Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Kwa manufaa na faida yetu sote, muungano lazima uwepo, kinachotakiwa kutatua changamoto tu.
 
Kwa manufaa na faida yetu sote, muungano lazima uwepo, kinachotakiwa kutatua changamoto tu.

Sio lazima, muungano ni jambo la hiyari ni jambo letu wenyewe, jambo la lazima ni kumuabudu alie kuumba
 
Habari zenu wanaharakati na wadau mbalimbali,

Nimejaribu kufatilia huu muungano wetu, mpaka sasahivi bado sijapata kujua faida zake hasa kwa watu wa upande wa bara, mwanzo nilijuwa kwamba muungano ni swala litakalotufanya tuwe kitu kimoja.

Yaani mwingiliano wetu usiwe wa kuhojiwa, lakini kinachoonekana ni sawa na ndoa ya watu wawili ambapo mwanamke akiihitaji vitu vya mme anachukua tu, ila mme anapohitaji vitu vya mke lazima atongozwe upya ndo apewe.

Haiwezekani ndani ya muungano kuishi Zanzibar lazima uwe na kitambulisho cha uzanzibari, haiwezekani mizigo kutoa bara bei chee lakini kutoa Zanzibar ushuru ni mkubwa kiasi hiki, achilia mbali mauza uza ya katiba mbili na mabunge mawili yaliyopo, mimi nataka nieleweshwe faida wazipatazo wanaichi wa kawaida ni zipi?

Mi nilijuwa muungano kufanya watu wawe kitu kimoja, yaani iwe sawa kama ulivyo kwa mtu wa bara avukapo kwenda visiwa vya Ukerewe ama Kigamboni.

Naomba mtu anifahamishe hivi ni faida gani zilizopo kwenye muungano huu hadi watu wanaung'ang'ania.?

Nataka kujua tafadhali maana hata nikikumbuka vile matokeo ya urais Zanzibar yalivyofutwa kwa ubatili halafu ya muungano yakawa halali wakati wapiga kura ni walewale na siku ya uchaguzi ilikuwa ni ile ile, wasimamizi walikuwa ni walewale, nini siri na faida ya muungano huu.

Naomba kujuzwa tafadhali.
 
Kwani muungano huu ulifuata vigezo kuundwa hakuna mwananchi wa Zanzibar wala Bara alieshirikishwa kutoa maoni kama wameridhia nchi hizi ziungane ama, na ndiyo maana mpaka leo watu wanatafuta makubaliano yaliyofanywa kisheria kwa nchi hizi kuungana hakuna inapooneka...Kwa hiyo twaweza sema ni Muungano uliofanywa na Wazee wetu walale pema pepon(Karume na Nyerere) inasemekana Karume alikubali kuungana haraka kwa ajili ya hofu ya kupinduliwa na John Okello.
 
manuu,

Kutumia Mazingira ya sasa kutafsiri hali ya miaka iliyopita ni kuganzisha akili.
Muungano wa United Kingdom ni miongoni mwa miungano kongwe zaid Ulimwenguni lakin hawakufanya kura za maoni!
Mkutano wa Berlin uliogawanya na kuunganisha baadhi ya maeneo tunautambua na kuuheshimu japo hatukufanya kura za maoni wala kuwakilishwa na Mtu yoyote.

Muungano wa Kilimanjaro na Mbeya kuifanya Tanganyika ulipata ridhaa ya wachaga na wanyakyusa? Muungano wa Unguja na Pemba ulipigiwa kura ya maoni? Iweje Mjerumani Bismack awe sahihi kuunga na kugawanya maeneo yote bila ya kura za maoni halafu iwe haramu kwa Julius Nyerere na Abeid Karume?
Kabla ya kutafuta uhalali wa Tanganyika kuungana na Zanzibar tueleze kwanza uhalali wenyewe wa unification ya Tanganyika yenyewe na Zanzibar kwa kuwa zenyewe hazikufuata utaratibu unaotaka ziufuate walipoungana.
 
Faida yake ni sisi bara kuendelea kuitawala zanzibar mpaka wazanzibari watakapoamua kumwachia nchi maalimu seif
 
Faida ni nyingi sana
1. Njia muruwa ya kuimeza Zanzibarr
2. Njia nyepesi ya kuwaibia mchana bila ya wao kupiga kelele
3 Tutahodhi vitalu vya mafuta na gesi pamoja na mali asili ya bahari kuu
4 Tutaudhibiti uislamu kuzidi kuenea bara kwa kuwakuwadhibiti maimamu wao
5 kuzuwia ugaidi

6 kuwasimikia viongozi tunaowataka tu
 
dmkali,
Ndugu dmkali
Muungano una faida moja kubwa nayo ni kuwapatia wananchi "maisha bora"(kuwagawia wananchi wa Tanganyika na Zanzibar umasikini).
Kama unapojiuliza kuhusu faida tuseme husikii , macho je huna ya kuona faida hiyo?

Faida ya pili ni kuhakikisha chama cha M kinatawala walalahoi na wadanganyika wa nchi zilizongana kwa hiari na si mtutu ili mapenzi ya bwana yatimizwe.





Link Jecha alitumwa na nani kufuta matokeo ya Uchaguzi Zanzibar
 
Kivip mkuu, ebu fafanua
Watatukaribia sana wale jamaa, hata wazungu hawana mchechetó na cuf kuingia madarakani, moto ungekuwa mkali kama wangekuwa chadema, saa hizi tungekuw chini ya vikwazo
 
Kutumia Mazingira ya sasa kutafsiri hali ya miaka iliyopita ni kuganzisha akili.
Muungano wa United Kingdom ni miongoni mwa miungano kongwe zaid Ulimwenguni lakin hawakufanya kura za maoni!
Mkutano wa Berlin uliogawanya na kuunganisha baadhi ya maeneo tunautambua na kuuheshimu japo hatukufanya kura za maoni wala kuwakilishwa na Mtu yoyote. Muungano wa Kilimanjaro na Mbeya kuifanya Tanganyika ulipata ridhaa ya wachaga na wanyakyusa? Muungano wa Unguja na Pemba ulipigiwa kura ya maoni? Iweje Mjerumani Bismack awe sahihi kuunga na kugawanya maeneo yote bila ya kura za maoni halafu iwe haramu kwa Julius Nyerere na Abeid Karume?
Kabla ya kutafuta uhalali wa Tanganyika kuungana na Zanzibar tueleze kwanza uhalali wenyewe wa unification ya Tanganyika yenyewe na Zanzibar kwa kuwa zenyewe hazikufuata utaratibu unaotaka ziufuate walipoungana.
Mkuu zile zilikuwa nchi mbili tayari Tanganyika na Zanzibar na wrote ni wanachama wa UN sasa ukiniletea wachaga na wanyakusa mm sikuelewi ni nchi mbili zilizo jitambua
 
Back
Top Bottom