Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Nonda,

Nashukuru kwa maoni yako, i have watched all 19 series pamoja na documentary ya Aljazeera nimekuelewa sana bwana Nonda. Tatizo ni kwamba, hawa jamaa wamagharibi wana Intertwined ambitions, ukingalia hizo series zinaonyesha uvamizi wa Iraq, Afghan n.k ulikuwa wa Kibiashara zaidi, pia wanaonyesha how America walivyotumia False Flag kubomoa WTC ili kuanzisha vita nchini Iraq.

Lakini pia tambua kuwa ni kiasi gani America inasurpport dini ya Ukisto katika bajeti yake dunia. It is believed pale kwenye Ukristo ni rahisi zaidi kupenyeza interest za mabepari kuliko pale penye uislam. Wakati wa vita baridi ilikuwa ni vigumu sana kwa America na mataifa mengine ya magharibi kuwekeza pale ambapo kuna mkono wa USSR hivyo walitumia pupet readers na kutrain waasi kama Savimbi ili kupata walichokihitaji.

Lakini baada ya Vita baridi viongozi wengi wa wakristo wanasign hiyo mikataba bila shida, na ndio ulikuwa mwisho wa vita kama za Angola.Sio siri kwamba sasa watu wa magharibi wanapata shida kufanya biashara na nchi za kiislam, wanachofanya ni kuwepo puppet leaders kama Akina Kaizar na wengine ili wasign mikataba wanayotaka. Na kwa sasa wakiangusha Libya nafikiri sasa itakuwa ni Iran kwani huko ndio kunaonekana bado hawajaweka mtu wao.

Lakini pia zote hizo plan zinabaraka ya Ukristo kwani pia zinatumika kudhoofisha nguvu ya uislam
Kuhusu kuweka hii thread mpya bwana Nonda muungano huu watu wanaufamu tofauti labda kuweka thread kama unataka kujua uelewa wa watu kuhusu kwamba kwa nini Tanganyika iliungana na Zanzibar ninauhakika hapo utapata maoni tofauti tofauti. Mengi ya maoni ninayoona humu ndani watu wanasema muungani huu uko kwa ajili ya viongozi wa ccm Zanzibar na Bara.

Nimezipenda series zako inawezekana sababu ya kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar ambazo watu wengi wanafundishwa mashuleni ikawa ni FALSE FLAG na sababu halisi zipo.Ila mheshimiwa role ya dini ipo sana na ni very sensitive kwa Tanzania, viongozi wengi hawapendi kuliongea hilo. Jikumbushe kauli ya Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania alipokuwa pro OIC miaka michache iliyopita , kilichoendelea makanisani haikuwa dini tena ilikuwa propaganda.
 
Last edited by a moderator:
dizzle1,
Mzanzibar aweza KUKUJIBU kwa kusema 'kama wewe hupendi sana wanachotaka Zanzibar kwa nini usimeze vipande vya chupa na unywe ili ufe'. Ninachotaka kusema ni kuwa mambo yote yanayoendelea na hiyo tabia ya Zanzibar yanalelewa na CCM. CCM ni kama kaopoa bi mdogo Zanzibar na haambiliki. Unawalaumu Zanzibar bure wakati wanalelewa na CCM, wenzako wanajua chochote wanachotaka watapewa leo ama kesho, sasa kwa nini unataka wachague kati ya 'kujitenga ama kufyata mkia'. Zanzibar itafyata mkia pale tu CCM itapoanguka.
 
Kwanza mimi nashangaa watalii wanaenda kutizama nini zanzibar,nlienda kutalii and to be honest nothng impressed me,absolutely nothng.
 
hivi inawezekana kila mkoa ikaanzisha bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na zipewe fedha na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Tanzania (HELSB)? maana hii itakuwa rahisi kufanya ratio ya mikoa mingine ya bara na hii ya unguja na pemba.

Zaidi ya hapo, huu upendeleo utafanana na ule wakina dada zetu mashuleni! Tuwe wakweli tu jamani...
 
Hivi hyo hela ya kuipa hiyo itayoitwa/inayoitwa HESLB ya zanzibar ya watanzania gani? kodi tukatwe sisi huku ili wakasomeshwe hatutakubali heri kila mtu ajitegemee kwa lake,
Muungano muungano tumechoka sasa faida yenyewe hatuioni,heri tuambiwe faida ya muungano kwanza baada ya hapo ndio tujue faida ya kuwasomesha wanzanzibar kwa hela ya watanganyika

Tunanyonyana tu bila msingi wowote
 
Historia ni historia si mchezo wa kuigiza. Zanzibar ilikuwa nchi na itaendelea kuwa hivyo. Hata sokwe huvishwa nguo kama binaadamu lakini hawi binaadamu.
nakubaliana nawe mkuu lakini pia ukumbuke kuwa 10km kutoka pwani (ufukweni) ilikuwa milki ya Sultan na sidhani kama haya makabila yataidai hiyo historia siku moja. Lakini tatizo la Zanzibar kujitenga ni sababu ya watu wachache wenye dharau (ya asili) juu ya wengine kama historia inavyoonyesha, wengine wanaingia kimkumbo na wataona matokeo yake baada ya hiyo 'split'. Fikiria mara mbili bili japo ni vigumu
 
Ngekewa,

Kamwe sijapinga Zanzibar kujitegemea wala kuwa huru na Muungano ndo maana katika post yangu niliwakumbusha kudeal na vitu ambavyo kweli vitaleta output nzuri ikiwa pamoja na free port na niliita bubu kwa kuwa Kenya wako race katika kujenga free port kule Lamu.

