Chama Cha Mapinduzi CCM kimekua kikijishushia heshima kutokana na tabia yake ya kuweka maslahi ya chama mbele hata pale yanapo kinzana na maslahi ya taifa. Hii inajidhihirisha pale wanapotumia uwingi wao bungeni kupinga hoja zote zilizo kinyume na matakwa ya chama hata kama ni za manufaa kwa mwanachi. Katika muendelezo wa tabia hii chafu, chama hiki kimekua kikiutetea muungano unaoonekana kuwa mradi binafsi "private project" wa chama hiki tawala pamoja na kuwa na kero lukuki kwa wananchi hususan wa Zanzibar.
Sasa kutokana na ari ya wananchi kutaka kizifikisha tamati sera za kizandiki za CCM, inayokua sikuhadi siku siku inawalazimu viongozi wa chama hiki kusambaza taarifa potofu juu ya hatma ya wananchi wa pande moja ya muungano walio hamia pande nyingine iwe kibiashara, makazi, nk. Viongozi hawa wamekua wakikaririwa wakisema kuwa eti wananchi wengi wa bara wameji-establish unguja "and vice versa", wengine wamezaliana hivyo muungano ukivunjika itakua tabu kwa watu hawa!
Hawataki kuzungumzia tatizo halisi ambalo ni muungano wa kisiasa na kiuchumi. Ninacho taka kusema ni kwamba muungano wa kijamii sio kitu kinaweza kuvunjwa kwa makubaliano ya kisheria, wahindi wangapi wapo wamelowea hapa nchini ilhali tanzania haina muungano na India, halikadhalika waarabu pamoja na wachina wanaozidi kumiminika, tujiulize watanzania wangapi wamelowea nchi za ulaya na hutuna muungano na nchi hizo! Baada ya kuvunjika Sudan wananchi walipewa fursa ya kuchagua aidha South Sudan au North na maisha yanaendelea.
Muungano huu usio na faida (wa iuchumi na kisiasa) ukivunjika wanachi walio upande wa pili wa muungano watapewa fursa ya aidha kuchagua kubaki au kurudi upande wao wa asili. Maisha yataendelea kama kawaida isitoshe kero zilizopo ni sawa tu na nchi mbili tofauti! Watu wamechoshwa na vitendo kama vya TRA kutoza kodi bidhaa Across pande mbili za muungano, ushirikishwaji mdogo wa wananchi wa Zanzibar ktk maswala ya muungano, the list is endless!
Ni hayo tu!