Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

ni sisi watanganyika pamoja na umaskini wetu kuwapa wapemba ardhi bwelelele na kuhudumia wabunge lukiki toka zanzibar magari ya kifahari na posho nyingi ili wawakilishe wanzanzibar kwenye masilayi yao,umaskini mwigine bwana tunajitakia wenyewe
 
Chama Cha Mapinduzi CCM kimekua kikijishushia heshima kutokana na tabia yake ya kuweka maslahi ya chama mbele hata pale yanapo kinzana na maslahi ya taifa. Hii inajidhihirisha pale wanapotumia uwingi wao bungeni kupinga hoja zote zilizo kinyume na matakwa ya chama hata kama ni za manufaa kwa mwanachi. Katika muendelezo wa tabia hii chafu, chama hiki kimekua kikiutetea muungano unaoonekana kuwa mradi binafsi "private project" wa chama hiki tawala pamoja na kuwa na kero lukuki kwa wananchi hususan wa Zanzibar.

Sasa kutokana na ari ya wananchi kutaka kizifikisha tamati sera za kizandiki za CCM, inayokua sikuhadi siku siku inawalazimu viongozi wa chama hiki kusambaza taarifa potofu juu ya hatma ya wananchi wa pande moja ya muungano walio hamia pande nyingine iwe kibiashara, makazi, nk. Viongozi hawa wamekua wakikaririwa wakisema kuwa eti wananchi wengi wa bara wameji-establish unguja "and vice versa", wengine wamezaliana hivyo muungano ukivunjika itakua tabu kwa watu hawa!

Hawataki kuzungumzia tatizo halisi ambalo ni muungano wa kisiasa na kiuchumi. Ninacho taka kusema ni kwamba muungano wa kijamii sio kitu kinaweza kuvunjwa kwa makubaliano ya kisheria, wahindi wangapi wapo wamelowea hapa nchini ilhali tanzania haina muungano na India, halikadhalika waarabu pamoja na wachina wanaozidi kumiminika, tujiulize watanzania wangapi wamelowea nchi za ulaya na hutuna muungano na nchi hizo! Baada ya kuvunjika Sudan wananchi walipewa fursa ya kuchagua aidha South Sudan au North na maisha yanaendelea.


Muungano huu usio na faida (wa iuchumi na kisiasa) ukivunjika wanachi walio upande wa pili wa muungano watapewa fursa ya aidha kuchagua kubaki au kurudi upande wao wa asili. Maisha yataendelea kama kawaida isitoshe kero zilizopo ni sawa tu na nchi mbili tofauti! Watu wamechoshwa na vitendo kama vya TRA kutoza kodi bidhaa Across pande mbili za muungano, ushirikishwaji mdogo wa wananchi wa Zanzibar ktk maswala ya muungano, the list is endless!

Ni hayo tu!
 
serikali tatu ndio suluhisho

Serikali ya Tanganyika yenye makao makuu Dodoma

Serikali ya Zanzibar yenye makao makuu Unguja

Serikalu ya ndogo ya JMT yenye makuu Dar es Salaam.

Kelele zote zitaisha
 
serikali tatu ndio suluhisho

Serikali ya Tanganyika yenye makao makuu Dodoma

Serikali ya Zanzibar yenye makao makuu Unguja

Serikalu ya ndogo ya JMT yenye makuu Dar es Salaam.

Kelele zote zitaisha



Serikali tatu kwa faida ya nani? Kwa nini tusivunje muungano wenyewe? Una faida gani kwa bara au visiwani? Huu ulikuwa muungano wa Karume na Nyerer,sasa wote wamekufa, ni vyema na muungano wao ukawafuata.
 
Serikali tatu kwa faida ya nani? Kwa nini tusivunje muungano wenyewe? Una faida gani kwa bara au visiwani? Huu ulikuwa muungano wa Karume na Nyerer,sasa wote wamekufa, ni vyema na muungano wao ukawafuata.

Muungano hautavunjika huo ni national pride; muundo utabadilishwa period..kwa faida ya taifa na wananchi wake..
 
NITAFURAHI SANA TUKIWA NA SERIKALI 1, KULIKO MUUNGANO UVUNJIKE ALAFU MAGAIDO WAJAE ZNZ BORA IJE VITA! Hivi kwa nini Nyerere hakuunganisha ikawa nchi 1?
 
Re: Ccm na upotou juu ya kuvunjika kwa muungano
NITAFURAHI SANA TUKIWA NA SERIKALI 1, KULIKO MUUNGANO UVUNJIKE ALAFU MAGAIDO WAJAE ZNZ BORA IJE VITA! Hivi kwa nini Nyerere hakuunganisha ikawa nchi 1?


Hahahahah ndoto hii ilimshinda babenu Julius K. Nyerere. Pale ilikuwa rahisi kuuwa Zanzibar, leo wenzenu wameamka.hahhahaahah
 
Muungano hautavunjika huo ni national pride; muundo utabadilishwa period..kwa faida ya taifa na wananchi wake..


Hakuna national pride kwenye huu muungano wa wafu. Wenyewe wameshakufa sharti na muungano wao ufe. period
 
Serikali tatu kwa faida ya nani? Kwa nini tusivunje muungano wenyewe? Una faida gani kwa bara au visiwani? Huu ulikuwa muungano wa Karume na Nyerer,sasa wote wamekufa, ni vyema na muungano wao ukawafuata.
Comrade punguza jazba kidogo ndg yng kuungana ni jambo jema kabisa na kuungana si kutokutofautiana tofauti za mapishano lazima ziwepo kusolve hizo tofauti ndio ukomavu wa Muungano.
Serikali 3 yaweza kuwa sulruhisho
 
Wazanzibar hawataki muungano na makongamano/semina/warsha zinaendelea kwa fujo visiwani, nyie endeleeni na upinzani wenu feki watawasuprise mwaka huu.
 
Nimekuwa nimefikisha umri nilokuwa nao sasa nimekuwa nikisikia watu wanawalaumu sana watu wasiotaka muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa ni wasaliti, lakini mimi binafsi huwa sielewi kwa nini hawa watu hutukanwa na hukejeliwa. Nilivokuwa mtoto nilifikiri huu muungano ni sawa na kumuabudu mungu kwamba endapo basi utakwenda kinyume na mungu utakiona cha moto lakini mawazo ya ki utu uzima yalivonijia nikagundua kuwa no, hiki ni kitu cha kawaida na kimefanywa kwa makubaliano tu na watu wa dunia hii. Sasa sielewi kama mimi mtanganyika sioni faida ya muungano nisiseme uvunjwe ili tuishi bila kelele toka kwa wenzetu wazanzibar?

Samahani kama kuna mtu anazijua faida amabazo sisi watanganyika tunazipata kutokana na muungano huu naomba anieleweshe.
 
Kama hujui faida basi ungetueleza hasara za Muungano kwani kinyume chake ndio faida zake.
 
Hakuna faida yoyote ya Muungano,zaidi sana ni Tanganyika kubeba mzigo usio wa lazima.
 
big,hands,small,feet-ae3bcb9f5dd5a88cde306865ca021603_i.jpg


Poleni Watanganyika, kulea kuna bughdha zake!
Katoto unakapakata lakini duh, kanakunyea!
Lakini hakakawii kulialia myee, ukikatelekeza!
 
Wakati wa Chama kushika hatamu ulipita zamaaani! Sasa hivi Watanzania wameelimika na wanajua nini ni nini mambo ya kupeana miongozo hayapo tena. Suala la Katiba ni la watu binafsi na siyo la kivyama. Kila mtu atatoa mawazo yake binafsi. Kama lingekuwa la vyama basi wangekusanya vyama vya siasa na kwenda kupata maoni.
 
Kimsingi hali inaonesha kuwa tunahitajika kama Watanganyika kupata nafasi ya kuzungumza misingi yetu kama Watanganyika. Tunajivunga kwa kufikiri tunakuwa wema kwa kutoonesha ukweli kuwa nasi tunakereka kwa kuonekana kama ving'ang'anizi wa Muungano.

Pamoja na kuwa Rwanda na Burundi wanajiunga na EAC, bado wanajiunga kama Taifa kamili wanaoweza kusimamia social and economic position zao bila mashaka ya kuulizwa na mwingine nje ya mipaka ya uhuru wao wa kitaifa.

Kwangu naona ni wakati kwa kupitia mabadiliko ya Katiba kuruhusu mawazo ya kupata mwelekeo, ikibidi Taifa la Tanganyika ili hata Wapemba na Waznz wanaoishi hapa waishi wakijua tunajitambua na kuthamini Utanganyika wetu pamoja na kuwa hatuna mpango wa kuwabagua wala kuwanyima ajira kama wanavyofanya.:A S-fire1:
 
Zanzibar hatutaki hata huo muungano wa mkataba,
Wabara waondoke huku zanzibar na tutawafukuza wote, wanyonyaji wakubwa!
 
Back
Top Bottom