Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Unajua nimekuja kugundua hivi karibuni kuwa wazanzibari wengi ni wanafiki. Wakikaa na wazanzibari wenzao wanasema muungano hauna maana. Wakija bara wanasema muungano una maana sana. Sasa nadhani kama wazanzibari kweli wako serious watafute kwanza mtu anayewafaa hasa ndio wadai uhuru wao otherwise tutakuwa tunayasikia haya mambo kila siku but hakuna ambaye atakuwa tayari kusimama akatetea haki za wazanzibar. Sometimes nampa pongezi Seif Shariff kwa kuweza kusimama akasema yaliyo moyoni mwa wazanzibari but nikimuangalia uhusiano wake na SMZ ndio hapo narudi nyuma kuhusu uhuru wake wa maamuzi
Si hivyo! Hao unaowazungumza huwa daima wanajitenga katika kuitetea Zanzibar. Bilali amefanya hivyo, Shamsi amefanya hivyo kiasi cha kufutuka anapokuwa ndani ya Baraza la Wawakilishi wakati wenzake wanapotowa msimamo wao juu ya suwala la Muungano! Kundi la Bilali ni wale wasioitakia mema Zanzibar kwa manufaa yao ya kibinafsi. Hawa ni watu wanaoishi kwa chuki na fitina miongoni mwa Wazanzibari. Watu kama hawa hawastajabiwi kwani hata Bara wako kina Mrema.
 
Unajua nimekuja kugundua hivi karibuni kuwa wazanzibari wengi ni wanafiki. Wakikaa na wazanzibari wenzao wanasema muungano hauna maana. Wakija bara wanasema muungano una maana sana. Sasa nadhani kama wazanzibari kweli wako serious watafute kwanza mtu anayewafaa hasa ndio wadai uhuru wao otherwise tutakuwa tunayasikia haya mambo kila siku but hakuna ambaye atakuwa tayari kusimama akatetea haki za wazanzibar. Sometimes nampa pongezi Seif Shariff kwa kuweza kusimama akasema yaliyo moyoni mwa wazanzibari but nikimuangalia uhusiano wake na SMZ ndio hapo narudi nyuma kuhusu uhuru wake wa maamuzi

Wingi wa hao Wazanzibari unaowajuwa kuwa ni wanafiki ni kiasi gani kulingana na idadi halisi ya Wazanzibari? Wazanzibari wangapi wana nafasi ya kwenda Bara na kufanya mazungumzo na wa huko? Iwapo unazungumzia idadi ndogo ya Wazanzibari unaowajua wanakuja Bara basi hakuna shaka kuwa aidha wanapata faida binafsi kwa Muungano au labda wanakwambia hivyo kwa kuogopa kufukuzwa au kuguswa maslaha yao. Hili si liwe sawa na mfano wa msimamo wa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki? Mwapachu amefika hadi kuwaona wasomi wanaopinga ulaji wake kuwa viumbe wa ajabu.

Suwala la msingi si faida ya Muungano kama jitihada za kuleta umoja bali jee Muungano huo unamfaidia kiasi gani Mzanzibari wa kawaida asiekuja Bara (ambao ndio wengi). Kwa mfumo huu tulionao Wazanzibari wanaangushwa na umoja wa namna hii.
 
Indeed Ngekewa na hilo ndio tatizo wazanzibari wengi hawafaidiki na muungano. Kimsingi tatizo kubwa ni tuliungana vipi kati yetu na zanzibar. nikikumbuka wakati nasoma historia ilikuwa muungano huo ni kwa faida ya usalama wa zanzibar na ukumbozi wa zanzibar dhidi ya waarabu. Nilipo kuwa zanzibar nikakuta stori tofauti kumbe muungano ilikuwa for national security na woga wa Karume kuhofia kupinduliwa. Na kadri nilipokuwa nikiuchokonoa muungano nikakuta hata mawaziri wa SMZ hawajui kwanini wamungana na Tanganyika but wao ndio watetezi wakuu wa muungano. Sasa ikiwa muungano sababu zake hazijulikani unadhani utadumuje? Mie sitetei kuvunjika but ikibidi nadhani ni bora ukavunjika ili uundwe upya ukiwa na malengo yanayokubaliwa na pande zote mbili.

