Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

MushyNoel,

Thanks for your post. Please could you provide us with reference if any, or else please attest that this is your article.
I would like to use this in future reference.

Thanks

NG
 
BARAZA la Wawakilishi limepitisha Muswada wa Sheria ya kuanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar na baadhi ya wawakilishi wamependekeza Bodi hiyo ipewe fedha na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Tanzania (HELSB).

Uamuzi huo wa Zanzibar, utakuwa umeondoa suala la elimu ya juu kutoka kuwa la Muungano na kuwa suala la Zanzibar na linaweza kuzua changamoto ya Muungano kuhusu fomula ya kugawana fedha za HELSB, kwa kuwa mpaka sasa fomula ya kugawana fedha za misaada inaonekana kuwa changamoto inayoendelea.

Angalizo: Sidhani kama muungano unafaa kuendelea kuwepo tena kama waloungana hawauheshimu!!
 
Hivi ni kitu gani ambacho kina wapa wazanzibari kiburi?....ule si mkoa tu, hauna madini wala nini.
 
Hivi ni kitu gani ambacho kina wapa wazanzibari kiburi?....ule si mkoa tu, hauna madini wala nini.
Mkuu nadhani tumezidi sana kuwabembeleza... wametoa hili jambo kwenye muungano na sasa eti wanataka wawe wanapata mgao kutoka HELSB.... mimi sielewi tunaenda wapi :embarassed2:
 
Wazanzibari si wajinga, wanapanga mambo yao kwa uangalifu mkubwa sana, hiki si kiburi kama wangine wanavyoona, ila ni kuendelea kujipanga possibly kujitenga, tunalotakiwa kujiuliza hukubara ni;

1.Muungano ni kwa faida ya nani, mimi sijawahi kuona faida ya huu mungano, wanasiasa wa ccm wanafaidika nao na ndio maana hawataku uzungumzwe.

2.Sifa na faida za muungani zi za kufikirika, sioni fahari yoyote wanayoitaja, au kusema kuwa eti ni wakipekee afrika! lol
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?

Kwani Tz tuna uwezo wa kuzizuia nchi nyingine za jirani kujiunga na hiyo 'dubai'? Hii hatari kwa 'usalama wa taifa' inatokea zanzibar tu?
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?

Hayo matumizi ya neno kuhatarisha usalama wa taifa mara nyingi uashiria udikiteta na ukandamizaji.

Ebu tujifanye Zenj wamejitenga, usalama wa taifa utahatarishwa vipi?

 
Kama muungano ni wakuvunjika hatimaye utavunjika. Huu muungano una lalamikiwa sana kila upande, Lakini siku ukivunjika kuna upande utaumia sanaaaaaaaaa!

Ningetamani kuona ukiboreshwa hasa kwa kuwa na serikali moja tu! Lakini kwa vile uroho wa madaraka unatawala; kuwa na serikali moja ni ndoto!
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?


Kwani asilimia ya mchango wao kwenye usalama wa taifa ikoje kwa sasa kiasi wakiondoka kutuathiri?

Unaweza kuifafanua na namna itakovyoathiri usalama wa Tanganyika yangu?
 
Ndiyo maana sisi Chadema tulisema siku nyingi kwamba nchini kwetu lazima kuwepo na Serikali tatu. Hili ndilo suluhisho. CCM wakabishabisha muda wote. Sasa maji yamewafika shingoni lazima watekeleze sera ya Chadema ya Serikali tatu.
Na hii ni sababu mojawapo inayowatisha na kuogopesha sana - suala la katiba mpya ambayo mwisho wake nayo lazima itatungwa tu - watake wasitake.
 
Sisi wa Tanganyika tumelala bado usingizi wa pono hasa viongozi wetu, mambo haya yanamaudhi kweli ndiyo maana wazanzibar wamechoka na mambo yetu sasa wameamua kuwa kitu kimoja wote CUF na CCM na wanaonesha uzalendo wao wakupigania nchi yao,Sisi tulitegemea nini maelewano ya CCM na CUF visiwani!walikaa chini wakaona Kumbe Uzalendo kwanza sio vyama,vyama ugomvi tu na kugawa wananchi.

