Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Barubaru,
Wao walinufaika sana na suala la elimu ya juu kwani walikuwa wanapata mikopo wakati si wa Tanzania halisi tulikuwa hatupati kitu. Kwa kweli kuendelea kung'ang'ania muungano ni kupoteza muda. Kila mtu aanze mbele na tuone nini kitatutokea. Tumebembeleza na kubembeleza lakini wenzetu wamekuwa kama ngamia waliomba kuingiza pua tu katika nyumba sasa wanataka kuingia wazima wazima. Haiwezekani kuelewana na mtu anayeamini kuwa "chako chetu lakini changu changu." Madhali muungano hawautaki na ulilenga kutunufaisha wote kila mtu achukue chake.
 
Kama wataanzisha wenyewe kwa nini wapewe hizo hela na HELSB? Wewe utapangaje bajeti yako kwa mfuko wa mwingine?
wakianzisha wanatakiwa waishughulikie na kui-fund wenyewe. Wanavyo vitega uchumi huko Zanzibar.
Mkuu.
Bajeti ya Tanzania aka Tanganyika inapata ufadhili wa si chini ya 40% kutoka kwa "wafadhili".
 
lukindo,

Historia ni historia si mchezo wa kuigiza. Zanzibar ilikuwa nchi na itaendelea kuwa hivyo. Hata sokwe huvishwa nguo kama binaadamu lakini hawi binaadamu.
 
Tuwaache wajitenge ili waone kilichomtoa kanga manyonya. Lakini hili la kuwa na bodi yao ya mikopo na kwamba sifa ya kupata mkopo lazima uwe mzanzibar ni hoja za kiuendawazimu. Yaani wanafanya mambo ya kiinga kama UVCCM.

Jee unamkubali Seif kuwa Makamo wako wa Rais? Ukikubali basi na mkopo wa Wazanzibari ni halali yako.
 
Pharaoh,
Ndugu yangu usinifanye nihisi kuwa hukufanya utafiti na unachokieleza? mbona Utalii Zanzibar ulishaendelea hata kabla ya Zakia?
 
MAMMAMIA,

Mkuu.
Umekuwa mkali sana. Calm down.
Kwa sababu mambo ya Muungano hayakuwa yanazungumzwa kwa uwazi basi mambo yamechanganyika sana kiasi tunashindwa kuchambua nini ni nini!

Kitu kimoja ni kuwa Zanzibar leo kutokana na Muungano unavyoendeshwa haina mamlaka ya kiinchi,kila kitu kinapitia Muungano. Ukivunjika muungano ni kuwa wanarudisha ile sovereignty yao yote. Hiyo itakuwa hatua kubwa kwao. Sasa hili la kufa itategemea umakini wa viongozi wao watakaowachagua.

Viongozi wao wakirudisha siasa za ubaguzi basi kweli watapata tabu lakini kama wataendeleza spirit ya GNU basi hawa watu wanaweza kukwamuka kwa haraka. Mkuu zipo nchi za Sychelles, Cape Verde na Mauritious hapa Afrika ambazo ni nchi za visiwa na zipo wapi kimaendeleo ukilinganisha udogo wao na idadi ya wakaazi wake na maendeleo ya Tanzania?

Tatizo hata la Tanzania ,Tanganyika ni viongozi tu , siasa za kubabaisha na kutokuwa na priorities.
Maliasili iliyopo na nguvu kazi isiyotumika ipasavyo,Tanzania sio wa kuwa kwenye orodha ya mkiani kabisa kwa umaskini.

Ni maoni yangu kuwa Zanzibar wamebanwa sana na Muungano kiasi hawawezi kufanya maamuzi ya maana ya kuiendeleza Zanzibar hasa wanapokosa nguvu za kisheria kushirikiana na mataifa mengine duniani kama Zanzibar.

Kwa manung'uniko wanayotoa wazanzibari ni kuwa kuna mambo mengi ambayo si ya Muungano lakini hakuna mechanism ya wao kutafuta development partners bila ya kupitia Muungano. Hilo linakwamisha juhudi zao za kujiletea maendeleo.
 
