Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
kwani kampeni zishaanza? na jee kutembelea wagonjwa sharti uwe na timu kubwa na waandishi wa habari? na kuomba kibali rasmi? maalim allikuwa na ajenda ya siri? ya kujinufaisha kisiasa>?
 
Maalim azuiwa Zanzibar



na Mohammed Abduralhman



ZIARA ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kutembelea wagonjwa katika hospitali za wilayani Unguja na Pemba imeingia dosari, baada ya kuzuiliwa kutembelea Hospitali ya Mkoa Kaskazini Unguja iliyopo Kivunge.
Hamad juzi alitembelea wagonjwa waliopo majumbani, lakini Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar imemzuia kutembelea hospitali hiyo kwa kile kilichoelezwa sababu za kitaalamu.

Ujumbe wa Maalim Seif ulikuwa umeambatana na Mwenyekiti wa CUF, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Bakari Makame, Katibu wa jimbo hilo, Khamis Abass na Mbunge wa Viti Maalumu wa CUF, Mwajuma pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Mawasiliano ya Umma, Salum Bimani.
Kiongozi huyo amezuiwa kutembelea katika hospitali hiyo na Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge, Mtumwa Ibrahim, ambaye alisema kutokana na sababu za kitaalamu, ujumbe huo hauruhusiwi kutembelea hospitali hiyo. Hata hivyo hakufafanua zaidi.

Alisema ni kweli uongozi wa hospitali ulipokea ombi la ujumbe huo kutaka kuruhusiwa hospitalini kuwajulia hali wagonjwa wanaopatiwa matibabu, lakini kutokana na sababu hizo haikuwezekana.

“Kutokana na sababu za kitaalamu haitawezekana kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Kivunge,” alisema daktari huyo Dhamana, katika barua yake ya Oktoba 5, mwaka huu.

Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Bimani, alisema CUF imesikitishwa na uamuzi huo, kwa vile umewanyima haki wagonjwa kusalimiwa na kupatiwa msaada.

Bimani, alisema ni jambo la kushangaza wakati Maalim Seif anazuiwa kuwatembelea wagonjwa, wananchi mbalimbali wanaruhusiwa kuwatembelea katika hospitali hiyo hiyo.

Alieleza kuwa tangu ziara ya Maalim Seif kuanza kuwatembelea wagonjwa hospitalini na majumbani, kumekuwa kukijitokeza matatizo mbalimbali, ikiwamo huko Micheweni ambako wafanyakazi wa hospiatli walitakiwa kujieleza ni kwanini walimruhusu katibu mkuu huyo wa CUF kutembelea hospitalini hapo.

Alisema CUF imeamua suala hilo kulikabidhi kwa kiongozi wa upinzani katika Baraza la Wawakilishi, ili kuhoiji kwanini serikali inafanya hivyo.

Tangu kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Maalim Seif amekuwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa majumbani, hospitalini na ziara hiyo aliianzia katika mikoa miwili ya Pemba na sasa inaendelea kisiwani Unguja.

Akiwa kisiwani Pemba, katibu mkuu huyo alitembelea hospitali za Mkoani, Abdalla Mzee, Wete na Micheweni, na kutoa misaada kwa ajili ya wagonjwa, ikiwemo mashuka ya kutandikia vitanda na vyandarua.

Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, aliwataka viongozi wa CCM Zanzibar kuwa na utamaduni wa kutembelea wagonjwa hospitali ili kuwa karibu na wananchi.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mpendae, Makamba alisema viongozi wanapotembelea wagonjwa na kubeba zawadi kama vile matunda, kunajenga faraja kwa wahusika.

source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/8/habari3.php


Mtu wa pwani.......

siasa za znz ni ngumu,mie hapo namlaumu SSH moja kwa moja,kwa nn?ndani ya roho yake hana nia kwenda kuwatazama wagonjwa,nia yake ni kuwenda kufanya siasa ndani ya hospitali,kwa sababu kama angekuwa na nia ya kwenda kuwaona wagonjwa angeenda yeye peke yake na mlinzi wake na dereva wake tu basi,lkn angalia hapo juu hiyo deligation ina maana hapo si chini ya gari 10-15 with full ulinzi wake waandishi wake na wapiga pic ina mana hapo ni siasa tu na sio kwenda kuwaona wagonjwa.
mie namuunga mkono kabisa huyo daktari mkuu kumkatalia kwenda kuona wagonjwa.
 