Ama sivyo ni bomu la muda linalosubiri kuripuka tu.
 
..utafiti wa Prof.Malyamkono na wataalamu wenzake ulibainisha kwamba Zenj inanyonya Tanganyika.

..someni hii habari hapa, pia mkitafute kitabu walichoandika ili mpate kujua jinsi Tanganyika yenu inavyonyonywa na Zenj.

ZANZIBAR A DRAIN ON UNION ECONOMY

The astronomical rise of Zanzibar’s financial dependence on the mainland government is the latest wave of criticism levelled at the Tanzanian union by leading academics.

They quantify the dependence at nearly 835 million US dollars in
transfers between 1983-84 and 1998-99 in a new publication, entitled
‘The Political Plight of Zanzibar’, launched after a two-year study in
the island.

“This, as the book points out, is equivalent to the mainland giving
every Zanzibari a gift of 1,202 dollars a year, or roughly five years
of Tanzania’s per capita Gross National Product,
” Teddy Maliyamkono,
the publication’s editor, says.

“It is also equal to the average total annual revenue of Zanzibar’s
government during the past six years,” he adds.

Further questions are raised as to why the Zanzibari constitution
refuses the semi-autonomous state to contribute to the union budget
although the union bore the expenses of supporting its annual balance
of payments deficit.

“By refusing to pay and making it their constitutional right not to,
Zanzibar is implicitly denouncing the union. Now the question is, why
is the mainland Tanzania paying a fortune to keep the union unless they
have an immeasurable intrinsic love for the people of Zanzibar!”
Maliyamkono, a political scientist, says in the book.

“It is argued in some quarters that the political and economic costs
of letting Zanzibar go on its own, could, by far, outweigh present
transfers and benefits which accrue to Zanzibar from the union,” he
adds.

Maliyamkono notes that the mainland sends much money to Zanzibar,
and subsidises its power consumption.

Some of the transfers, like smuggling, tax evasion and the money
sent into the island by Zanzibaris working on the mainland, are
invisible and cannot be quantified.

“From the economic point of view, there is no denying that it is
Zanzibar that needs the union more than mainlanders do. The union is
Zanzibar’s livelihood, there is no Zanzibar without the union,
” he
points out.

The political marriage of Tanganyika and Zanzibar in 1964 has been
plagued by a plethora of operational problems.

Zanzibar, which is heavily dependent on cloves to sustain its
economy, has been complaining that the mainland is benefiting too much
from the union and that it should, in the spirit of its ’sovereignty,’
be allowed to have its own flag.

But according to the authors of the book, there is no denying that
it is Zanzibar that needs the union the most.

Maliyamkono warns that dissolution of the union would be
 
Mwiba, choko choko mchokoe pweza, binadamu huta muweza!, hata kuku ukimchambua sana, utashindwa kumla! Hapa wataka tena kuuchoka Muungano halafu mkiambiwa ukweli, hamweshi kulia lia.

Ni kweli Zanzibar na Tanzania bara zinatakiwa kuuchangia mfuko wa Muungano, ikumbukwe Serikali ya Jamuhuri ya Muungano pia ndiyo ile ya Tanganyika, ila Zanzibar ndio yenye serikali yake.

Kama hapa tulipo, Zanzibar inatumia umeme bure, nani anayegharimia, ni serikali ya Muungano. Kama umeme tuu mnashindwa kulipa, itakuwa mtoe mchango kuchangia muungano?. Kwa uwezo upi nyie Zanzibar mlionao?!. Au ni hiyo jeuri ya mafuta ya kinibu ndio mtatumia mapato hayo kuuchangia mfuko wa Muungano?.

Na kama mfuko huo ungekuwepo, serikali ya Zanzibar ikatoa fungu kuuchangia, na serikali ya Muungano ikatoa fungu kuuchasngia kwa niaba ya bara, halafu hilo fungu likatumiwa na serikali ya Muungano kwa niana ya mambo ya Muungano, si ndio mgepiga kelele mpaka mbinguni kuwa mnanyonywa!.

Hoja ya Zanzibar ambayo ni kilio cha msingi, ni hoja kuhusu mgao halali wa Zanzibar ambao ingetakiwa kupata kutokana na misaada mbalimbali kwa Tanzania inayoipata toka kwa wafadhili na washitiri mbalimbali ambayo Tanzania inatia ndani.

Tukirudi kwenye issue za Muungano, kwa vile muungano huu unamatatizo kwenye structure, there is no way out, ni kukubali kubomoa na kujenga upya muungano imara, vingevyovyo tutaendelea kuziba nyufa na kutia viraka wee na bado nyufa zitaendelea mwishowe tutajenga ukuta.

Pasco naona umeingia kwenye mtego wa "Mpemba". Si mkikataa kuwa Zanzibar si nchi ndani ya Muungano? Kauli yako ni kukiri kuwa kuna sehemu mbili sawa kwenye Muungano huu.
Kuhusu mchango wa Zanzibar kwa Serikali ya Muungano, Zanzibar ina uwezo wa kutosha wa kuchangia sehemu yake hasa pale sehemu mbili hizi zikipewa nafasi sawa. Kwani Bara wana nini kikubwa cha kuwafanya waweze kuchangia sehemu yao? Ni nchi kubwa yenye mahitaji makubwa sana kuliko Zanzibar. Ni nchi yenye watu masikini zaidi kuliko walioko Zanzibar, na wanahitaji fedha nyingi kuwaondoa kwenye umasikini. Sasa fanya hesabu zako na utuambie hiyo jeuri ya Bara kuweza kulipa mchango wake wote inatoka wapi? Chukua mfano wa vyombo vya Muungano, jeshi, polisi na Mambo ya nje na uangalie kiasi gani Serikali ya Muungano inashindwa kuviendesha vizuri vitu hivyi. Jee Serikali inashindwa eti kwa kuwa Zanzibar haitowi mchango wake?

Kuhusu la umeme mbona mnashangaza sana. Si juzi tu tumesikia kutoka Baraza la Wawakilishi wakiuliza sababu ya Tanesco kupandisha umeme wa Zanzibar kwa asilimia kubwa kulinganisha na Bara? Kitu cha bure kimemfikisha Idrisa Rashid kutoleana maneno na viongozi wa Zanzibar kwa kutishia kuukata kutokana na kucheleweshewa malipo, ni malipo gani hayo iwapo umeme mnawapa bure?
 
..utafiti wa Prof.Malyamkono na wataalamu wenzake ulibainisha kwamba Zenj inanyonya Tanganyika.

..someni hii habari hapa, pia mkitafute kitabu walichoandika ili mpate kujua jinsi Tanganyika yenu inavyonyonywa na Zenj.

Mwandishi au mchunguzi wa habari hii aidha anapotosha makusudi au mipaka yake ya uchunguzi ni midogo sana. Kwanini uchunguzi wake umeanzia mwaka 1983 na usiende nyuma na kuona kiasi gani Muungano umesababisha kuifanya Zanzibar iwe katika hali yake ya sasa hivi? Kipindi kifupi tu kabla ya mwaka 1983 wakati wa vita vya Tanzania na Uganda ni kiasi gani Zanzibar iliporwa kugharamia vita?
Hili la utegemezi si la kweli kabisa kwani Zanzibar nje ya Muundo huu wa Muungano ina uhakika wa kujitegemea sana kwani kabla ya 1977 zanzibar ikijiendesha vipi? Mpaka sasa sijaona faida ya kusema Zanzibar haiwezi kujiendesha bila Muungano kwani hata suwala la Usalama kwani Zanzibar wakati wa Karume majaribio mangapi ya Mapinduzi yalizimwa na Wazanzibari wenyewe?
Nimekuwa nikiuliza kila siku na kukosa jibu! Hivyo Tanzania imeshawahi kukumbwa na balaa la njaa mara ngapi na kupokea misaada ya chakula kutoka nje mbona mara zote Zanzibar haipatiwi misaada hiyo? Kuna la faida zaidi kuliko kuwapatia wananchi huduma wakati wa maafa na Serikali ya Muungano inashindwa kuisaidia Zanzibar, huo utegemezi unaletwa na kitu gani?
 