Watu milion 1 wanataka kuunda nchi. Nawapongeza kwa ilo la sivo miaka7 ijayo nilikuwa na proposal watu mil1 hao ambao 50% wako bara,k.koo,bugurun,mwembechai na magomen na mtwara, tupeleke boti wote tuwalete na kuwagawia plots pale kibaha alafu zbar tuifanye zoo na sehemu ya kutunza silaha. Kama wanaitaka zbar yao wapeni! Alaf wape na masaa kamili ya kuwa wametoweka bara,na kuja kwa sharti la visa,pia sharti kuacha kila kitu bara. Umeme,maji na usafiri tutang'oa na kuelekeza rukwa!
 
kweli kama watafikia hatua ya kupewa pesa kutoka HESLB nipo radhi kwa muasi-mbaona zanzibar wanatusumbua hivi?napata hasira sana nikisikia madudu ya zanzibar-kwa nini hawa viongozi wetu hawataki kuvunja huu muungano?wananiboa sana
Mkuu.
Unanifanya niamini kuwa at last unaelewa nani ndio tatizo..."viongozi wetu"...sasa lililobaki ni moja tu.Tuelimishe wanaTanganyika ili tuwasukume viongozi wetu wauvunje huu muungano ,na hivyo madudu, ubebaji na usumbuvu ufikie ukomo.

Kumbuka viongozi wa serikali ya Muungano ndio wanaoshikilia nguvu za dola..wanapoamua hili liwe basi ni kama vile kumsukuma mlevi. Atadondoka tu.

Vyenginevyo "viongozi wetu" wana siri kubwa ambayo hawataki sisi tuijue. Kwa hiyo tuwalazimishe watekeleze sera ya ukweli na uwazi!
 
Bado nabaki na msimamo wangu, hakuna haja ya kuwaruhusu kujitenga, kwa kuwa wameanza vita ya kujitoa sisi Tanganyika tumelala, inatakaiwa twanzishe programme za kueimeza kabisa Zanzibar. Kitu kimoja alichokosea Mwalimu (R.I.P) ni kuwapa uhuru wa kuwa na serikali yao, toka mda mrefu walitakiwa wawe mkoa tu wa Tanganyika, ndio maana sasa wanasumbua.

Sikubaliani na hoja ya CHADEMA ya Serikali Tatu, bora kuuwa muungano kuliko serikali tatu, bado watatusumbua tu. Hao ngozi nyeusi walioko Zanzibar shida wataiona baada ya kufa muungano na watatusumbua mno baada ya kuvunja muungano. Naamini Zanzibar ni Kisiwa ambacho waarabu (mabwana) na waafrica (watwana) wamekutana hapo kwa karne nyingi na mpaka sasa dunia hizi race mbili ziko katika antagonist criss. Kwa sasa wajifanya mwarabu na mwafrica wote wako pamoja na wadai uhuru wao toka Tanganyika. Thats fine!!11.

Baada ya huo Uhuru ni wazi kuwa kamwe jamii ya kiarabu haitaishi pamoja na jamii ya Kiafrica hasa ngozi nyeusi kama ya makamu wa pili wa rais na hilo litakuwa ndoto na wala halijatokea mpaka sasa Duniani.Kama Tanganyika inashindwa kuimeza Zanzibar watalaam tupo, watupe kazi tuimalize decade mbili kwisha habari yake.
 
LINCOLINMTZA,
Ikiwa nyie huko kwenu mnaamuwa hivyo sawa. Zanzibar haikuungana na mikoa ya Tanganyika bali iliungana na Tanganyika na kupatikana Tanzania
 
Kama wataanzisha wenyewe kwa nini wapewe hizo hela na HELSB? Wewe utapangaje bajeti yako kwa mfuko wa mwingine?
wakianzisha wanatakiwa waishughulikie na kui-fund wenyewe. Wanavyo vitega uchumi huko Zanzibar.

Kwani hizo pesa si za Watanzania? Kwani hao Wazanzibari kwako si Watanzania? Lengo la huo mkopo ni lipi? Au unataka kusema kuwa Wazanzibari hawana haki na fedha hizo?
 
