Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

dizzle1,
pole sana...kwanza jifunze historia ya Tanganyika na Zanzibar, baadae jifunze historia ya Tanzania. Mambo haya hayataki ushabiki, usiwe mtu wa kufuata mkumbo kirahisi.
 
Nitasema kweli daima,fitina kwangu mwiko. Muungano wa tanganyika na zanzibar ni utapeli wa hali ya juu. Warudi kwao watoke kwetu. wakirudi kwao watalipia umeme kwa fedha za kigeni. Tunawabembeleza mno ndio maana wanafanya wapendayo. Lakini kimsingi wanajipanga ili wajitoe. Wakijitoa nitafurahi mno. Wahimizeni wajitoe haraka.
 
hii structure (sio muungano) ya muungano wetu inaweza kuwa imechangia matatizo mengi tuliyonayo leo maana wakati mwingine yanakuja maamuzi mazuri sana halafu tunalazimika kuyachakachua ili kufurahisha watu kama 900,000 juu ya 50,000,000!!! FIKIRIA KWELI. Hivi kwa hali ilivyo hatuwezi kuwa na matatizo ya kiutawala na Kenya, Burundi, Rwanda na Uganda kwa vile mikataba ya 'muungano' wetu iko wazi.

Hili suala la Zanzibar kuwa nchi inabidi tuachane na sababu za kihistoria na tuichukulie kiukweli tu kuwa ni nchi moja ya Tanzania. Kwani ni kitu gani kinafanya Wakurya wa Musoma wajione sawa na Wangoni wa Songea!!?? ....hivi 'nchi' ya Unguja ina makabila mangapi vile?
 
Watanganyika mmeuzwa nyinyi, hata jina lenu la mababu mmelitosa kwa kukubali ubatizo wa Tanzania, lakini wenzenu bado ni Wazanzibar vile vile wanataka kuwa Jamhuri ya Zanzibar na Pemba na haiko mbali, tikiendelea kuwa softi watazamisha kidole, au hamjui kuwa ni wataalamu wa kubonyeza? kama huamini soma web hii www mzalendo . net
 
Mimi naona ni wakati umefika kwa tanganyika nasi kuanzisha movement yetu-kama walivyofanya wazee wa pemba-basi nasi tujiite wazee wa tanganyika-maana naona viongozi tunao ila naona wao ndo wanaonufaika na muungano na ndo maana wanaung'ang'ania-bora sisi kama sisi tuji organise wenyewe-la sivyo hii nchi itakuwa inafanya mambo ya ajabu ajabu huku tunaona-zanzibar ibakie kivyake na sisi tuende kivyetu-wazenji walioko huku bara warud kwao-na wananchi wetu walio visiwan warud bara-kila nchi ifanye utaratibu wake mpya-maana naona tunawabeba kama watoto-sasa wanataka kutukata na viwembe mgongoni ila sisi bado tuna wabeba tu
 
MAMMAMIA,
Tuwaache wajitenge ili waone kilichomtoa kanga manyonya. Lakini hili la kuwa na bodi yao ya mikopo na kwamba sifa ya kupata mkopo lazima uwe mzanzibar ni hoja za kiuendawazimu. Yaani wanafanya mambo ya kiinga kama UVCCM.
 
ni kweli lakini wanasema tunawaibia! lakini ukweli ni shibe ya pesa za watalii, utalii aliouleta Zakia Meghji, waziri wetu wa utalii wa muungano alielekeza makampuni yote Zenji, akiwa waziri wa muungano, na huko watalii na wawekezaji wanapewa maoni mabaya juu ya tanzania bara ili wasije wekeza, bora waende kenya lakini sio bara.

www.mzalendo.net ujue muungano ilivyokwisha.
 
Ukiwasikiliza wazanzibar wanaongea unajua hakuna muungano, nilisikia mtangazaji mmoja akitangaza habari ya "wanzanzibar" na si watanzania waliokuwa wakirejea kutoka Ushelisheli. Sidhani kama wangekuwa wasukuma wa shinyanga au wanyakyusa wa tukuyu wangetangazwa kuwa wasukuma au watanganyika waliokuwa wametekwa bali wangesema watanzania
 
Huu ni uchokozi tena wa hadarani. Kwani HELSB ina wabagua wazanzibar? Hebu watupe sababu za kuamua kuomba hivyo. Basi ratio iende kiukubwa wa eneo/mkoa aur idadi ya watu. Kila mkoa upewe fungu lake kwa ajiri ya kusomesha vijana wa mkoa wake.Haya mayakhe yanataka kuanza kupewa kila kitu na wajomba zao, waarabu ndo maana akiri fupi. Kama mmechoka muungano tangazeni kesho, sisi hatuna shida na muungano. Kwanzan munatuongezeee kero na kutupoteza kwenye issue nyeti kama Richmond, Dowans zinazohusu taifa na nyinyi huko. Munaona mambo yanaenda ndo maana munafikiria utumbo tu, sisi huku wa bara ndo tufanya kazi.
 
Babu Lao,

Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
Wanalotaka Wazanzibar ni jambo la msingi kwa vile Jamhuri ya Muungano imejitwisha mizigo mingine ambayo si ya lazima kwa zanzibar. Masuala ya Muungao yangejumuisha katika jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania, Uchapishaji wa pesa na mikataba ya kimataifa kama Marekani ifanyavyo. Elimu, jeshi la polisi na mengineyo ni mambo ya state ambayo jamhuri ya Muungano isingebaba mzigo huo.
 