Ngekewa,

..Zenj, ama hailipi umeme tanesco, au wanachelewesha malipo. ndiyo maana kila kukicha Zenj wana mgogoro na shirika hili. mwaka 2004 iliwalazimu Tanesco kukata umeme Zenj.

..majuzi kulikuwa na malalamiko huku Tanganyika kwamba wa-Zenj wanauziwa umeme kwa bei poa kuliko wenzao wa Tanganyika. yaani pamoja na serikali kuwahurumia kwa kuwauzia umeme kwa bei poa bado mnashindwa kulipa.

.
 
Joka Kuu naomba nitofautiane na wewe kwani huyo Professa anapotosha ukweli na figures zake. Ingelikuwa kweli anataka kufanya utafiti uliokuwa robust angelianzia from 1920 whereby zanzibar ilikuwa na private banking sectors na kulikuwa na economic sectors nyingi zilikuwa zinafanya kazi. Kaa ukijua kuwa Zanzibar miaka 1920 mpaka 1970 ilikuwa ikiwalisha Tanganyika. Kama umesahau wacha nikupe dokezo Zanzibar walikuwa the largest exporter wa spices, cloves pamoja bandari huru before mapinduzi. Figures za zamani zinaonyesha uchumi wa zanzibar ulikuwa kuliko Uganda, Kenya na Tanganyika (Cheki Wikipedia). Sasa labda tukuulize kilitokea nini kwa pesa za kigeni zilizokuwa zikipatikana zikaingia ndani ya mfuko wa muungano?

Na kama Ngekewa anauliza mbona misaada ikija Tanganyika Zanzibar hawapewi. Wao hawahitaji au wanajua wanajiweza. Kama ni hivyo inakuwaje huyu profesa anadai Tanzania Bara inawapa $1,200 wakati misaada hawapewi does it realy make sense. Waswahili husema ajizi nyumba ya njaa kama wana njaa basi kwanini wasipewe misaada zaidi zanzibar kama hawana kitu badala yake wanaachwa na njaa zao?
 
Ngekewa said:
Mwandishi au mchunguzi wa habari hii aidha anapotosha makusudi au mipaka yake ya uchunguzi ni midogo sana. Kwanini uchunguzi wake umeanzia mwaka 1983 na usiende nyuma na kuona kiasi gani Muungano umesababisha kuifanya Zanzibar iwe katika hali yake ya sasa hivi? Kipindi kifupi tu kabla ya mwaka 1983 wakati wa vita vya Tanzania na Uganda ni kiasi gani Zanzibar iliporwa kugharamia vita?
Hili la utegemezi si la kweli kabisa kwani Zanzibar nje ya Muundo huu wa Muungano ina uhakika wa kujitegemea sana kwani kabla ya 1977 zanzibar ikijiendesha vipi? Mpaka sasa sijaona faida ya kusema Zanzibar haiwezi kujiendesha bila Muungano kwani hata suwala la Usalama kwani Zanzibar wakati wa Karume majaribio mangapi ya Mapinduzi yalizimwa na Wazanzibari wenyewe?
Nimekuwa nikiuliza kila siku na kukosa jibu! Hivyo Tanzania imeshawahi kukumbwa na balaa la njaa mara ngapi na kupokea misaada ya chakula kutoka nje mbona mara zote Zanzibar haipatiwi misaada hiyo? Kuna la faida zaidi kuliko kuwapatia wananchi huduma wakati wa maafa na Serikali ya Muungano inashindwa kuisaidia Zanzibar, huo utegemezi unaletwa na kitu gani?