@Straatkasyambe
Mkuu.
Kama Mwalimu Nyerere yalimshinda haya mambo ya kuimeza Zanzibar kweli wewe mwanafunzi wake utaweza?
Inaonekana katika uendeshaji wa serikali ya Muungano na muungano wenyewe Mwalimu alikuwa na nia ya kuimeza Zanzibar. Viashiria vya hilo.

Kubadili jina la Muungano

Kifo cha Karume

Kuongezeka kwa orodha ya mambo ya Muungano.

Kuunganisha vyama vya Tanu na ASP

katiba iliyoanza kutumia Tanzania Bara ikimaanisha Tanganyika na Tanzania visiwani ikimaanisha Zanzibar

Kumtupa nje Jumbe alipotaka marekebisho ya Muungano

Kuwafukuza kutoka CCM viongozi wa Zanzibar(kundi la Seif Shariff na Hamad Rashid)

Kuzuia kwa nguvu zake zote juhudi za G55 kuirejesha Tanganyika ndani ya Muungano

CCM kutangaza sera ya kutoka serikali mbili kuelekea moja.

Marekebisho ya katiba ya Muungano yaliyofuta Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Muungano.

Kwa bahati mbaya, Kifo hakikuwa upande wa Mwalimu kuona azma hii inatimia kwa asilimia mia moja na hivyo kifo kilichukua uhai wa Mwalimu bila ya ndoto yake kutimia.

Sasa wazanzibari wamepata maridhiano, wameunda GNU basi hili la kuimeza Zanzibar naamini litabaki kuwa ni ndoto.
Lililo zuri kufanya ni kufanya Muungano wa haki na usawa au kutengana nao kwa amani kwa kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na Muundo wake.
 
Nonda,

mkuu Nonda... umefunga mchezo hongera sana. Watu wengi hapa huwa na ushabiki wa ajabu. Hii tabia sijui wameipata wapi? WE CAN NEVER RUN AWAY FROM THE TRUTH...
 
Nonda

Mkuu...Hapa JF watu wengi ni mashabiki tuu. Hata hawajui kutofautisha mchele na pumba, kazi kuchonga maneno tu. Lakini haya ni mafanikio ya CCM kuwatia ujinga raia wa Tanzania. Mimi naomba sana Zanzibar wafanikiwe kwani hiyi ndio itakayo wakomboa Watanganyika kwasababu hawa viongozi hawatakua na visingizio tena. Tusiwalaumu waZanzibar kudai haki zao ni haki yao kufanya hivyo. Kama waTanganyika hawawezi au wemeridhika na maisha hiyo juu yao.
 
Nonda,

Yote uliyoandika nayakubali kiongozi, kilichopo ki kwamba watu wengi humu JF hawajui kiini cha muungano huu. Waliojaribu kufuatilia kwa karibu huu muungano watakueleza kuwa huu muungano una nguvu kubwa ya nje kuliko ya ndani. Docement za CIA zinaonyesha kuwa US ilikuwa imejiandaa kuivamia Zanzibar kama muungano huu ungeshindikana 1964.

Sio siri kuwa Kanisa Katoliki lilishiriki vya kutosha kufanya mapinduzi Zanzibar, kwani nani hajui kuwa Okello alikuwa Chriastian fundamentalist. Kitu kingine hakuna siri kuwa pia huu muungano ulichochewa na vita baridi. Lakini ni vema tukajua kuwa baada ya vita baridi kuna mfumo mpya ambao umeambatana na utandawazi ambao wasomi kama Samwel Huntington wanaita CRASH OF CIVILIZATION.

Sio siri kwamba sasa kuna msuguano mkali baina dini mbili kubwa duniani (Civilization Clash), yaani Uislam na Ukristo na huu msuguano umekuwa mkali zaidi after september 11. Na kwa kuwa sasa Dunia inatawaliwa na mfumo wa magharibi na huu mfumo kuutengenisha na Christian tradition ni kazi sana. Licha ya kwamba watu wengi wa magharibi ni religious by tradition niliwa na maana ni waumini wa jina tu, wala si kama sisi wa swala tano lakni ni wazi mfumo wao unahusianishwa na Ukristo.