Hivi ni kitu gani ambacho kina wapa wazanzibari kiburi?....ule si mkoa tu, hauna madini wala nini.

We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?

Mkuu.
Msimamo wako ni upi hasa katika hayo mawili uliyoyasema?
Halafu ukisema Zanzibar ni mkoa. Ni vyema urudi kwenye historia.Tanganyika ilikuwa nchi, iliunganisha mambo kumi na moja na nchi ya Zanzibar na kufanya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Hasira zetu, hofu zetu, uchungu wetu, dharau zetu, furaha zetu au chuki zetu zisitufanye kuukana ukweli au kuupindisha ukweli.
Kama Muungano usingefanywa "taboo" tokea pale ulipoundwa basi hizi hofu, chuki, au dhana za kudhulumiana zisingepata nafasi.
Tunavuna tuliyopanda. Njia pekee ya kututoa katika usanii huu wa Muungano ni kuanza kuwa wawazi na kujadiliana kama pande mbili za muungano, kama nchi mbili za muungano . Tena iwe mijadala ya uwazi na kwa nia njema.
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?


Na hasa wakiamua kudai Pwani yote pamoja na tanga ni ya Sultan bila kusahu mafia!
Lakini kwanini tuwaogope DUBAI?
 
Kama wataanzisha wenyewe kwa nini wapewe hizo hela na HELSB? Wewe utapangaje bajeti yako kwa mfuko wa mwingine?
wakianzisha wanatakiwa waishughulikie na kui-fund wenyewe. Wanavyo vitega uchumi huko Zanzibar.
 
Kuna tofauti kubwa sana ya kiitikadi na hilo ndio limeibuka hivi karibuni.

hakika Zanzibar tumekuwa wanyonge sana katika kutetea haki zetu haswa ukizingatia Siasa za JK Nyerere za mabavu katika kuitawala Zanzibar. Tujue kuwa sasa tumezinduka na kujaribu kuvipitia vipengele vyote vilivyoingizwa kinyemela katika mkataba wetu wa Muungano.

Sasa hii ni sehemu ndogo tu . lakini kuna mengi ni lazima yawe sawia kabisa na makubaliano yetu ya Muungano
 
Hivi ni kitu gani ambacho kina wapa wazanzibari kiburi?....ule si mkoa tu, hauna madini wala nini.
wewe mdanganyika mwenye madini yanakusaidia nini?au yanawasaidia makaburu nawewe unaachiwa mahandaki matupu.
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?
Hata kidogo kwani badala ya kpoteza nauli kwenda huko basi mnapanda Sea Epress mnakuja kubeba tosha yenu halafu mnapeleka Malawi, Uganda, Rwanda na hata Kongo mbili.
 
Kama muungano ni wakuvunjika hatimaye utavunjika. Huu muungano una lalamikiwa sana kila upande, Lakini siku ukivunjika kuna upande utaumia sanaaaaaaaaa!

Ningetamani kuona ukiboreshwa hasa kwa kuwa na serikali moja tu! Lakini kwa vile uroho wa madaraka unatawala; kuwa na serikali moja ni ndoto!
Unaonaje kuondowa huo uroho wa madaraka tukafanya kama anavyotaka Kagame na Museveni? Hebu angalia nchi tano zikiwa na Rais mmoja na bunge moja huo uroho wa madaraka uaosema hautokuwepo.
 
MAMMAMIA,

Ni wazi kuwa bila kutumia akili ikiwa ipo basi unaweza ukasema Pumba sana. Hivyo wawakilishi sio wanaowakilisha wananchi? Bila shaka wanalosema ni msimamo wa wananchi hivyo hiyo assumption yako kuwa walioko nje ndio wanaochochea si kweli

Pili hili la kuwa Zanzibar hawana uchumi wanaoutegemea inawezekana ikawa si issue kwani hata sasa hawana uchumi na hakuna msaada wowote kutoka Bara si wa hali wala mali.

Hili la kuchaguwa nani apewe huo mkopo ni wazi itakuwa kwa wanafunzi wa Zanzibar kwani hilo ndio lengo la kuanzishwa huo mfuko. Na siajabu kwani vyuo vilivyoko Tanzania vinasomesha wanafunzi kutoka nchi za nje lakini hawa hawapewi mkopo kwani sio wao na hali hiyo itakuwa sawa na Zanzibar. Huo ndio uamuzi tuliokubaliana tulipoungana.

Kuhusu HESLB na kutowa fedha hizo kwa bodi nayo si issue ya kuleta wasi wasi kwani hili halitokuwa jambo la mwanzo kwa Serikali inayojiita ya Muungano kutotowa fedha za pamoja kwa visingizio chungu nzima.

Hivyo hujuulizi katika akili yako kuwa hujasikia Wazanzibari kufa kwa njaa kama mwenye akili ungejiuliza kuwa kweli visiwa hivi havipatwi na shida? Ukipata jawabu nafikiri utafahamu kuwa hatuwa yoyote mtakayochukuwa juu ya Zanzibar si ngeni na wala hawashituki nayo.
 
Back
Top Bottom