Na nilisema Zanzibar inajichanganya kwasababu inaunda bodi then inataka kupata share kutoka bodi ya mikopo ya muungano-ivi huku ndo kujitegemea bana Ngekewa-Tuwe serious katika issues jamani; Zanzibar inahitaji kuwa na Bandari Imara na Huru ili kuvutia Wafanyabiashara kutumia kama kituo cha kupitishia bidhaa zao.

Zanzibar inahitaji light Industries ili ipunguze wimbi la bidhaa zinazokuwa imported bila sababu za msingi, Zanzibar inahitaji msingi imara wa elimu ya msingi na Secondary hususan masomo ya sayansi ambayo vijana wengi huyakimbia na kuwa na matokeo mabaya kupita maelezo.

Zanzibar inahitaji kujenga miundo mbinu imara ili kuvutia watalii; Zanzibar inahitaji Shirika la Ndege ili kuifanya Zanzibar iwe tourist destination in East Africa; yaani mengi siyo Zanzibar loan board. Nasema loan Board kwa Zanzibar siyo tatizo kwani nnao jamaa ambao ni Wazanzibar na wasio wazanzibar wanaosoma vyuo vya zanzibar na wana-accesss loan from HELSB very easily.
 
@Straatkasyambe,

Wakati Mandela unapiganina uhuru, watu kama Straatkasyembe walikua wakisema Mandela unajisumbua bure,anapoteza muda, hatofanikiwa...it is always negatives. Wakati Obama anataka kugombania urais wa Marekani ,tena watu kama Straatkasyembe walisema huyu jamaa anajisumbua bure, wakati haujafika kwa mtu mweusi kuwa Rais wa Marekani , bora akae pembeni, it is always same negatives preaching. Mimi sishangai sana kama Tanzania itaendelea kuwa masikini sana kwa miaka mingi ijayo. it seems many people still live in fear and always afraid to face the challenges...I hope you change for the better of Tanganyika and Zanzibar.
 
Sababu za muungano kama zilikuwapo hivi sasa hazipo, na wala wananchi wa kawaida wa bara hatuoni faida wala umuhimu wa muungano huu. Nadhani umefika wakati wa wananchi kushirikishwa kwenye maamuzi ya muungano, inavyooenekana CCM wanalazimisha muungano huu sijui ni kwa faida ya nani.

Hawa ndugu zetu wazanzibar wanatatizo la ubinafsi, kama mtakumbuka siku waliposema kuna mafuta kwenye rasi ya Zanzibar walikurupuka na kusema mafuta si suala la muungano, hivi sasa hawana je wakipata si itakuwa balaa? Muungano ni suala la hiari serikali na CCM waache kuwaburuza wananchi kama kuna munufao ambayo mtanzania aneyeishi Songea ama Singida anayapata kutokana na muungano huu wayaseme na kuyaweka hadharani.
 
Ndugu Makandokando,

Huo 'mkoa', ninahisi una watu binafsi wanaomiliki karibu theluthi au zaidi ya uchumi wa Tanzania bara. Ndiyo kusema, hata muungano ungelivunjika, bado sehemu ya uchumi wa bara watakuwa wakiumiliki wao hasa katika magorofa makubwa ya kupangisha na vitega uchumi vingine muhimu: pengine hata ardhi. Katika muktadha huo, inawezekana hali ikawa kidogo zaidi ya nilivyoieleza. Jaribu kupiga taswira baada ya 'Azimio la Zanzibar' kutangazwa, ni maafisa wangapi wa kutoka visiwani humo waliinuka mara moja kiuchumi (tuseme kuwa matajiri wa kupindukia) kutokana na 'azimio' hilo. Na ni wangapi kutoka bara wamenufaika namna ile huko Zanzibar?

Na sizungumzii Wazanzibari wanaojidai kuwa wamiliki wa Dowans. Tafadhali unapozungumzia 'mkoa' huo, usisahau mambo muhimu kama hayo. Leo hii uvunje muungano, 'mkoa' huo utakumiliki zaidi kiuchumi (pengine hata kisiasa na kijamii) kuliko wewe Mtanzania wa bara, ambaye hata jina la taifa lako huna tena, unavyoweza kuwamiliki wao.

Hii ni Anschluss ambayo hatimaye inaweza isiwe na maana kwa wale walioizatiti.

