Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Faida za muungano ni kwa wazanzibari kupata mahali pa kufanyia biashara na kuzaliana sana kuliko kwao ukiachia mbali kubebwa katika kila jambo.
 
Jadi ndo nasema wabara muudai utanganyika kama sisi tunavoudai Uzanzibari, nyerere alitaka kuifuta Zanzibar moja kwa moja na alikua na nia mbaya,lakini goma limemgeukia yeye ameifuta Tanganyika moja kwa moja na Serikali pia inaelekea Znz, mkikaa na ukimya wenu Serikali ya TZ itakua inaongozwa na Mzenji,,,, mtapokonywa kila kitu, kaeni tu.

Kuhusu bahari Zanzibar ina haki kubwa sana kwenye suala ilo, bahati mbaya sheet lenye iyo sheria lipo mbali now.

Mpayukaji kweli umepayuka, Zanzibar munaibeba katika nini hasa ebu naomba uyataje! Na suala la kufanya biashara, itabidi tuulize, viwanja kariakoo alokuwa anaviuza hasa ni nani? Wabara wenyewe ndo wauzaji sasa unamlaumu nani? Au unamjua mznz alopewa kiwanja na serikali bure bure tu? Ndo hayoooo ya kudanganya watu, wapalestina walikuwa wanauza viwanja kwa waizraili waliposhtuka goma limekula kwao, zanzibar maebeo ya pwani mengi wamiliki ni wazungu saiv na wauzaji ni wazenji, sasa nani alaumiwe mpayukaji?

Suala la Muungano limeanza kuwaka moto pale Pinda aliposema znz ni mkoa na suala la mafuta hapo kibanda cha muungano kikaanza kuunguwa,,,,
Mnaogopa nn kusema ukweli? Mi mzenji na ukweli nasema na nawaambia wazenji kuwa znz si nchi, znz inazuia maamuzi ya tanganyika, znz ina upendeleo ktk maamuzi, lakini znz katika serikali ya Muungano haimo, serikali ya muungano ni ya TANGANYIKA!!!! wazenji tushalia na Sitta ameshuhudia znz haitaki muungano, amekosewa kupigwa Sitta na wazenji, muswada ulichanwa mbele yake, lakini wabara mmefanya nini kuonesha kama hamuutaki muungano?
 
mpaka ss tz bara tuna zaidi ya miaka 45 ya muungano na visiwa vya pemba na unguja, ss tz bara tunafaidika nn hasa na huu muungano? Binafsi sioni sbb ya kuendelea kuwa nao. Naomba mowazo chanya zaidi

Kwa mawanzo yangu ni kuwa hilo lako ni domo kaya tu. Waulize CDM wakupe silaha ya kutangaza msiyoyapenda.
 
Faida za muungano ni kwa wazanzibari kupata mahali pa kufanyia biashara na kuzaliana sana kuliko kwao ukiachia mbali kubebwa katika kila jambo.
Faida ya Muungano ni nyinyi kujengewa majengo ya kistaarabu na Wapemba na kutoka mabara kuja kuyashangalia maghorofa mkiwaachia Wahindi kuishi na kutanua.
 
Hakuna muungano usio na faida tatizo ni kwamba una mapungufu mengi na tangu mwanzo malengo yake hayakuwa wazi mambo yake mengi hayajadiliwi kwa uwazi na ukweli.
Kwa maoni yangu mimi naona tatizo liko hapo.
Sio lazima kila muungano uwe na faida, na kwa watanganyika huu muungano ni hasara tupu. Hiyo hoja ya usalama ni dhaifu sana maana kuna nchi ziko karibu na visiwa kama sao tome, cape verde na hata comoro lakini ziko salama na wala hazijalazimisha muungano.
 
Kwavile hatujui historia ya upatikanaji wa uhuru wa Tanganyika na Zanzibr ndiyo maana tunataka Muungano uvunjike, nawadokeza kidogo:-
1. Muungano ulikuwa kwaajili ya kulikumbuka taifa la awali lililoundwa mwaka 1885 ambalo ndilo lililotoa waasisi wa uhuru wetu ila historia yetu ya upatikanaji uhuru wetu hatujaikamilisha ndiyo maana tunapata taabu ju ya hili.
2. Muungano ungekuwa wa serikali moja kama tulikokua tunaelekea haya yasingekuwepo.
3. Mwisho tutafute namna ya kujitambua sisi na taifa letu tukizingatia historia ya uwepo wa mataifa yetu mawili na jamhuri yetu bila ya mashinikizo ya nje kisha tujipange upya tufike tunakokwenda, la sivyo tutanyang`aywa dhahabu na wajanja kisha tupewe jiwe tushangilie kama mazuzu sasa, baadae tulalamike kama tufanyavyo kwenye miliki za vyetu, elimu, ajira, viwanda nk.
Kama ishu ilikuwa kukumbuka taifa la 1885 mbona hawakuungana na rwanda na burundi?
 
Ukiunganisha Hydrogen na Oxygen unapata Maji. Hiyo nayo ni faida mojawapo ya muungano.
 
mpaka ss tz bara tuna zaidi ya miaka 45 ya muungano na visiwa vya pemba na unguja, ss tz bara tunafaidika nn hasa na huu muungano? Binafsi sioni sbb ya kuendelea kuwa nao. Naomba mowazo chanya zaidi

Mi Naona Mungano ni kiza tu Kwa sababu Wa Zanzibar siku zote story zao ni kuuvunja muungano tu kila wakiamka wanawaza nini wafanye zaidi mpaka wafanikiwe kuuvunja Muungano.
kama kweli na sisi Wa Tanganyika tunataka kuuvunja Muungano lazima tuwe na sauti moja kama Wa Zanzibari basi kwa hilo tutafanikiwa kuirudisha Tanganyika yetu:A S 465:
 
Sio lazima kila muungano uwe na faida, na kwa watanganyika huu muungano ni hasara tupu. Hiyo hoja ya usalama ni dhaifu sana maana kuna nchi ziko karibu na visiwa kama sao tome, cape verde na hata comoro lakini ziko salama na wala hazijalazimisha muungano.

ki ukweli naona ni bora zaidi tungewachia Wa Zanzibari wajitoe katika muungano wabake na visiwa vyao kama vile majirani zao Comoro, Seychelles, Mauritius, Reunion na Madagasca...visiwa hivyo vyote viko huru hawajawahi kufanya Muunganowowote ule na kila kisiwa kina kiti chake ndani ya United Nation kama ilivyokuwa Zanzibar 1963.

Tubakishe Ujirani Mzuri hata kiuchumi na mambo mengine vile vile lakini kila nchi iwe na taifa lake huru:juggle:
 
Halafu mimi watanganyika wanaoenda kuishi Zenji wananiudhi sana!!
Ondokeni huko!...
Na sisi tuanze kuwatimua huku.
Wakenya nao wote waondoke!!, kama wanataka bahari or whatever let'em have it!
Just leave us the hell alone!!, they are soft anywayz!
 
jamani faida ya muungano anayo raisi katika sherehe za kitaifa. Utakuta kabla ya kuingia katika sherehe lazima watangulie wadogo zake kwamza. Anaanza naibu katibu mkuu wa chama bara halafu znz! halafu anakuja, waziri kiongozi! halafu waziri mkuu watanzania! halafu makamu wa raisi tanzania bara, makamu wa raisi visiwani, katibu mkuu wa ccm, raisi wa zanzibari halafu baada ya dakika ishirini za kusubiri anatokea raiasi wa tanzania na mwenyekiti wa cc tanzania!!

Yaani hapo raisi wa tanzania anaonekana ni mtu mziiiiitoooo ile mbaya! ni ujiko huooo, . hii ndio faida kubwa ya muungano! zaidi ya hapo , ki uvhumi ni hasara kubwa saana saana , mpaka inatisha ! ndiyo nchi pekee africa, tanzania ina tawaliwa na viongozi kumi na moja kwa wakati mooja . hasara ya kuwalipa mishahara na misafara yao ya mabodigadi wao ni mara nne ya kujenga hospitali na kuweka rami mitaa sita!

sasa tufanyeje? lazima tuandika katiba mpya. Katiba itakayokomesha uwiano sawa kati ya tanganyika na zanzibari. Katiba itakayoyotoa raisi mmoja kutawala bara na visiwani. katiba itakayofuta baraza la wawakilishi, waziri kiongozi na makamu wa raisi zanzibari. Kama nchi tajiri marekani wameweza kufuta ulaji wa maraisi 55 kabla ya kuungana, je sisi tushindwe nini? huo ndio muungano, la sivyo watanganyika na wazanzibari, tutaishia kutukanana kama machizi mpaka kuja kuchinjana wenyewe kwa wenyewe kwa sbabau ya kumuogopa nyerere , eti fikira zake bado ni sahihi!!!!!!

Nyerere alijua kabisaakuwa Ujamaa na kujitegemea hautakufa wala siasa za kikomunisti. Uhuru wa maoni ya watu lazima serikali iuheshimu, na huu ndio wakati mwafaka wa kujenga Tanzania imara kama milima ya kimara!!
 
muungano hauna faida yoyote ile kwa watanganyika zaidi ya kutufanya kuwa watumwa wa ccm. mataifa makubwa kama urusi yameshndwa kuwa na muungano alaf sisi tunajisifu kuwa tunaudumisha muungano kumbe ni upuuzi tupu na kuonyesha ufinyu wa kufikiri kwetu sisi watanganyika . ikitokea nikawanauwezo wa kuongoza nchi hii basi kazi ya kwanza ni kuondoa uchafu unaoitwa muungangano na hizo mnazoita mbio za mwenge
 
SOBY utakereka kwa sana tu, wanahama bara uku because mtu huna peace of mind kabisa, hamna ustaarabu hata kidogo, watu wabapiga rusha roho mtaani mpk alfajiri bila kujali kama wanakera wenzao, watu wanafata ustaarabu visiwani bara hakuna ustaarabu, kwa hili hamuwezi kubishaaa! SOBY we might be soft but toi bad tumewatawala kiakili, saivi bungeni likija suala la muungano basi wazenji ndo wanaosikilizwa zaidi, unafikiri kula sembe ndo utamtisha mtu? Muhimu utumiaji wa akili na sio maguvu yasiyona maana!

Ngekewa ametoa moja safi, tunawajengea majengo ya ustaarabu mjini na tunawapa Ajira!!! Hamna shukrani kweli!!
 
Faida zote zimo katika kiinyume ya zile hoja zote za Wapinzani wa Muungano wa dola mbili huru.Wakizisahau hisia butu za
"Usisi/Utanganyika" na "Uwao/Uzanziibari" au kuwacha hisia butu za "Uvisiwani dhidi ya "Ubara" na badala yake kuboresha
na kuudhibiti Utanzania,wenye misingi ya jadi ya kitamaduni na ya Kihistoria ,faida zipo wazi kabisa,haihitaji kua na darubuni.

Wapinzani wa Muungano,wanafaidika kwa kuwepo Muungano ; kinacho watiya upofu na kutowea kusikia ni ushupavu wa
siasa mgando za urithi wa hisia za kubaguana .Watakapo uathiri uzuri na faida za Muungano na kuupoteza ndipo watakapo
jitafuna ulimi - kwa majuto. Wazanzibari wakijitowa,"Wavisiwani watatafuta na Wabara",hiyo itafuatiliwa na kutafutana baina
Wazaramo na Wahaya/Wachaga huko Dar-es-salaam,hiyo itafuatwa na baina ya "Wapemba na Waunguja" -mviriongo
mbovu huo utasambaa katika miji mingine na vijijini - jee itakuwa na mwisho ?

Faida zaidi ni hii amani na maendeleo ya kujivunia - ingawaje bado upo uhuni na ufisadi - bora nusu ya shari kuliko ile
shari ya kamili kama zile zinazotokea katika nhi jirani .
 
Ni JK kutaka kurejea madarakani 2015 kwa sura ya H.Mwinyi, Shein
 
Hakuna kitu.Manungana nchi mbili halafu tena mnazaa nchi mbili--hii nimeona Tanzania peke yake.Halafu kila Tarehe 9 Desemba mnasheherekea uhuru wa nchi isiyokuwepo ambayo aliyeivunja (Marehemu) hakupenda hata kuisikia (Na wasiwasi kama hakuwa Mnyarwanda manake Mtanganyika wa kweli asingekubali hilo) jina lake likitajwa.Billioni 64 walizotupa zingeweza kumaliza kipande kilichobaki cha barabara ya Bagamoyo-MSATA na kutupunguzia foleni barabara ya Morogoro.Hakuna kitu kinachoitwa TANZANIA BARA--- ndo maana waandaji mpaka leo wanaficha huo mkataba wa Muungano.IKITOKEA NAPATA URAISI CHA KWANZA NAVUNJA MUUNGANO ILI KILA MTU AWE NA UHURU WA KUJIAMULIA MAMBO YAKE.MUUNGANO HUU WA MTU NA MKE KUDEKA HAUNA FAINA MWENYE KUZIJUA AJIMWAGE HAPA AZIWEKE HADHARANI
 


Faida kubwa kuliko zote ni kuwazuia Waunguja na Wapemba wasichinjane. Full Stop.
 
Back
Top Bottom