Ngekewa,

..mwaka 1983 Tanganyika ilikuwa na matatizo makubwa ya kiuchumi. sasa utafiti unaonyesha kwamba hata wakati huo bado tulikuwa tunawafadhili na kuwasitiri wa-Zenj.

..mimi nadhani ifike mahali wa-Zenj muwe na shukrani na heshima kwa msaada na fadhila tunayowapatia.

..Zenj imewahi kuwa na matatizo ya chakula. matatizo hayo ndiyo yaliyopelekea serikali ya Mzee Sheikh Idiris Abdul Wakil kuanzisha mpango wa kilimo uliopewa jina "mtakula."

..hakuna anayesema kwamba wa-Zenj hamna uwezo wa kujitegemea. kama Mauritius na Seycheles wameweza basi na nyie hamna sababu ya kushindwa.

..tatizo lenu ni kwamba mna uongozi mbovu usiokuwa na mbinu za kuwaletea maendeleo. hicho ndicho chanzo kikuu kinachosababisha Zenj u iwe tegemezi kwa wa-Tanganyika
 
Nakubaliana nawe katika uongozi mbovu Zanzibar but huo unasababishwa na siasa za kihafidhina za kina Shamhuna na wenzie kuleta ubaguzi kwa manufaa yao binafsi (ufisadi). Once wakiweza kuweka mazingira ya uongozi wenye uadilifu wanaweza kusimama wenyewe.

Ila napingana na wewe kuhusu zanzibar wawe na shukrani kwa kulishwa na Tanganyika. Labda mtuambie nani alikuwa akiwalisha Tanganyika miaka ya 70? Nani aliwakopesha pesa miaka 1960s? Pia hiyo miaka 1980s nyerere alikataa pesa za IMF na World kwa madai ya masharti magumu alipata wapi pesa za kuendesha nchi?
 
Mdondoaji said:
Joka Kuu naomba nitofautiane na wewe kwani huyo Professa anapotosha ukweli na figures zake. Ingelikuwa kweli anataka kufanya utafiti uliokuwa robust angelianzia from 1920 whereby zanzibar ilikuwa na private banking sectors na kulikuwa na economic sectors nyingi zilikuwa zinafanya kazi. Kaa ukijua kuwa Zanzibar miaka 1920 mpaka 1970 ilikuwa ikiwalisha Tanganyika. Kama umesahau wacha nikupe dokezo Zanzibar walikuwa the largest exporter wa spices, cloves pamoja bandari huru before mapinduzi. Figures za zamani zinaonyesha uchumi wa zanzibar ulikuwa kuliko Uganda, Kenya na Tanganyika (Cheki Wikipedia). Sasa labda tukuulize kilitokea nini kwa pesa za kigeni zilizokuwa zikipatikana zikaingia ndani ya mfuko wa muungano?

Na kama Ngekewa anauliza mbona misaada ikija Tanganyika Zanzibar hawapewi. Wao hawahitaji au wanajua wanajiweza. Kama ni hivyo inakuwaje huyu profesa anadai Tanzania Bara inawapa $1,200 wakati misaada hawapewi does it realy make sense. Waswahili husema ajizi nyumba ya njaa kama wana njaa basi kwanini wasipewe misaada zaidi zanzibar kama hawana kitu badala yake wanaachwa na njaa zao?

Mdondoaji,

..hata kama utafiti wa Prof.Malyamkono haukwenda as far back as 1920 bado hiyo siyo sababu tosha ya kuupuuza mchango wake.

..lakini kwa tabia ya wa-Zenj ya kupenda kubisha na kupotosha kila kitu, hata ukiwaletea utafiti wa toka mwaka 1920 wataukataa na kudai mbona haujaenda as back as 1700 miaka ambayo Zenj ilikuwa ikikamata watumwa huku Tanganyika!!!

..madai kwamba Zenj ilikuwa inawalisha wa-Tanganyika sijui unayatoa wapi. binafsi sikumbuki wakati wowote ule ambapo Zenj imewahi kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula ktk eneo la Afrika Mashariki.

