Cuf ya Maalim ni chama kinachopata pesa toka kwa Sultani aliepinduliwa. (Maalim anakutanishwa na Sultani Jemshid Qatar, na Karume anajua) Kwanini tunachezea shilingi chooni? Pia kinaitwa Hizbu kama chama asilia ya Sultani yaani kwa kiswahili ndio chama cha wananchi. Chama kichafu hichi kwa amani na mustakabali wa nchi yetu. Chama kifutwe mara moja. Migogoro mingine sio ya lazima, tuachwe tufanye kazi, hawa wanaotamani uarabu kama suluhu ya matatizo ya kiuchumi waone Siria, Somalia na Yemen wakigombania kula mizoga ya mbwa na watu. Futeni chama chenye ndoto ya piga ua kuigawa Tanzania.
Mkuu Maalim Seif sio mwarabu,Maalim Seif ana asili ya Kishirazi,si unakumbuka Afro Shirazi Party(ASP),chama kilichoongozwa na Karume,Chama kiilichompindua Sultan wa Zanzibar,halafu chama hicho kikaungana na TANU mwaka wa 1977 halafu kikazaliwa CCM
Sasa hizi propaganda za Hizbu zimetokea wapi,kwanza unajua maana ya Hizbu,Hizbu ni neno la Kiarabu linalomaanisha "chama",kwahiyo ukisema "Hizbu" lazima uweke neno jengine mbele yake mfano:"Hizbu alwatan" au "Hizbu llah" nakadhalika
Aliekuwa Sutani wa Zanzibar Jemshid hayuko arabuni yuko Portland Uingereza,Wa Oman walimkataa kumchukua baada ya kupinduliwa kwasababu waliona sio mwanarabu sio Muomani,ni Mzanzibari...Jemshid yuko Uk anaishi kama mkimbizi hana tafauti na wasomali au mkimbizi yoyote yule.
Mkuu propanganda kama hizi zimepitwa na wakati,"zilipendwa",lete propaganda ambazo zitaleta maendeleo Zanzibar,sizo ambazo zitawagawa wazanzibar.....
Hamna mtu anaetamani uarabu,wazanzibar wanatamani wajitawale wenyewe,walimuondoa Sultan ili wawe na nchi ya Jamuhuri,sasa wanaona wanatawaliwa,wanaona hakuna faida yoyote ya huu mungano...
Zanzibar haiwezi kukopa ili ijipatie maendeleo,Zanzibar haiwezi kucheza michezo ya kimataifa,Zanzibar haiwezi kujiendeleza kiuchumi,Kwa jina la Muungano unazidi Zanzibar kila kukicha...
Kwahali ilivyo sifikirii kama kuna mzanzibari anaweza kuzisikiliza propaganda kama hizi....