Ona sasa bara yameanza mambo ya ukanda,pwani wanasema ooh rais hatoki kaskazini,mara ooh udini tumekalia kulumbana mambo yasiyo ya maana huku wawekezaji kwenye madini actually wanyonyaji wanatuibia madini yetu kumbe kuna mpaka viwanja vya ndege kwenye mogodi du!

Wazinzibar waachwe waende zao wenzetu wamejanjaruka,sisi tumezubaa sana kama tunaibiwa hivyo madini unadhani wao watakuwa tayari kuendelea kuungana na sisi? mimi huwa najiuliza hivi ni jambo gani waliloongea Seif na Karume mara moja wakaelewana na kuamua kuwa wazarendo wa nchi yao! najipa jibu mwenyewe hawa watakuwa wameona mwenendo wetu ulivyo wakaona tunawapotezea muda maana hata rasimali zetu za huku bara hatujari tumekalia malumbano yasiyo na maana na uzalendo sifuri wakaona waunganishe nguvu dhidi yetu na sasa wanatuacha taratibu lakini kwa uhakika leo hii wanataka bodi yao ya mikopo ya elimu ya juu.

Narudia kusema kwani wao hawaoni uozo unafanywa bara? waache wamegundua tunadanganyana tu,mimi sio mzenj lakini naona sawa wanavyo fanya.Tunaibiwa madini tumekaa kimya,ufisadi mwingine tumesikia tena leo billion mia tatu na kitu wa zantel na airtel mpaka Mtu unajiuliza kwanini lakini jamani Watanzania,halafu wizara ya mali asili billion tisini du ajabu kweli, mara tunaambiwa hata wabunge wetu wa Africa Mashariki hawajui wanachofanya huko bungeni,hawajajipanga kama wenzao wa kenya tunategemea nini nchi ya namna hii jamani!

Haya angalia malumbano ya UVCCM, sasa Sumaye amejibu nae anawashangaa kwa maneno wanayo jiongelea tu bila kujua athari kwa nchi,sasa UVCCM kilimanjaro nao wamejibu wanawashangaa viongozi wa UVCCM taifa du, amakweli CCM imekufa jamani.

Wananchi sisi ndiyo tutakao amua mustakabali wa nchi hii na sio CCM. Chadema wameamua kuwaelimisha wananchi lakini wanaonekana wachochezi ajabu kabisa hii,kwani maisha hatuyaoni magumu! kwani sisi wajinga hatujui ugumu unachangiwa nini? Utapeli,ufisadi,wizi wa mali asili yetu ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha yetu,hivi watanzania nani ametuloga?.

Mmambo yote haya yanasababishwa na kuwa na katiba mbovu ambayo watu wachahche wamerundikiwa madara yote ya maamuzi na matokeo yake ndiyo haya, jamani tukate haya mambo tuache ushabiki usio na tija, mambo ya udini, ukabila, ukanda hayatatua matatizo yetu ya Njaa, elimu duni na kuchapika ila tu uongozi bora na katiba nzuri na tujue nchi hii yetu wote sio ya dola, tumeisikia amesema Sumaye kumbe ili uwe Rais vyombo vya DOLA vikukubali nashangaa sana kumbe tulipoteza muda wetu kusikiliza mikutano ya kampeni na hata kupiga kula,tumetumia billions of money kumbe ilikuwa changa la macho tu,kauli ya Sumaye ina nguvu maana alikuwa waziri mkuu na alikuwa jikoni na anajua anachokisema mimi mtu wa kawaida inaniingia kweli kauli kama hayo na nimeamini Dr slaa alikuwa ana haki ya kulalamika. Sasa maskini CCM mmeanza kulumbana wenyewe na ukweli wote tutaujua, mmeamua kumwaga ugali na wengine wanamwaga mboga sasa kumekucha.
 
Msiwabeza Wazanzibar hata kidogo kwa sababu wao wanayo dira na wameweka malengo kuyafikia, hivyo muafaka wa CUF na CCM sii bahati mbaya..