..ni kweli kwamba kabla na mara baada ya Mapinduzi Zenj ilikuwa na akiba kubwa ya fedha za kigeni. lakini hata huku Tanganyika hali ilikuwa hivyohivyo, mkoloni aliacha akiba ya fedha za kigeni. tatizo lilojitokeza ni serikali zote mbili kuanzisha social services nyingi bila kuwa na uchumi ulioimarika wa kuweza kubeba majukumu hayo mapya. vilevile kuanguka kwa bei ya mazao ya karafuu na katani kulisababisha uchumi wa Zenj na Tanganyika kuyumba kwa kiasi kikubwa.
 
Mdondoaji said:
Ila napingana na wewe kuhusu zanzibar wawe na shukrani kwa kulishwa na Tanganyika. Labda mtuambie nani alikuwa akiwalisha Tanganyika miaka ya 70? Nani aliwakopesha pesa miaka 1960s? Pia hiyo miaka 1980s nyerere alikataa pesa za IMF na World kwa madai ya masharti magumu alipata wapi pesa za kuendesha nchi?

Mdondoaji,

..miaka ya 60 na 70 tulikuwa tunajilisha wenyewe. miaka hiyo uzalishaji wa katani/mkonge,kahawa,na pamba, ulikuwa mzuri. pia tulikuwa tunakopesheka, na mazingira ya kupewa misaada yalikuwa mazuri. Tanganyika iliweza kuhimili ile oil price crisis ya miaka ya 70 kwasababu na sisi tulikuwa na ka-coffee boom ketu hapa.

..nchi za Scandinavia ndizo zilizokuwa zikitusitiri wakati Mwalimu Nyerere analumbana na IMF miaka ile ya 80. kipindi hicho pia Zenj ilikuwa tayari ni choka mbaya na aliyeokoa jahazi ni Mzee Ruksa aliyefungua milango ya uagizaji Zenj. hata wakati wa Mzee Idiris Wakil Zenj ilikuwa na matatizo ya uzalishaji chakula ndiyo maana ukaanzishwa ule mpango wa kilimo ulioitwa "mtakula."
 
Nyinyi watanganyika na serikali yenu nakupeni changamoto ya wazanzibar wengi, ambao hawataki muungano huu wa kindumilakuwili, ikiwa kweli mna yakini kuwa muungano huu ni imara, fanyeni referendum kwa zanzibar tu muwaulize, WANAUTAKA au HAWAUTAKI?
Sina shaka matokeo kama yale ya ERITREA NA ETHIOPIA 1990s yatatokea, sina shaka kabisa.
 
Junius said:

Junius,

..Zenj mtapiga kura hivi karibuni kama mnataka serikali ya mseto ama la.

..pia Baraza la Wawakilishi limeshapitisha azimio kuondoa suala la mafuta kwenye muungano.

..sasa sijui kwanini mnaogopa kutamka ndani ya baraza la wawakilishi au bunge la jamhuri kwamba hamtaki muungano, au mnataka kura ya maoni kuhusu muungano.

..Muungano siyo priority ya wa-Tanganyika walio wengi. uwepo, au usiwepo, maisha yao hayataathirika kwa kiwango kikubwa.
 
Mdondoaji,

..miaka ya 60 na 70 tulikuwa tunajilisha wenyewe. miaka hiyo uzalishaji wa katani/mkonge,kahawa,na pamba, ulikuwa mzuri. pia tulikuwa tunakopesheka, na mazingira ya kupewa misaada yalikuwa mazuri. Tanganyika iliweza kuhimili ile oil price crisis ya miaka ya 70 kwasababu na sisi tulikuwa na ka-coffee boom ketu hapa.

..nchi za Scandinavia ndizo zilizokuwa zikitusitiri wakati Mwalimu Nyerere analumbana na IMF miaka ile ya 80. kipindi hicho pia Zenj ilikuwa tayari ni choka mbaya na aliyeokoa jahazi ni Mzee Ruksa aliyefungua milango ya uagizaji Zenj. hata wakati wa Mzee Idiris Wakil Zenj ilikuwa na matatizo ya uzalishaji chakula ndiyo maana ukaanzishwa ule mpango wa kilimo ulioitwa "mtakula."