Mimi simlaumu Maalim Seif, hizi ni karata ambazo chama chochote kinaweza kuzicheza, why not?
 
Marekani yavutiwa Z`bar
na mwandishi wetu, zanzibar

KAMPUNI ya Good Works International (GWICONSULTING) kutoka Marekani imesema imevutiwa na mazingira ya Visiwa vya Zanzibar na kwa sababu hiyo, inakusudia kuanza kuwekeza.

Akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi jana, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni hiyo, Jill Bishop, alisema kuwa Kampuni ya GWICONSULTING imeona maeneo mengi ya uwekezaji, yakiwamo ya sekta ya utalii kutokana na kuwapo vivutio vingi.

Jill alisema kwamba kuja kwake kunatokana na hatua kubwa za kiuchumi na maendeleo zilizopatikana nchini Tanzania, ikiwamo Zanzibar, ambayo imepiga hatua katika uwekezaji kwenye utalii.

Alisema kutokana na ziara yake fupi aliyofanya kwenye maeneo mbalimbali, amebaini kuwapo kwa mafanikio katika sekta ya utalii kutokana na Zanzibar kuwa na vivutio vya kutosha. Mkurugenzi huyo alieleza kuwa ardhi ya visiwa inavutia na inaonyesha kuwa na rutuba nzuri inayostahili kuzalisha mazao ya chakula na biashara.

Alisema kampuni yake pia imeona uwezo kubwa wa kuitangaza Zanzibar kiutalii kupitia vyombo vya habari vya nchini mwake, ili kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji.

Alisema kampuni yake imeshawekeza katika nchi za Nigeria, Ghana na Afrika Kusini.

Kwa upande wake, Rais Karume alisema kuwa tayari mafanikio yameshapatikana katika sekta ya utalii, kutokana na wawekezaji wengi kujielekeza kwenye sekta hiyo. Rais Karume alisema kwamba Serikali imekuwa ikifanya juhudi za makusudi kuimarisha sekta za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wote.

Alisema kuwa kujitokeza kwa kampuni kutoka Marekani kutaendeleza sekta ya uwekezaji katika utalii na sekta nyingine
 
Kama ningelikuwa Raisi wa Tanzania tayari ningelikwisha uvunja Muungano uliokuwepo wa Tanganyika na Zanzibar na kila mmoja akabeba mzigo wake mwenyewe.
Kipimo ninachokiona ni lawama kutoka kwa Wazanzibar ambao wanaona Watanganyika hutumika katika mauaji yanayotokea kila ufikapo wakati wa Uchaguzi Mkuu,na pia waZanzibar hawaeshi kulalamika kila siku kuwa wanabanwa wanamezwa,na Mawaziri wanapotembelea nchi za inje hukumbwa na masuala yanayowadhalilisha kuwa Serikali yao ni ya ukandamizaji na hpo huekewa caseti za kideo kujionea udhalilishaji na mauaji yanayofanywa na vikosi vilivyovaa nembo ya Muungano,kiasi cha mawaziri huwa hawana jibu muafaka kujibu tuhuma hizo ambazo zinaonyweshwa live mbele ya macho yao.
Nini Tanganyika itakosa ikiwa tutaachana na Muungano huu.
Naomba kuwasilisha hoja.
 
mie nnaona bomba tu, nnategemea itakuwa poa kinoma. ila mume hataki kumuacha mke.

hee heee kapendezewa na kunogewa
 
mie nnaona bomba tu, nnategemea itakuwa poa kinoma. ila mume hataki kumuacha mke.

hee heee kapendezewa na kunogewa

..imekuwa muda sasa huonekani jamvini!kulikoni?

..si unajua marashi ya karafuu na udi wa kufukiza!bila kusahau jasmine!
 
Zamani, Wazenji hawakuupenda.
Sasa, Wabara ndio wasioupenda zaidi.

Ukivunjika, hawa Wapemba waliojazana Kariakoo, Mtoni, Ilala, Buguruni nk. watahama na nyumba "zetu"? Mare living space.

Mchele, nyanya, Vitunguu, sembe tutauza kwa dola. Faida tosha kwa Wabara.

