Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Huu muungano una faida kwa ccm pale waZanzibar wanapowapigia kura kutuchagulia sisi rais otherwise haina faida nyingine
 
Hakuna muungano usio na faida tatizo ni kwamba una mapungufu mengi na tangu mwanzo malengo yake hayakuwa wazi mambo yake mengi hayajadiliwi kwa uwazi na ukweli.
Kwa maoni yangu mimi naona tatizo liko hapo.
 
Nyie Faida hamuioni? hamuoni ZNZ wana taifa wakati Tanganyika haipo? hamuoni watu chini ya milion 2 wanawachimba mkwara watu mil 40 wote mnafyata? hamuoni faida wakati wa ZNZ wanawaongoza wa Bara wakati wa bara ni makurufu kwa mtu wa Bara kuwa kiongozi wa siasa ZNZ.

Nyie hamuoni faida wakati katika mchakato wa katiba mpya maamuzi yote lazima wakubaliane Raisi wa ZNZ na Raisi wa Tanzania sasa napata shaka Bara wao nani anakubali kwa niaba yao?


Aaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhh FAIDA ZIPO BANA acha UVIVU WA KUFIKIRI
 
na hata bado! c mnajifaNya kujua. 2015 rais wa znz na watanganyika aka Tanzania wote watatoka zenj, hapo ndio mtajuwa nyerere alizidiwa mere na karume.
 

sio siri,hizi ni faida hasi au hasara kwa lugha nyingine,aibu tupu,tatizo tuliibia taratibu za muungano badala ya watu kujadili kwenye mdahalo.

Mi naona tuwaache tu wazanzibari wajinafasi,hata FIFA wanawabania uanachama wa makupe sie kuwang'ang'ania. Tuwaache,waasisi walishakufa na muungano wao tuanzeupya,inawezekana walikurupuka tu kuungana hakuna hata mmoja anayeweza kuhadithia faida yake
 
mimi ni mfuasi na muumini mkubwa wa Hayati Mwalimu Nyerere. Bila yeye na sera zake nisingekuwa hapa nilipo. Lakini kwa hili la muungano natofautiana naye. Kama nitabahatika kuiona Tanganyika imefufuka kabla sijafa nitakwenda kaburini kwa amani. Muungano una faida kwa wazanzibari na hasa viongozi. Kwa sisi waTanganyika ni bugudha tupu kila kukicha.
 

Mkuu umenitia hasira sana yaani nimetamani kwenda pale magogoni nakuwafurumusha mjengoni na kuwapigisha kwata wote halafu wanavunja kichefuchefu muungano
 
Katika hili acheni kumlaumu Nyerere na Karume (wote hawakuwa wanasheria). Huu Muungano uliletwa kwa nia safi na kwa udugu-sawa na hulka za watu wakati huo, hakukuwa na majungu au mauzauza mengi.
Ilibidi kila wakati ulipoendelea tuurudie na kusawazisha mapungufu yake. Leo tungekuwa na kitu kizuri. Lakini uvivu wa kufikiri, personal interests, uchu nk ndio vimetufikisha hapa.
Napendekeza: kwanza kuwepo kura ya maoni, Tanganyika na Zanzibar. Kura hiyo isiulize wapenda au hupendi, bali iulize namna gani ya muungano wataka? Watu wengi hawajui hata vipengee vya sasa vya Muungano. Mimi niko dhidi ya kuvunja Muungano, lakini naunga mkono ukarabati mkubwa wa muungano- au hata serikali moja.
Mara nyingi Muungano unapovunjika, mahali pake pachukuliwa na chuki na hata vita.
 
Binmgeni umenfurahisha, Nyerere kazidiwa nini na Karume? Lol!

Anyway ebu tuacheni izi chuki pembeni na ukweli usemwe. Tanganyika inafaidika na muungano na kutokana izo faida chache basi ni muhimu kuliko wanavyonufaika na wazanzibar. Mi mwenyewe mzenji mnatwita urojo, mdebwedo na maneno mengine ya dharau. Lakini mwisho wake mnaonekana nyinyi ndi mdebwedo na urojo, kama alivosema jamaa Tanzania inachimbwa mkwala na watu milioni 2, ata mbunge wa chadema kalisema ilo na nnakubaliana nae, Zanzibar ya urojo ndio kizuizi cha mambo mengi ya Tanganyika Sembe! Na msipolitizama mtajikuta kuwa aloyataka Nyerere yatamgeukia, jamani simameni muidai Tanganyika!
Na alosema kuwa Zanzibar nchi amekosea, twende UN tutafute bendera na uwakilishi wa Zanzibar, Zanzibar na Palestine bora palestine angalau inatambulika km ni watu wanaodai utaifa Sisi Zanzibar hatujafika ata EAC kudai utaifa.
Anyway nlioneshwa sheria flani za international about kumiliki bahari basi nkaona kuwa Tanganyika inafaidika apo because sheria imeipa nguvu kisiwa kumili eneo kubwa la bahari, manake umiliki wa bahari Tanganyika ni mdogo kwa sababu visiwa vya Zanzibar vipo karibu na bahari ni milki yao, hapo nlijua kwanini nyerere alisema kuwa kama angekuwa na uwezo angeliviondoa visiwa hivyo!
Mnasema kuwa mnaibeba Zanzibar, sijafaham apo mana mi naona kula cha Zanzibar kinafanywa na Zanzibar yenyewe! Tena mwaibeba vipi? TRA nao wanakula hela za zanzibar, mana inakuaje ulipe ushuru mara 2? Zanzibar ulipe na Dar ulipe heh! TRA imeambiwa iweke account 1 kwa TRA zote zilizopo then about 14% am not sure iende Zanzibar, hilo limepungwa!!
Kuna watu wanasema kuwa wabara hawapewi ardhi unguja, hilo ni uongo, hamujatembea znz, ukienda Shamba utakuta wenye kumiliki na wenye hela zao hununua majumba ama kukodi nyumba zanzibar. Wengine wanasema Biashara za wabingo Zanzibar zinachomwa moto, hebu jiulize kwanini zinachomwa moto? Unajenga Bar na kuharibu watoto wa watu unategemea wazazi wafanye nini?
Waznz waliopo Dar wanajiendesha wenyewe na huskii biashara zao zikichomwa moto because hawajishuhulisha katika mambo ya kipuuzi kama Bar na kuuza wanawake.