Muafaka ullikuwa kuwaunganisha Wazanzibar na sio vyama, to face one common enemy wao - Bara na CCM yao..

Nachoweza kuwaambia CCM ni kwamba mke anayedai talaka hata siku moja hawezi kushawishika na zawazi mtakazo mpa..Mwisho wa siku talaka utaitoa na hasara kwako kupoteza uda na fedha..

Zanzibar wamejipanga vizuri sana na dio maana CUF wameunga a na CCM kwani wanamhitaji CCM zaidi ya CDM ili kufikia malengo yao..

Kazi ipo kwa CUF bara na wataachwa mataani na wenzao wakiachiwa chama maana wao wameisha unda umoja kwa jina la mseto wa serikali visiwani,huku bara patupu hamna kitu...

Wanachoambulia bara ni viti viwili bungeni wenzao wakishika madaraka ya juu na bado haitoshi kwao hadi Zanzibar imetoka ktk muungano..

Hapo ndipo mtajikuta nyie ni Wabara na hamtakiwi machogo visiwani hata kama una kadi ya CUF..
 
Watanzania kwa mwenye ilimu ya sheria na kuangalia ule mkataba wa makubaliano wa kuunganisha hizo nchi mbili yaani Zanzibar na Tanganyika hawezi kulishangaa hilo.

Kwani kwenye makubaliano ya Awali Elimu haimo. Ila limeingizwa kinyemela sana na kulipa sura ya kimuungano.

Bila shaka WaZanzibar wameliona hilo na kuvunja ukimya.
 
:tongue:

Siwezi kueleweka leo lakini keshokutwa nitaeleweka

Zanzibar they are up to something...wanajua wanachokifanya, wanajua Watanganyika tumelala

Tutashtuka keshokutwa wakati wakiwa wamjiwekea mfumo mzuri wa kujitawala binafsi.....hapo tutabaki haaaaaa na madomo wazi

Keep it up Zenji

Napenda kuiona zanzibar kama nchi na sio kama sehemu ya muungano na Tanganyika!
 
Muungano, muungano, muungano.... ah tumechoka.

Mimi siamini ktk muungano wa Tanganyika na Zanzibar na naomba uvunje mara moja. tunaung'ang'ania wa nini jamani? wazenj wanasema wananyonywa, watanganyika wanasema wnanyonywa sasa kwa nini tusiachane nao?
Nawapongeza sana wazenj kwa kuamua kujiletea maendeleo yao wenyewe maana imetamkwa kila mtu atakula kwa jasho lao. wanapanga vizuri mipango yao ya maendeleo, wabara sisi alieturoga kafa na hatuna wa kumwomba msamaha ndo maana wenzetu wanajiita wazenj sisi tunajiita wabara utadhani imetolewa marukufu kutamka watanganyika...

Kondoo ni rahisi kumbeba ila ni vigumu kumlisha
 
We hudhani kuwa kujitenga na zenji kunaweza hatarisha usalama wa taifa....especially kama baada tu ya kujitenga wakaamua kujiunga na dubai?

Usalama wa Taifa ki vipi mkuu? Elaborate tuzame jamvini?
 
Zanzibar ni nchi, na itakuwa busara kuwaachia wafanye watakavyo. Kwa maana nyingine huu muundo wa muungano haufai na umepitwa na wakati. Tunapoteza muda mwingi kujadili mambo ya muungano ambao hauna manufaa yoyote kwa Tanganyika
 
Hivi ni kitu gani ambacho kina wapa wazanzibari kiburi?....ule si mkoa tu, hauna madini wala nini.

acha kuongea pumba....nani amekuambia kama Zanzibar ni mkoa. Makubaliyano ya muungano yameharibiwa na Tanganyika...Hapo zilipoungana zote Tanganyika na Zanzibar zilikua nchi huru...Tukumbuke kama Senegal na Gambia ziliungana na muungano wao haukudumu kwa sababu kama hizi za upande mmoja kutaka kuwaamulia upande mwengine kila kitu. Mpaka hapo Tanganyika itakapo kuwa na serikali yake ndio kasoro za muungano zinaweza kutatuliwa.
 
Back
Top Bottom