Gharama za kuwalipa wabunge wa ng'ambo ya pili zitatoweka. Hii ni saving kubwa hasa ukifanya cost-benefit analysis.

Udini uliopo hapa Bara umeletwa na influx ya Wapemba. Kutoka kwao itakuwa baraka kubwa.
 
Zamani, Wazenji hawakuupenda.
Sasa, Wabara ndio wasioupenda zaidi.

Ukivunjika, hawa Wapemba waliojazana Kariakoo, Mtoni, Ilala, Buguruni nk. watahama na nyumba "zetu"? Mare living space.

Mchele, nyanya, Vitunguu, sembe tutauza kwa dola. Faida tosha kwa Wabara.

Gharama za kuwalipa wabunge wa ng'ambo ya pili zitatoweka. Hii ni saving kubwa hasa ukifanya cost-benefit analysis.

Udini uliopo hapa Bara umeletwa na influx ya Wapemba. Kutoka kwao itakuwa baraka kubwa.
Sio upemba kwani wapemba ni watu wazuri tu,tena ni watu wenye imani sana tofauti na Wazanzibari wengine wenye asili ya Unguja ambao inasemekana ni wavivu sana.Bora kuwepo Wapemba hapa Bongo kuliko hawa wa kutoka Unguja ambao mara nyingi inaonekana ni mizigo kama walivyo huko Bungeni,wapemba walioko bungeni wanapigania maslahi ya Tanzania nzima na wanahoji kila kitu wanachokiona kina maslahi na Taifa na ni bora tukaungana na Wapemba kuliko waunguja,weka mbali hilo.
Ninachokisema ni hizi serikali ya Zanzibar ambayoinaonekana ni mzigo usio tulika hapa kwetu Bongo,wanatudhalilisha vibaya sana leo gazetini wamewapiga marufuku wanao toa mihadhara kuhutubia huko Zanzibar ,kama mtakumbuka yuko shehe ajulikanae kwa jina la shehe Kurwa huyu alitimuliwa Zanzibar chini ya mtutu au chini ya ulinzi mkali na walisema anarudishwa kwao Tanganyika eti anajihusiha na uchochezi hiyo ni chini ya utawala wa Salimini,hivi huku ndio kuungana kama si unyanyasaji wa mtu ndani ya Nchi yake ni kitu gani ? Na hili si kwa mashehe tu hata dini zingine hazina uhuru wa kueneza neno lao,wanaogopa.
Wapemba wana mabiashara hapa na wameajiri vijana wengi wa Tanganyika kuliko kutoka kwao naweza kusema ni waekezaji wazuri tu wanaokubalika na jamii yetu,sifa yao nasikia ni ya kuhama hama na kuenea kibiashara kama walivyo wa jamii ya kichaga na huweza kujituma bila ya kuchagua kazi kama walivyo jamii ya kisambaa,hivyo kuwepo kwao sio mzigo bali ni lubricate kwa vijana wetu.
 
Zamani, Wazenji hawakuupenda.
Sasa, Wabara ndio wasioupenda zaidi.

Ukivunjika, hawa Wapemba waliojazana Kariakoo, Mtoni, Ilala, Buguruni nk. watahama na nyumba "zetu"? Mare living space.

Mchele, nyanya, Vitunguu, sembe tutauza kwa dola. Faida tosha kwa Wabara.

Gharama za kuwalipa wabunge wa ng'ambo ya pili zitatoweka. Hii ni saving kubwa hasa ukifanya cost-benefit analysis.

Udini uliopo hapa Bara umeletwa na influx ya Wapemba. Kutoka kwao itakuwa baraka kubwa.

Halafu nashangaa sana, watu wanakuwa wagumu na wazito sana kuongelea muungano utadhani ulitoka kwa Mungu, kuwa hakuna wa kuutangua milele. Of couse we will one day sit and calculate CBA, Cost benefit analysis na kuamua kama muungano unatufaa ama la. Jumbe alichafua hali ya hewa kutokana na kutaka CBA ifanyike na ajue A-Z za mkataba wa muungano. Sidhani kama kuna awaye yeyote katika sisiemu aliye tayari kuzungumzia hili suala la Muungano kwa uwazi na kinagaubaga.
Tuuchambue muungano.
 
fanya research that gonna sound better to air yr views,naamini muungano huu ni muzigo kwetu tz bara just to say in brief.
 
