Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Waarabu wanataka kutuvamia watupore madini, gesi na wanyamapori wetu--si unakumbuka wamewahi kutuibia twiga na mpaka leo hawajaturudishia wanyama wetu hao? Chezea mwarabu wewe!
Okay, walipowaibia hao Twiga Waarabu walikuwa wameingia kutokea Zanzibar?

Waarabu wanataka kuwaibia madini? Hivi Barrick Gold wanavyokomba haya madini kama majambazi walipitia Zanzibar? Muarabu akuibie gesi, hebu nikuulize... hizo gezi sisi zimetusaidia nini mpaka Muarabu azitemee mate?

Eti tumeshikilia Muungano ili tusije kuibiwa twiga na Muarabu! Jamani, how preposterous is that? Muarabu kaja kuiba twiga kapitia airport humu humu Tanganyika, yani vi sababu vya Muungano ridiculous sijapata kuona
 
Android 00,
Hao wapemba waliopo ulaya hawatuhusu. Wapemba tunaozungumzia ni hawa walioko hapa Tanganyika.
 
Wakuu, baada ya kuangalia sarakasi mbalimbali kuhusu muundo wa muungno wetu, nimeona ni vema tukabainisha faida zitokanazo na muungano huu kwa pande zote mbili. Hii itatupatia mwanga kuweza kujua ni muundo upi utafaa ili kuweza kunufaika na hizo faida.

Pia si mbaya tukitazama na hasara zake, kama zipo, ili tuweze kulinganisha na kutoa maamuzi bora. Tuchangie kwa kuzingatia uhalisia na sio mitazamo ya kisiasa.

Mimi naanza na faida kwa upande wa Zanzibar; umepanua wigo wa kibiashara. Wazanzibari wanafanya biashara Tanganyika kwenye soko kubwa bila vikwazo vyovyote. Pia watangnyika kwa upande wao wanakwenda kutalii Zanzibar bila visa za kitalii
 
Huu muungano feki tushaukataa, nasema tena hatuutakiiiiiiiii, akili yako ndo imegota hapo ukaona hizo ndo faida kubwa sana kwako, hivi kwa akili yako hizo faida ulizozitaja tukiwa nje ya muungano hatuwezi kuzipata!? Mbona nchi za jirani kama Kenya na Congo hizo fursa unazoziita faida tunapata, kwani wao tumeungana!? Something is wrong in your coconut, sorry to burst your wonderful bubles
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
 
Badala ya kushughulikia maendeleo yetu tunapoteza muda na resources kuhangaikia eti kero za muungano, mara serikali 2/1/3. Kuachana kabisa na hii kitu ndio njia pekee kwa ujirani mwema kati ya Tanganyika Zanzibar.
 

Umemaliza? Mbona hizi hata uki-copy na ku-paste kwa uhusiano wa Congo, Rwanda, Kenya etc ndo hizo hizo tu? Toa faida tuelimike sie tumesikia kila mwanaSerikali akiulizwa faida za muungano wao ni kuoana na kufanya biashara. Kumbuka pia sie tumeoa waKenya, wanyaRwanda kibao
 
kwa watanganyika:-
  • kupata ajira kwenye sekta ya utalii znz
  • makahaba wa kitanganyika kufaidika na zenji yenye makahaba wachache.

Kwa wazanzibar:-
  • kupata soko kubwa la biashara
  • kupata ardhi kubwa kwa uwekezaji kirahisi kuliko mgeni
  • kupata makazi
  • Kufaidika na ardhi sehemu mbili za muungano.
  • Kuweza kupata ajira za kibunge kwa wingi( jimbo moja znz lina watu elfu 2 angali tanganyika lina mapaka watu laki 4) dar yenye watu mil 6 ina wabunge 4, angali znz yenye watu mil 1 ina wabunge 80 ndani ya bunge la muungano
  • kupata fursa ya kuwa waziri znz au Tanzania.
  • kufaidika na polisi na jeshi ambalo hawalilipii
  • kufaidika na kodi ndogo ya mizigo bandarini angali mkataba wa muungano uliainisha kama bandari ni swala la muungano.
  • Kuringia utaifa wao na kuwa na kigezo cha kudharau wengine.
 