Check role of Blackwalter in Iraq na viongozi wake (Check video on u tube titled blackwater christian crusiders) ndio utajua ninachoandika hapa.

Sasa kilichopo hapa ni kwamba nchi za Magharibi wala hazitakuwa tayari kuiona Zanzibar inakuwa mikononi mwa fundamental muslims kwa mfumo wa sasa, Zanzibar inafahamika kuwa kuna watu wengi waliokimbia wakati wa mapindizi wako uarabuni huko na wana nia ya kurudi.

Na kwa nyongeza kama tunavyojua kuwa yale mauaji ya januari 27 watu walikufa visiwani... ulishasikia nani amewahi ameshitakiwa?. Nafikiri hakuna hata mmoja na pia wakati wa mapinduzi kuna watu walikufa lakini wala uwezi sikia haya yakiongelewa nchi za magharibi.

Ndio hapo ninaposema kuwa Tanganyika ina uwezo wa kuimeza Zanzibar kwa karne hii . Zanzibar itakuja kuwa na nguvu tu ya kusimama pale ambapo mfumo kidunia utatawaliwa na uislam. Wale ndugu zangu waislamu msinichukie hii ni hali halisi dunia sasa ni ya kibepari na wale wanaojua kukua kwa ubepari kuliambana na dini gani wanajua ninachosema, sanasana unaweza soma Calvinism principles na kuenea kwa ubepari.

Tanganyika inaweza kufanya propaganda zozote na kuemeza Zanzibar zikakubalika duniani kwa sasa. Zanzibar inaangaliwa kwa jicho la tatu, hata waliolipua ubalozi wa Marekani Dsm nafikiri mmoja wao anajulikana anatoka wapi na mpaka sasa anatumikia kifungo nchi gani..Sasa ndio huko kujitawala ndugu zangu naona tu msahau karne hii.

Hizo blabla za bodi ya mikopo ni njaa tu inawasumua baadhi ya watu wanataka hela huko.. Kama CUF walivyokuwa wanapiga miayo wamemegewa keki kidogo sasa wako Kimya kabisa.

Msilaumu sana Tanganyika kuwa tunawang'ang'ania mfumo wa kidunia wa sasa hauwaruhu Zanzibar kuwa huru kwa historia yenu na culture yenu, Tanganyika ni kuhadi tu toka wakati wa mapinduzi. Hiyo security ya Tanganyika wala sio kweli. Mbona tumepaka na Rwanda na Burundi kule ni vita zinamelindima miaka mingi na bado hakujakaa sawa toka lini usalama wetu umeyumba?

Tumepakana na nchi nane kwa nini Zanzibar tu ndio iwe tishio?. Hayo maswali jiulizeni Wazanzibar, nyie wala si tishio kwa Tanganyika bali ni tishio kwa mfumo wa Kidunia na maslahi ya wakubwa wa Dunia. Tanganyika is negrigible in this.

Wakati mwingine madai ya Zanzibar kuwa huru huwa yakuwa kichekesho tu kwa watu wengine ambao wanajua Wanzanzibar mko ndotoni wala hamjui mfumo wa Dunia umelalia upande gani kwa sasa.

Ni wazi kuwa nchi nyingi za kiarabu zinatawaliwa na watu wenye maslahi kwa nchi za magharibi, itakuwa gharama kubwa kwa nchi za magharibi kuweka mamluki mzanzibar atawale wakati tupo sisi Tanganyika tunawamudu vizuri tu.
Zanzubar soveignity ni ndoto ya alinacha kwa sasa subirini vitukuu vyenu labda
 
Kwani Zanzibar inachangia asilimia ngapi katika Bodi ya Mikopo wandugu? Maana bajeti yao haifiki hata trilioni moja!
 
Babu Lao,

kwa hiyo watakuwa wanapata mikopo kutika sehemu 3?

  1. SMZ
  2. OIC
  3. HESLB
i hope watasoma kama wapo peponi.
 
Back
Top Bottom