Honestly huu muungano hauna faida kwa watanganyika ni ile khali tu ya kuwa tumeongezewa ndugu from the other side. Maana hatufaidiki na chochote kutoka kwao ila wao sasa mambo lukuki wanapata. Lakini bado wao ndiyo wanachonga kupita kiasi mara madini yawe ya muungano, mara jeshi wakati kasehemu kenyewe hata dar hakaifikii robo.
Tumewabeba kwa mengi hapo kabla inabidi waonyeshe shukrani otherwise watoswe tu.
 
Kinachojadiliwa hapa naona ni upimbi tu usio na mipaka. Wapemba wanaofanya biashara Tanzania bara wanalipa kodi ambayo inasaidia nchi nzima. Hivyo faida sio ya mfanyabiashara peke yake.

Na kuhusu muungano hakuna sababu ya kuuvunja kwa sababu Tanganyika na Zanzibar ni wanachama wa Jumuia Ya Afrika Mashariki. Na muungano ukivunjika bado wapemba watafanya biashara Tanganyika kama wakazi wa jumuia ya Afrika mashariki.

Kama ni COST BENEFIT Analysis, kuna mikoa mingi Tanganyika haizalishi kitu chochote na mzigo kwa mikoa mingine. Siku muungano unavunjika lazima turudishe majimbo. Na kila jimbo lijitegemea lenyewe.
 
Kinachojadiliwa hapa naona ni upimbi tu usio na mipaka. Wapemba wanaofanya biashara Tanzania bara wanalipa kodi ambayo inasaidia nchi nzima. Hivyo faida sio ya mfanyabiashara peke yake.

Na kuhusu muungano hakuna sababu ya kuuvunja kwa sababu Tanganyika na Zanzibar ni wanachama wa Jumuia Ya Afrika Mashariki. Na muungano ukivunjika bado wapemba watafanya biashara Tanganyika kama wakazi wa jumuia ya Afrika mashariki.

Kama ni COST BENEFIT Analysis, kuna mikoa mingi Tanganyika haizalishi kitu chochote na mzigo kwa mikoa mingine. Siku muungano unavunjika lazima turudishe majimbo. Na kila jimbo lijitegemea lenyewe.
Hapana ndugu,katika hili ni tofauti na kufananisha mkoa,hizi ni Inchi mbili zilizoungana,leo Wazanzibar wakikusikia unawaita mkoa basi kidole machoni,kuna ule wakati waliambiwa hawajalipa umeme,wakasikika wakisema umeme ukikatwa Muungano ndio mwisho,sasa wakilipa wasilipe ni hiari yao,hapo hawakulipa kitu na umeme hatukuona kukatwa inamaanisha sisi ndio tunawahitaji bila ya wao hatuwezi kujiongoza,hatuwezi kujiamulia imekuwa kama wanatuburuza na hata hivyo bado wanasema hatuwatendei haki,haki gani hiyo watumie umeme bure na mapato waweke ndani,lile deni hawajalilipa mpaka kesho.
Kuhusu mikoa iliyokuwa haizalishi hii ni yetu na hailalamiki kama inatengwa ,na haiwezi kulalamika kwani wanajijua kwamba hawazalishi kitu hivyo ni tegemezi lakini kwa upande wa Zanzibar wanajiona wao ni matajiri sijui mila zao ni kubwa na za ajabu ambazo sisi huku tunaonekana wahuni tu,tukienda huko tunaenda kuwaharibia na kuwaenezea magonjwa na kuharibu mila zao,sijui wana mila gani ambazo ni bora kuliko zetu ,mimi sijaona utamaduni wao wala siujui na kuambiwa huu ni utamaduni wa wazanziba.Imetoka amri jamii ya wamasai wavae suruali na shati hivi huu kama si udhalilishaji ni kitu gani,ni ubabe tu tunaofanyiwa na watu hawa.
Kuna rafiki yangu wa Arusha ambae yuko katika cheo ndani ya chama CCM nilimuuliza kuna faida gani kuendelea na watu hawa ambao wanatuona waTanganyika ni wakandamizaji akanijibu ,unajua hawa tukiwaacha kutawalana watauana halafu lawama zitaturudia sisi,nikamjibu si bora waachiwe wauane wenyewe kwa wenyewe kuliko sisi ndio tunaonekana ndio tunaopeleka majeshi na kuwaua kila unapofika uchaguzi mkuu,na lawama zinazotufika ni kubwa kiasi cha kutukosesha maslahi na kuturudisha nyuma,kila tunapopagusa pako moto kwa hali ya huko Zanzibar tunaambiwa tunahusika wakati hatupati faida yeyote kuwepo kwa huu muungano angalau tuna cha kusema tukivunja Muungano basi Inchi yetu itaporomoka kwa sababu huko Zanzibar tunategemea kitu hiki na kile,hivi jamani ni vitu gani hivyo tusivyovijuwa sisi wingine??
 
