Jadi ndo nasema wabara muudai utanganyika kama sisi tunavoudai Uzanzibari, nyerere alitaka kuifuta Zanzibar moja kwa moja na alikua na nia mbaya,lakini goma limemgeukia yeye ameifuta Tanganyika moja kwa moja na Serikali pia inaelekea Znz, mkikaa na ukimya wenu Serikali ya TZ itakua inaongozwa na Mzenji,,,, mtapokonywa kila kitu, kaeni tu.
Kuhusu bahari Zanzibar ina haki kubwa sana kwenye suala ilo, bahati mbaya sheet lenye iyo sheria lipo mbali now.
Mpayukaji kweli umepayuka, Zanzibar munaibeba katika nini hasa ebu naomba uyataje! Na suala la kufanya biashara, itabidi tuulize, viwanja kariakoo alokuwa anaviuza hasa ni nani? Wabara wenyewe ndo wauzaji sasa unamlaumu nani? Au unamjua mznz alopewa kiwanja na serikali bure bure tu? Ndo hayoooo ya kudanganya watu, wapalestina walikuwa wanauza viwanja kwa waizraili waliposhtuka goma limekula kwao, zanzibar maebeo ya pwani mengi wamiliki ni wazungu saiv na wauzaji ni wazenji, sasa nani alaumiwe mpayukaji?
Suala la Muungano limeanza kuwaka moto pale Pinda aliposema znz ni mkoa na suala la mafuta hapo kibanda cha muungano kikaanza kuunguwa,,,,
Mnaogopa nn kusema ukweli? Mi mzenji na ukweli nasema na nawaambia wazenji kuwa znz si nchi, znz inazuia maamuzi ya tanganyika, znz ina upendeleo ktk maamuzi, lakini znz katika serikali ya Muungano haimo, serikali ya muungano ni ya TANGANYIKA!!!! wazenji tushalia na Sitta ameshuhudia znz haitaki muungano, amekosewa kupigwa Sitta na wazenji, muswada ulichanwa mbele yake, lakini wabara mmefanya nini kuonesha kama hamuutaki muungano?