Mkuu, hoja yangu ni kutaka kuelewa kama kuna haja hasa ya kuwa na muungano huu. Kuna fauda zipi hasa? Kwa nini baadhi waung'ang'anie japokuwa umeshikizwa kwa super glue?
 
huo muungano wako haujawahi kuwa na faida, hauna faida na hautakuwa na faida zaidi ya kutuletea shida tu. kila mtu ajenge nyumba yake bwana, anayewapenda sana wazanzibar basi ahamie huko
 
faida kubwa ya muungano kwa mtanganyika ni kwamba atakwenda zenji kwenye honey moon.tatizo la faida hii CCM wanaogopa kusema
 
Faida za muungano kwa mujibu wa Prof Shivji ambaye kanunuliwa na chama cha magamba. Ile hotuba yake ya upotoshaji imejaa unafiki. Hakuna suala la hasara na faida kabla hatuja-establish muungano nini? Yale maandishi yenye sign ya Mwl Nyerere ya ku-forge? Nina hoja na Shivji angalau nitoe yangu kama ifuatavyo. Tanganyika ni mzimu unaowafanya CCM na ma-darling wao waweweseke kama wana majini. Shivji anajaribu kucheza na jargon za kinadharia tu na kwa aina ya vijana wale wenye upeo finyu wa kuutafuta UKWELI kama ilivyo ndani ya CCM, sioni kwa nini wasiungane naye.
Shivji kama mabarakala wenzake wanaiogopa sana Tanganyika kwa sababu wanazozijua wao. Tanganyika ni kuleta uwazi ndio maana wahafidhina wote wanaiogopa. Wakati shivji Anahalalisha Uzanzibar eti upo karne mbili za akina Seyyed Said na ukoo wake na kwamba Utanganyika ni ukoloni. Hivi huyu Shivji ndiye yule wa dialectical materialism au amegeuka wa dialectical idealism (Hegelian?). Ni wazi kama unaukubali uzanzibar wenye asili ya ukoloni wa Waarabu sharti ukubali Utanganyika japo ni wa ukoloni wa kingereza. Unaogopa nini kuukubali ukweli huu.
Serikali tatu Shivji anasema inaamsha na kushawishi hisia za Utanganyika, na, pili, kufanya watu wa Tanzania Bara wawachukie wenzao wa Zanzibar.(kifungu hiki kilikuwemo kwenye hotuba ya JK Dodoma, nadhani kuna ubia kati ya JK na Shivji). This is obvious huwezi kufuta awareness ya Watanganyika kwa kuficha ukweli wa historia kwamba Tanganyika ilikuwepo na itaendelea kuwemo kwenye historia. Eti kuwepo hadharani kwa Tanganyika inahatarisha muungano badala ya kuuimarisha. Ni ajabu prof anashindwa kuelewa muungano wa watanganyika na wazanzibar haukuanza 1964 kwa Articles of Union. Hivi Karume, Mwinyi, Moyo, Kisasi, Mfaranyaki, Mwakanjuki, nk. ni wenyeji wa wapi? Hao na wengine wengi wana asili ya Tanganyika na historia inatueleza hivyo. Shivji mwenyewe ana asili ya Zanzibar akahamia Morogoro (kama ilivyo kwa Wahindi na Wazanzibar wengi ambao wako Tanganyika) kabla ya 1964. Watu hao bila kujali articles of union za 1964 wanaendelea kuhusiana kijamii, kibiashara, kiuchumi, kuoana nk. Huu ndio muungano wa kweli ambao hauhitaji serikali mbili, moja, tatu, au nne. Na Shivji ansema muungano wowote hauwezi kudumu, au kudumu kwa amani, kama hauna mizizi katika watu na hisia zao. Nani kamwambia shivji eti Watanganyika na Wazanzibar hawana hisia za kushirikiana? Kinachoendelea Dodoma ni ya wanasiasa na kwa kuwatumia vibaraka wao kama akina shivji na wenzao kama visemeo(ndio maana Shivji anamnukuu Kikwete au Kinyume chake) - eti Tanganyika itaamsha nationalist tendencies, kwani Zanzibar hakuna nationalist tendencies? Kwa nini kwa Tanganyika iwe dhambi kuonyesha utaifa wao?
Shivji anawatisha vijana eti Na Utanganyika wenu hautadumu kwa sababu mtaanza kudai sasa Jamhuri ya Makonde na Jamhuri ya Sukuma! Mtakuwa vipande vipande. Shivji usitishe na kudanganya vijana hao. Hivi ni vitisho; Mmakonde kaolewa Moshi, msukuma kaoa Tanga, Mmatengo kaolewa Musoma, Mmasai kaolewa Mbamba Bay, Mwera kaolewa Mbeyya nk. Mhehe anaishi Kilwa, Mkaguru anaishi Kigoma nk. Suala la jamhuri hizi za Shivji za kufikirika ni alinacha za prof. za mchana. Kutumiwa ni kubaya, unaweza kuhadhirika na heshima yako kama prof wangu anavyojidhalilisha. Shivji anatoa mifano hai mbele yetu ya Somalia imesabaratika, Libya pia, Sudan, Afrika ya Kati, na nchi nyingine nje ya Afrika – Afghanistan, Pakistan, Syria, Iraq bila kutaja nchi za Ulaya. Hapo tunazungumzia muungano wa Tanzania, lakini mifano ya Shivji haihakisi context na historical conditions za Tanzania. Anaficha ukweli kwamba anachoshabikia yeye ndicho kilichofanya nchi hizo zisambaratike. Yaani kutumia gilba kulinda utaifa, kutumia udikteta katika kufanya maamuzi ya kitaifa kama CCM wanavyofanya, kukataa kusikiliza hoja za walalahoi (ambao kwa kipindi kirefu Shivji amekuwa mtetezi wao).
With due respect najua prof bado yeye kama mwanazuoni anapenda kuchochea mijadala ya kitaaluma ambayo kimsingi haiwezi ku-address practical problems za muungano. Na mwanasiasa atakayechukua ushauri aupeleke kufanyiwa kazi ajihakikishie anatumbukiza taifa katika mtafaruku. Na ndoto ya kupata katiba mpya haitakuwa kweli. Napenda kuungana na Mzee Msekwa aliyesema kuwepo kwa idadi yeyote ya serikali sio hoja maana muungano utakuwa imara ilimradi kuna political will. Je hawa wanasiasa (JK na CCM type) Shivji anawatetea anawajua wana nia gani? Kama Shivji anataka mfano hai akamwulize Prof. Mihanjo na Mukama na dossier la pendekezo lao la CCM kujivua gamba limeishia wapi. Chezea wanasiasa wa CCM wewe!
 