Alamsiki
Ludovick Mwijage
 
Duuh hiyo kali na mpya kwangu, thnx for the updates,

Nadhani kinachofuata ni Zanzibar kujitangazia uhuru wake, mpk sasa wana sifa za kuwa taifa huru coz wana nyimbo ya taifa, wana jeshi lao, raisi wao, baraza la mawaziri, bunge na mipaka ya nchi yao walicho bakisha ni fedha yao wenyewe!

Najiuliza kila siku kwa nini tuna wang'ang'ania kiasi hicho?majibu huwa na pewa eti ni sababu za ki usalama kwani hatuwezi kulinda mipaka yetu Zanzibar wakijitoa?
 
Mimi sioni kama ni tatizo kwa Zanzibar kuanzisha bodi yao ya mikopo, cha msingi ni kwamba, chanzo cha mapato ya bodi hiyo iwe Serikali ya Zanzibar na siyo ya Muungano!
 
Nonda,

Na kuongeze,hapa zanzibar kuna kambi za jeshi 30,sijui kila kambi ina watanganyika wanganpi,pia FFU watanganyika,vikosi vyote ni watanganyika,wanafikika laki tatu,tuwapunguze katika ya milioni moja tutoe laki tatu- halafu kuna wengine wanaishi uraiyani ambao hao ndio wanatudhalilisha hapa kwa kuchana msahafu,na kutujengea makanisa ya udogo na madanguroo,,,wahapungui elfu hamsiniii.

Zanzibar ni nchi na itaendela kuwa hata kama ina watu 300 lakini ni nchi. yangu tu
 
foro.jpg
mimi zanzibar naifahamu vyema-hembu naomba upload picha yoyote iliopigwa zanzibar ambayo utakuwa umerizika nayo ili uthibitishe huo-u-paradise wao-mimi sijaona picha yoyote nzur zaid ya hio nilio upload

Nafikiri utaridhishwa,huo ndio mwanzo tu, tumeshaanza darajani na tunaelekea bwawani,,na kumalizia wilaya nyengine Zanzibar na soon kuna bandari huru Zanzibar kama Dubai kazi za kumwaga si utakuja kubeba gunia za mchele
 
@Straatkasyambe,
Nakuhakikishia ikiwa zanzbar itajipanda vizuri hao christian watapotea zanzibar kwa sabau vizazi vyao hapa zanzibar wanasilimu ili tuwape ndugu zetu walochanga changanya,pia tatizo hapa ambalo la kuongezeka christian ni kutokana hakuna control border ambayo ya kujua nani anaingia na kutoka,ndio maana wabara wanaingia kiholela na kumiliki ardhi na kupa mwanaya ya kuongeza ukiristo na madanguro,lakini kama si huu muungano kungelikuwa hakuna christian tena

KAZI ipo kwenu huko munautwana mwaka huu kwa siasa ya padri chadema,bora atawale muislamu kuliko christian mana wana chuki mbaya sana,sisi kulingania dini kwetu hatulazimishi,mazingira yetu tu utaingia mwenyewe uislamu,vita vya dini vimeisha sana.

Zanzibar ni nchi ya kistaarabu na watu wake wastaarabu sana,unatembea wala hupigwi kabari saa nane za usiku,,,

MUNGU IBARIKI ZANZIBAR.
 
Wachangiaji wakumbuke kuwa Zanzibar ni nchi na ina Rais wake, baraza lake la wawakilishi, lakini kwa upande mwingine Tanzania ni muungano wa nchi mbili, zipi? hii ya pili, Tanganyika, ndio iliyokufa na haipo, imemezwa na Zanzibar. Kinachotakiwa kwanza wabara waunde nchi yao na ndipo waanze kuzungumza. Huo ndio ukweli. Bara hakuna nchi, kuna Muungano, Tanganyika yangu iko wapi?
 
..Baada ya kufufuliwa kwa EAC,kulifanyika mchakato wa haraka wa kuanzisha shirikisho la Afrika Mashariki...Na kwa bahati mbaya watanzania wengi tumelazimishwa tuamini kuwa shirikisho la Afrika Mashariki ni zuri ati kwasababu tutapata fursa za kufanya biashara na nchi nyingine wanachama wa EAC,japo hakuna jitihada za kweli toka kwa viongozi wetu ambazo zitatusaidia sisi tufanye vizuri kwenye hilo shirikisho.Sijui shirikisho hili litakuwaje maana hapa kwetu Muungano ndio huo unaelekea kufa tena kifo cha hakika.Itakuwaje nchi iliyoshindwa kuujenga Muungano wa ndani ikakimbilia muungano na nchi nyingine nje ya nchi? Kwa kweli sipati picha na hilo shirikisho letu....Ngoja tuone...
 
Me daima huwa najiuliza nitawahadithia nini watoto na wajukuu zangu Historia ya Tanzania siku itakayo kuwa Muungano
 
Back
Top Bottom