Habari zenu wanaharakati na wadau mbalimbali,
Nimejaribu kufatilia huu muungano wetu, mpaka sasahivi bado sijapata kujua faida zake hasa kwa watu wa upande wa bara, mwanzo nilijuwa kwamba muungano ni swala litakalotufanya tuwe kitu kimoja.
Yaani mwingiliano wetu usiwe wa kuhojiwa, lakini kinachoonekana ni sawa na ndoa ya watu wawili ambapo mwanamke akiihitaji vitu vya mme anachukua tu, ila mme anapohitaji vitu vya mke lazima atongozwe upya ndo apewe.
Haiwezekani ndani ya muungano kuishi Zanzibar lazima uwe na kitambulisho cha uzanzibari, haiwezekani mizigo kutoa bara bei chee lakini kutoa Zanzibar ushuru ni mkubwa kiasi hiki, achilia mbali mauza uza ya katiba mbili na mabunge mawili yaliyopo, mimi nataka nieleweshwe faida wazipatazo wanaichi wa kawaida ni zipi?
Mi nilijuwa muungano kufanya watu wawe kitu kimoja, yaani iwe sawa kama ulivyo kwa mtu wa bara avukapo kwenda visiwa vya Ukerewe ama Kigamboni.
Naomba mtu anifahamishe hivi ni faida gani zilizopo kwenye muungano huu hadi watu wanaung'ang'ania.?
Nataka kujua tafadhali maana hata nikikumbuka vile matokeo ya urais Zanzibar yalivyofutwa kwa ubatili halafu ya muungano yakawa halali wakati wapiga kura ni walewale na siku ya uchaguzi ilikuwa ni ile ile, wasimamizi walikuwa ni walewale, nini siri na faida ya muungano huu.
Naomba kujuzwa tafadhali.