Jamani muungano uwepo tu ila tukiruhusu serikali tatu tujue tutakuja leta matatizo hapo baadaye
 
Jamani muungano uwepo tu ila tukiruhusu serikali tatu tujue tutakuja leta matatizo hapo baadaye
ladyfurahia, huoni kama huu muungano kwa jinsi ulivyo tayari ni tatizo kubwa? Umesema muungano "uwepo tu." Je, ungependa uweje?
 
Last edited by a moderator:
huo muungano wako haujawahi kuwa na faida, hauna faida na hautakuwa na faida zaidi ya kutuletea shida tu. kila mtu ajenge nyumba yake bwana, anayewapenda sana wazanzibar basi ahamie huko

Wabara kupata ajira kwenye mahoteli visiwani sio faida? Vipi kupata nafasi kusoma chuo kikuu Zbar? Vifaa used vya kielektroniki vinapatikana kwa bei chee Zbar.
 
ningependa muungano uwepo ndani kwa ndani yaani tanganyika iwe na nchi yake na zanzibar iwe na nchi yake ila isiwe na marais wala mawaziri wawepo viongozi tu wa kawaida na pawepo sasa na tanzania ambayo itakuwa na rais pekee atakakuwepo pande zote mbili kwanini nasema hivi nchi ya zanz ilishauzwa siku nyingi na koloni hivyo pakiwepo na seirikali 3 kutatokea vita si unaona mwenyewe huko pande za visiwa

ladyfurahia, huoni kama huu muungano kwa jinsi ulivyo tayari ni tatizo kubwa? Umesema muungano "uwepo tu." Je, ungependa uweje?
 

Nchi mbili, serikali moja? Mkuu sijakupata vema.
 

hao waznz ndio hawataki muungano. unataka waendelee kuuwa wakristo huko viziwani? na viongozi wa uamsho kuwatukana watanganyika?
 
Maoni yalishatolewa kama hukutoa umechelewa maana sio muda wake sasa bunge liniafanya kazi yake iwe ya hovyo au ya kweli litafanya kaziz yake; mhimu nachukulia kama maoni yako tena ya mtu aliyechelewa so useless labda kama kutakuwa na katiba mpya ingine kama hii ikishindikana kwa jinsi inavyoonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…