Kuna watu wanafikiria kuwa Znz bila ya Muungano haitafika mbali, zanzibar itafika mbali tena sana, Zanzibar ndo ilokuwa the Gate to Africa, freeport, biashara ilikua Znz ndo penyewe asa!,,, msitutishe bureee, Serikali ya Tanzania ni ya Tanganyika!
 
Itumieni vizuri tena kabla haijatiwa mkononi na Mzanzibari afu akawa hayumbishwi, mtakuja kukosa yote mwisho!
Ata hamfikirii, Uzanzibari hautokufa hata kidogo, utanganyika umekufa, Taifa lenu mmelifuta direct lakini la Zanzibar limebaki na litaendelea kubaki, sisi tunavitambulisho vya uzanzibar, na tutakua na vya utanzania, je wenzangu vya kitanganyika mnaaaavo? Eee amkeni mdai serikali yenu!
 
Hii nchi ni tanganyika na sio Tanzania bara,pia muungano uvunjwe hata leo hiiiiii sioni faida ila hasara tupu.
 
Unatusaidia kuweka maadui mbali na pwani yetu kwa Dar es salaam. Tuna mahali pa kuweka majeshi yetu!!

Labda hilo tu, vingenevyo hauna faida yoyote zaidi ya kuongeza gharama za uendeshaji na malumbano yasiyo na tija.
 
Mtanganyika akienda kufanya kazi ya sanaa Zanzibar atatozwa 20,000 hamuoni kama hiyo ni faida? Waulizeni wasanii wa Bongofleva watawaambia
 
Chilubi hakuna aliyesema Zanzibar itakufa,kuishi mtaishi tu kama ambavyo mafia wanavyoishi pamoja na kutelekezwa na serikali,hata comoro na shelisheli wanaishi. Watanganyika tunaumia dhihakaza wazanzibar kama Jussa na wenzake. Kama umeme mtauziwa kama tunavyonunua Uganda na Zambia. Tuachane tu kama ni ndoa basi,ila mnatunyonya,kwa nini mnajiita minority,eti nafasi kidogo,mzanzibar awepo kama usawa wa wanawake kwenye system,kwa nini huko Znz mbara hapewi upendeleo?kero tu
 

kuhusu bahari, hebu chukua ramani ya Tanzania, angalia kuanzia Tanga kushuka chini mpaka mtwara Tanganyika ina kiasi gani cha bahari, halafu angalia kuelekea mashariki zaidi kwenda bahari kuu Tanganyika ina kiasi gani!. Tukivunja Muungano, Tanganyika bado ina bahari ya kutosha tu, kwa uvuvi na usafiri!.
Wazanzibar wanaweza kumiliki ardhi Tanganyika kiurahisi kabisa, na pia wanaweza kugombea nafasi za uongozi Tanganyika, je Watanganyika wananufaika na nini?
 
Kwavile hatujui historia ya upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika na Zanzibr ndiyo maana tunataka Muungano uvunjike, nawadokeza kidogo:-
1. Muungano ulikuwa kwaajili ya kulikumbuka taifa la awali lililoundwa mwaka 1885 ambalo ndilo lililotoa waasisi wa uhuru wetu ila historia yetu ya upatikanaji uhuru wetu hatujaikamilisha ndiyo maana tunapata taabu ju ya hili.
2. Muungano ungekuwa wa serikali moja kama tulikokua tunaelekea haya yasingekuwepo.
3. Mwisho tutafute namna ya kujitambua sisi na taifa letu tukizingatia historia ya uwepo wa mataifa yetu mawili na jamhuri yetu bila ya mashinikizo ya nje kisha tujipange upya tufike tunakokwenda, la sivyo tutanyang`aywa dhahabu na wajanja kisha tupewe jiwe tushangilie kama mazuzu sasa, baadae tulalamike kama tufanyavyo kwenye miliki za vyetu, elimu, ajira, viwanda nk.
 
Unatusaidia kuweka maadui mbali na pwani yetu kwa Dar es salaam. Tuna mahali pa kuweka majeshi yetu!!

this is no longer relevant now.

with the current high-tec millitary-wares, adui anaweza akawa atlantic ocean na bado akaibonda magogoni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…