Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

dmkali, kijamii, muungano wetu ni wa asili...mbagamoyo, kiudugu yuko karibu zaidi na muunguja, kupita mbara mwenzie wa ukerewe....na ktk hali yoyote mahusiano baina ya wa bagamoyo na waunguja, yana faida kubwa kwao, kupita ya wabagamoyo na wa Ukerewe. Lakini siasa na mawazo ambayo msingi wake ni kuutukuza ukoloni (ukoloni wa wazungu wa kikristu ktk bara,na ukoloni waarabu wa kiislam ktk zanzibar), imekuwa ni fitna inayotia upofu kuiona kweli, na faida za muungano.

Leo hii mfano, (very sad) mtu, mwanasiasa ambae kwa asili ni muhindi tu ambae amejaaliwa na Mungu kuzaliwa Zanzibar, ni sehemu ya wenye fikra za kuleta jeuri yenye lengo la kusaliti maamuzi ya "wazawa" huru, kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...lkn pia kuna sampuli ya watu wa aina hiyo hata ktk bara, ati wakiamini kuna faida kubwa kweli, ktk muungano wa mfyomi wa manyara, na mbagamoyo,yanayozidi mahusiano yote yakimuungano kati ya mbagamoyo na muunguja..
 
Mkuu zile zilikuwa nchi mbili tayari Tanganyika na Zanzibar na wrote ni wanachama wa UN sasa ukiniletea wachaga na wanyakusa mm sikuelewi ni nchi mbili zilizo jitambua

Rudi darasani kajifunze Tanganyika na Zanzibar zilianzaje? Kama kuwa Mwanachama wa UN ndio kigezo tusihoji basi hata Tz sasa ni mwanasiasa wa UN basi tusihoji
 
Faida kuu ya muungano ni kuifanya CCM iendelee kutawala.
 
Kuna Mzee mmoja alishawahi kuniambia kuwa endapo Zanzibar itajitenga na muungano basi kuna kitu kinaitwa mikataba ya sultani kuhusu mipaka ya Zanzibar akaniambia hiyo mikataba ikifuatishwa basi eneo lote la dar,tanga bagamoyo ,mkoa wa pwani yote itakuwa chini ya Zanzibar kutoka na hiyo mikataba ya kisultani na ndio maana kamwe Tanganyika haiwez kukubal hilo litoke,huyo Mzee aliyeniambia hayo ni mpemba na ni daktari wa hospital moja hapa Mwanza.cna uwakika ktk hili
 
Return2roots,
Mbona sikuelewi,kama unayoongea unaona ni point,kwanini tusiungane na Burundi kwani Waha na Warundi ni ndugu na wana maingiliano ya karibu mno au Wamanayema wa Tanzani na wale wa Kongo,tusijustfy kwa arguments ambazo ni illogical
 
walimu wa Civics leo siku ya mapumziko(Jumamosi)

tuambieni yale mnayowaambiaga wanafunzi juu ya faida za muungano
 
Hakuna asiyejua, sema wanasiasa wanatafuta maslahi yao binafsi
 
Mbona sikuelewi,kama unayoongea unaona ni point,kwanini tusiungane na Burundi kwani Waha na Warundi ni ndugu na wana maingiliano ya karibu mno au Wamanayema wa Tanzani na wale wa Kongo,tusijustfy kwa arguments ambazo ni illogical
....hata wao kama wataiona kweli ya udugu wetu wa asili,wakitambua faida zake,wakajua na hasara ya leo, ya fitna ya ukoloni ktk afrika, na huku kwetu tukawadhibiti wasaliti na wahujumu wa umoja wa afrika,(vibaraka wa wakoloni na ukoloni), warundi na wengine uliosema tunaweza ungana nao, na kama unafuatilia mambo utaona muelekeo ulivyo hususan ndani ya EAC...waliotumia uwanja wa ndege wa kigali, au hata wewe kama umeutumia,ulihudumiwa, kama raia wa EAC,kwenye mstari mmoja na wanyarwanda, mkiwaacha wasiokuwa raia EAC kwenye mstari wa wageni. lkn hakuna mahusiano yoyote yanayoweza kuleta muungano na maeneo kama, iindia,yemen,oman, au china....
 
kwani uongo? leo mnadiriki hata kufuta uchaguzi wa upande mmoja wakati chaguzi zote zilifanywa wakati mmoja, watu walewale na hata mchovya wino kwenye vidole mmoja. iwejeleo mmoja ukawa na vurugu na fujo mwengine ukawa safi!
 
Tuelimishane Wananchi

Je ni zipi faida na hasara za muungano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani?
 
Tuelimishane Wananchi

Je ni zipi faida na hasara za muungano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani?


Dunia inatamani kuwa nchi moja, kiongozi mmoja, sarafu moja, polisi moja na bunge moja. Ulaya wanatamani kuwa nchi moja. Hivyo msingi wa muungano wetu unaanzia hapo. Kwamba kwa hali zetu duni kiuchumi na kiusalama kwa nini tuishi mbalimbali? Ni busara kuungana tena si kuwa na Serikali mbili kama ilivyo sasa Bali kuwa na Serikali moja.

Mnapoungana mnakuwa wengi ndani ya eneo moja. Population katika ukuaji wa uchumi ni muhimu katika soko la pamoja. Chukulia kampuni ya Zantel (Zanzibar), kwa sababu ya muungano wetu inauza vocha zake hadi Musoma Vijijini badala ya kuishia Pemba. Hapo tunaona faida ya upanuzi wa soko.

Faida nyingine ni mahusiano mema. Kuwa huru kufika eneo lolote ndani ya mipaka ya nchi zetu bila kuhojiwa tofauti na kwenda Rwanda kwa jirani zetu. Hasara pekee ninayoiona ni kuendesha muungano kiujanja-ujanja. Mkubwa kumuonea mdogo au mdogo kumdekea mkubwa nk.
 
Waungwana,
Nimepewa kazi ya kuandika faida za kiuchumi za Muungano kwa pande zote mbili. Tafadhali naomba tujuzane
 
Umeme wa Tanesco zanzibar hawalipii chochote hela wanayokusanya shirika la umeme zanzibar wanalipana mishahara!!!
 
Naomba unieleweshe, tafadhali kwa sababu huu ni mwaka wangu wa 30! Sjawah kupata faida au hasara za muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…