Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Kwa upande wa wananchi Kuna faida kubwa sana , hakuna hasara hata moja .
 
Salaam ndugu zangu wote

Wacha kwa ufupi niwaeleze hasara kwa Tanganyika ikiwa muungano huu utavunjika kama mimi ambavyo nategemea kuwa hauwezi kudumu kwa kuulinda kwa vifaru ila utadumu tu iwapo maoni ya muundo wake yatazingatia matakwa ya wananchi wa pande zote mbili.

Kwanza kutatokea kushiktakiwa kwa Tanganyika na watu waliopoteza ndugu zao wakati wa mapinduzi kwa sababu Tanganyika ndio iliyofanya mauaji hayo na kusingizia watu wa Zanzibar ati walipindua serikali ya kisultani hili watu wengi hawalioni lakini nataka niwajuze tu kuwa ndio sababu kuu ya kulikataa jina la Tanganyika.

Pili mipaka ya Tanganyika ya baharini hiwezi kuichupa Zanzibar na kuwa nyuma ya Zanzibar. Hii ina maana kuwa upana wa bahari ya Tanganyika utakuwa finyu kiasi cha kuzua tafrani kwa wavuvi wa Tanganyika.
Tatu deni la Tanzania kwa kiasi kikubwa litabebwa na Tanganyika kama ilivyo hv sasa ambayo yenyewe ndio inayofaidika na GRANTS nyingi kwa jina la Tanzania.

Tanganyika itabidi ilipe deni la faida iliyotokana na Bank of Tanzania kwa sababu mtaji wa kuanzisha benki hiyo ulitokana na mchango wa nchi mbili lakini faida haikutolewa tangu kuanza kwa banki hyo mwaka 1967.

Nne Tanganyika itabidi irudishe pesa iliyochukua kutoka Normandy Bank ambazo zilikuwa pesa za Zanzibar kabla ya muungano lakini zilichukuliwa kwa ubabe na Julius Nyerere na muhindi wake Amir Jamal.

Nitaishia hapa lakini orodha ni ndefu sana na nasisitiza kuwa watu wa pande hizi mbili hawana ugomvi ila kuna dharau tu kwa baadhi ya viongozi kutokana na ulevi wa madaraka.

Ahsanteni
 
Ukivunjika utawapa nafasi wananchi wa pande zote mbili kuamua muungano gani wanaotaka.
 
Tangu nipate ufahamu nimekua nikisikia viongozi wakiusifia muungano wetu kwa mbwembwe nyingi sana lkn binafsi sijui faida yoyote tunayopata kama wananchi wa kawaida kutokana na muungano zaidi sana niliwasikia wajumbe wa bmk hasa toka ccm znbr wakisema ukivunjika serikali haitaweza kujiendesha kwani inabebwa na tangnyka.
 
1. Kujifunza chuki mf; mtu asiyekuunga mkono usimsaini fedha ya matibabu japo wao wanaopeana kodi zetu kujitibia wanakuga kama maskini wengine.

2. Vichekesho kupitia watu wazima kujifanya watoto mf: eti kufuga ndevu si kigezo cha kuwa rais.

Wao watakwambia ulinzi wa nchi ila usiwalaumu maana ni mawazo yao.
Unang'ang'ania kuwafanya masikini wa zenji wa watu ili ujilinde.
 
Naziona dalili za kuvunjika kwa Muungano wa Tanzania. Kuna matamshi kuwa Zanzibar imekuwa koloni la Tanganyika, mipaka ya Zanzibar ni maili kumi ndani ya Tanganyika mengine mengi. Kwa sasa Zanzibar wanayo katiba yao, bendera yao, wimbo wao wa taifa na wanasema Zanzibar ni nchi kamili. Rais wa SMZ anapigiwa mizinga 21 katika sikukuu za SMZ. Kama Rais wa Jamhuri yupo anakuwa kama Rais mgeni mualikwa toka nchi ya kigeni ilhali yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania.

Sishangai Rais John Magufuli akiacha kushiriki sherehe hizo. Ninachofikiri ni kuwa tunapaswa tuuanze upya huu muungano. Kama upo uhalali wa kuwepo SMZ ndani ya muungano ni vyema kukawa na uhalali huo huo wa kuwepo serikali ya Tanganyika ndani ya muungano iliyo na katiba yake, wimbo wake wa taifa, bendera yake na kiongozi wake anaye pigiwa mizinga 21 katika sikukuu za nchi yake. Vinginevyo kiuhalisia muungano mimi siuoni labda huu unaolindwa na jeshi.
 
PMNBuko,
Mkuu nimepitia hii hoja yako. kiukweli imenigusa na inawezekana itawagusa wengi tu haswa Watanganyika.
Kiukweli sielelwi ni nini kilichotufikisha hapa mpaka tukapoteza utaifa wetu wa Tanganyika kwa maan najaribu kuangalia mbele endapo siku moja itatokea zanzibar ikaamua kuachana na Muungano je sisi tutaendeleaje kujitambulisha utaifa wetu?
 
Tunaupenda, tunajivunia, tutazidi kuulinda na hakika tunazo sababu za kufanya hivyo.

Changamoto zipo ila haziondoi umuhimu wa muungano wetu

Hii ni kwa wazalendo pekee wenye uwezo wa kuweka itikadi za kisiasa pembeni.

Ni 26 Aprili tena.
 
Muungano wetu wa kindugu na wa damu ya Kiafrika, Muungano hoyeeee
 
Faida zake ni zipi haswa... unaweza uluzwa hili swali na mwanao ukashindwa jibu.

hapa majibu lazima watu wanayo. Hasa huku Bara....unafaida gani!??

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom