimbali, ikiwamo huko Micheweni ambako wafanyakazi wa hospiatli walitakiwa kujieleza ni kwanini walimruhusu katibu mkuu huyo wa CUF kutembelea hospitalini hapo.
Alisema CUF imeamua suala hilo kulikabidhi kwa kiongozi wa upinzani katika Baraza la Wawakilishi, ili kuhoiji kwanini serikali inafanya hivyo.
Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Maalim Seif amekuwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa majumbani, hospitalini na ziara hiyo aliianzia katika mikoa miwili ya Pemba na sasa inaendelea kisiwani Unguja.
Akiwa kisiwani Pemba, katibu mkuu huyo alitembelea hospitali za Mkoani, Abdalla Mzee, Wete na Micheweni, na kutoa misaada kwa ajili ya wagonjwa, ikiwemo mashuka ya kutandikia vitanda na vyandarua.
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, aliwataka viongozi wa CCM Zanzibar kuwa na utamaduni wa kutembelea wagonjwa hospitali ili kuwa karibu na wananchi.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mpendae, Makamba alisema viongozi wanapotembelea wagonjwa na kubeba zawadi kama vile matunda, kunajenga faraja kwa wahusika.
source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/8/habari3.php
Kazi nzuri sana......Please view my website about Zanzibar History.
KiSwahili:
http://zanzibarhistory.org/swahili_home_page.htm
English:
http://zanzibarhistory.org/
mie nnaona bomba tu, nnategemea itakuwa poa kinoma. ila mume hataki kumuacha mke.
hee heee kapendezewa na kunogewa
Sio upemba kwani wapemba ni watu wazuri tu,tena ni watu wenye imani sana tofauti na Wazanzibari wengine wenye asili ya Unguja ambao inasemekana ni wavivu sana.Bora kuwepo Wapemba hapa Bongo kuliko hawa wa kutoka Unguja ambao mara nyingi inaonekana ni mizigo kama walivyo huko Bungeni,wapemba walioko bungeni wanapigania maslahi ya Tanzania nzima na wanahoji kila kitu wanachokiona kina maslahi na Taifa na ni bora tukaungana na Wapemba kuliko waunguja,weka mbali hilo.Zamani, Wazenji hawakuupenda.
Sasa, Wabara ndio wasioupenda zaidi.
Ukivunjika, hawa Wapemba waliojazana Kariakoo, Mtoni, Ilala, Buguruni nk. watahama na nyumba "zetu"? Mare living space.
Mchele, nyanya, Vitunguu, sembe tutauza kwa dola. Faida tosha kwa Wabara.
Gharama za kuwalipa wabunge wa ng'ambo ya pili zitatoweka. Hii ni saving kubwa hasa ukifanya cost-benefit analysis.
Udini uliopo hapa Bara umeletwa na influx ya Wapemba. Kutoka kwao itakuwa baraka kubwa.
Zamani, Wazenji hawakuupenda.
Sasa, Wabara ndio wasioupenda zaidi.
Ukivunjika, hawa Wapemba waliojazana Kariakoo, Mtoni, Ilala, Buguruni nk. watahama na nyumba "zetu"? Mare living space.
Mchele, nyanya, Vitunguu, sembe tutauza kwa dola. Faida tosha kwa Wabara.
Gharama za kuwalipa wabunge wa ng'ambo ya pili zitatoweka. Hii ni saving kubwa hasa ukifanya cost-benefit analysis.
Udini uliopo hapa Bara umeletwa na influx ya Wapemba. Kutoka kwao itakuwa baraka kubwa.
Hapana ndugu,katika hili ni tofauti na kufananisha mkoa,hizi ni Inchi mbili zilizoungana,leo Wazanzibar wakikusikia unawaita mkoa basi kidole machoni,kuna ule wakati waliambiwa hawajalipa umeme,wakasikika wakisema umeme ukikatwa Muungano ndio mwisho,sasa wakilipa wasilipe ni hiari yao,hapo hawakulipa kitu na umeme hatukuona kukatwa inamaanisha sisi ndio tunawahitaji bila ya wao hatuwezi kujiongoza,hatuwezi kujiamulia imekuwa kama wanatuburuza na hata hivyo bado wanasema hatuwatendei haki,haki gani hiyo watumie umeme bure na mapato waweke ndani,lile deni hawajalilipa mpaka kesho.Kinachojadiliwa hapa naona ni upimbi tu usio na mipaka. Wapemba wanaofanya biashara Tanzania bara wanalipa kodi ambayo inasaidia nchi nzima. Hivyo faida sio ya mfanyabiashara peke yake.
Na kuhusu muungano hakuna sababu ya kuuvunja kwa sababu Tanganyika na Zanzibar ni wanachama wa Jumuia Ya Afrika Mashariki. Na muungano ukivunjika bado wapemba watafanya biashara Tanganyika kama wakazi wa jumuia ya Afrika mashariki.
Kama ni COST BENEFIT Analysis, kuna mikoa mingi Tanganyika haizalishi kitu chochote na mzigo kwa mikoa mingine. Siku muungano unavunjika lazima turudishe majimbo. Na kila jimbo lijitegemea lenyewe.
Kinachojadiliwa hapa naona ni upimbi tu usio na mipaka. Wapemba wanaofanya biashara Tanzania bara wanalipa kodi ambayo inasaidia nchi nzima. Hivyo faida sio ya mfanyabiashara peke yake.
Na kuhusu muungano hakuna sababu ya kuuvunja kwa sababu Tanganyika na Zanzibar ni wanachama wa Jumuia Ya Afrika Mashariki. Na muungano ukivunjika bado wapemba watafanya biashara Tanganyika kama wakazi wa jumuia ya Afrika mashariki.
Kama ni COST BENEFIT Analysis, kuna mikoa mingi Tanganyika haizalishi kitu chochote na mzigo kwa mikoa mingine. Siku muungano unavunjika lazima turudishe majimbo. Na kila jimbo lijitegemea lenyewe.