Kinachojadiliwa hapa naona ni upimbi tu usio na mipaka. Wapemba wanaofanya biashara Tanzania bara wanalipa kodi ambayo inasaidia nchi nzima. Hivyo faida sio ya mfanyabiashara peke yake.

Na kuhusu muungano hakuna sababu ya kuuvunja kwa sababu Tanganyika na Zanzibar ni wanachama wa Jumuia Ya Afrika Mashariki. Na muungano ukivunjika bado wapemba watafanya biashara Tanganyika kama wakazi wa jumuia ya Afrika mashariki.

Kama ni COST BENEFIT Analysis, kuna mikoa mingi Tanganyika haizalishi kitu chochote na mzigo kwa mikoa mingine. Siku muungano unavunjika lazima turudishe majimbo. Na kila jimbo lijitegemea lenyewe.

Hivi ni mkoa gani ambao ni mzigo wa mkoa mwingine? Unaweza kutupatia takwimu hapa ili tulinganishe maneno yako kama ni kweli au umeamua tu kuzusha kama mwanzilishi wa topic hii. Mzee Ruksa alikuwa rais wa Zanzibar na baadaye Tanzania hakuona sababu ya kuvunja muungano, BWM na sasa JK hakuna anayetaka kuvunja muungano.
 
Ndugu Mwiba:

Mpaka sasa unachemsha na ujaeleza sababu za kuvunja muungano. Kuhusu suala la wamasai kuvaa suruali nakubaliana na Wazanzibar. Mavazi ya asili ya kimasai yamepitwa na wakati kama ilivyopita mila ya kutahiri wanawake. Nimeisoma historia ya Tanzania vizuri sana. Wamasai, Wachagga, Wagogo na makabila mengi walikuwa wanavaa lubega kama wamasai. Kwanini wamasai bado wanaendekeza fasheni yao wakati makabila mengine yameshakuwa progressive. Na kama wanapenda jadi zao badi wavae ngozi au magamba ya miti.

Kuhusu suala la umeme ni upumbavu kuleta katika mjadala huu. Kuna mashirika yanayouza umeme na hayo yausike katika masuala ya kuuza umeme kwa wateja. Endelezeni sekta binafsi na usikie kama mtu atashindwa kulipa umeme, simu au maji.

Serikali ya kuu inafanya vitu vingi ambavyo vinaleta matatizo katika kuendesha shughuli za kila siku za serikali. Na moja ya vitu hivyo ni UMACHINGA. Serikali kuwa kwenye usambazaji wa umeme ni UMACHINGA na haitakiwi kufanya biashara hiyo.

Mfumo wa serikali wa sasa haufahi kwa wakati tulionao. Sioni sababu ya waziri wa nishati na madini kutia mikataba ambayo athari zake zinawakuta wa mikoa inayotoa madini na faida inatumika kwa wachache wasiotoka katika mikoa hiyo.

Tanganyika ina kila kitu na maendeleo yetu hayakwamishwi na muungano. Arusha ilivyo na rasimali nzuri hakuna sababu ya mtu kuvaa mavaa ya jadi ili apate kazi ya ulinzi Zanzibar. Ukiona mtu anafanya hivyo ujue kuna itilafu kichwani.

Idadi ya wakazi wa Kinondoni ni kubwa kuliko ya wananchi wa Zanzibar. You must be absolutely nuts kufikiri kuwa wakazi milioni moja wa Zanzibar yanailetea matatizo Tanganyika yenye wakazi zaidi ya 34 milioni.
 
Back
Top Bottom