Mkuu una uhakika gani kwamba Tanzania Bara ilikuwa na reserve kubwa ya fedha za kigeni (niliwahi kuzifatilia figures BOT nikakumbana na vikwazo vingi mpaka leo). Zanzibar inasemekana ilikuwa the leading exporter wa cloves plantation na spices. wanasema zanzibar ilikuwa ina supply 75% of global production of cloves duniani!!! je mauzo ya cloves yameenda wapi mpaka 1978???. Tuje katika bandari huru ilikufa baada ya muungano Tanganyika je kwanini? Mwisho tunamalizia na kuuliza hebu tupe habari zanzibar waliwahi kuwa na njaa hebu tufafanulie zaidi maana sikumbuki...
 
Mdondoaji,
Mkuuu wangu usisikie habari ya kuambiwa. Zanzibar haijawahi kuilisha Bara hata siku moja. Kumbuka tu kwamba miaka ya 60 na 70 Zanzibar ilikuwa na pato kubwa sana la Karafuu ikiwa moja ya nchi chache sana duniani zinazozalisha. Sasa GDP yake ilipanda kutokana na uuwiano wake na population less than millioni moja,hivyo usifikirie walikuwa wakipata mabillioni ya kulisha bara kwani mkoa wa dar tu ulikuwa ni mara 10 ya population ya Zanzibar yote..Na Uchumi wa Zanzibar ulikuja anguka wakati bei ya karafuu ilipodondoka vibaya sana na yasemekana tatizo lilikuwa Nyie wenyewe kuuza mbegu kwa mataifa ya Asia ambao walianza kuzalisha Karafuu kwa wingi na kwa bei nafuu..Hili siliamini sana.

Ila nachoweza kukwambia ni kwamba wakati Zanzibar inashamiri kwa Karafuu, bara pia tulikuwa juu ktk kuuza katani (second in the world), kahawa na Pamba na hata ukitazama data beteewn 1960 hadi 1975 uchumi wetu ulikuwa ukikua kwa asilimi 7 hadi 10. record ambayo hatujaifikia na sidhani kama tutaweza kuifikia tena. In the 60's tulikuwa ktk Jumuiya ya Africa mashariki (EAC) tukitumia fedha moja hivyo huwezi kuzungumzia uchumi wa Zanzibar kuendesha Bara kwa karafuu..comeon now!

Hata hivyo bidhaa hizi pia zilikuja shuka thamani baada ya vitu hivi kuzalishwa kwa wingi toka nchi za South America na Asia. Hivyo, uchumi wa nchi za kiafrika ulishuka ghafla na kwa bahati mbaya ndio wakati huo huo depression ya 1980 ikaingia baada ya mafuta kupanda juu..Hata uchumi wa US ulikuwa una collapse vibaya kama sii Reegan kuja na mbinu mpya..
 
So Mkandara kulikuwa na equal distribution of income from Zanzibar na Tanzania Bara according to maneno ulioyasema. Sasa kwanini inaonekana kama zanzibar inabebwa? Na hata kama sasa haichangii kwani isiachiwe zanzibar ikaendelea na mambo yake Tanzania Bara ikawa imepunguza mzigo mmoja mkubwa?
 
Mdondoaji,

..pesa zilikuwa zinafujwa huko huko Zenj na viongozi wenu.

..umesahau kashfa ya Aboud Jumbe kununua presidential jet wakati kuna uhaba wa chakula?

..unaifahamu kashfa ya matumizi ya fedha kwa ajili ya ranchi ya Makurunge?

..kinachosababisha Zenj kuwa na hali ngumu ya kiuchumi ni kukosa "plan b" baada ya kuanguka kwa biashara ya karafuu.

..badala ya kutafuta solution ya matatizo yenu mnasingizia kila kitu muungano. umeme mnapewa bure lakini haijulikani mnautumia kwa shughuli gani ya kiuchumi.

..
 
Back
Top Bottom