Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

hahaha upemba na unguja sio ukabila,ni sawa na kuita wewe mtu wa arusha na wewe mtu wa ziwa la viktoria,huo sio utengano kwetu,kwani hao waunguja wengewe hapa zanzbar ni asilimia 10 tu,na hivyo basi hawako tena kutoka damu zimeshaingiliana zamani,na hapa kwetu zanzbar mambo haya ya ubaguzi yamekuja juzi tu,miaka 200 nyuma hayakuwapo,hizi zilikuwa ni agenda za ccm tu.

Kibaya zaidi bara,naona kuna makabila 200 hapo ndio tuuwana ,naona tanganyika itagawika vipe vipande kama sudani,kutokana uwongozi mbovu,rasilimali wanfaidika wao tu,watoto wenu waka kaa chini mashuleni,huko vijijini,hospitali hakuna ,wanaofaidika watu wa mjini tu,na hata hivyo unachangia huduma ya afya na elimu sasa jiulize pesa zinaenda wapi za rasilimali zenu,kama barabara zinajengwa kwa misaada,na afya na elimu,

Bado kazi kwenu ,,sisi kheri kwetu,,,
 
Kwani huyo sheikh yeye ninani hasa mpaka awasemee wazanzibar? aliyosema ni mawazo yake banafsi tena yasiyo na hekima, maana hekima ya mtu hupimwa kwa maneno na vitendo vyake.Huyu sheikh maneno na vitendo vyake vinaonyesha hana hekima kabisa, inawezekana hata elimu hana.

Inakuwaje badala ya kujadili muswada husika na kuupinga au kukubaliana nao kwa nguvu ya hoja yeye anaanza kumtukana nyerere na kuichana nakala ya muswada hadharani ha hatimaye kikao kuvunjika? hii ni akili kweli? Nakubaliana kwamba muswada huu haufai kabisa, na moja ya kutofaa kwake ni kutotaka kujadiliwa kwa masuala ya muungano, huo ni udhaifu, lakini tunapopata nafasi za kuujadili muungano ni vizuri kujadili namna ya kuuboresha siyo kuuvunja kwa kuwa mwelekeo wa siasa za dunia ni kuungana siyo kutengana.

Hivi huyo sheikh anaelewa hata dunia ilivyo kwa sasa? Kama mambo yenyewe ndio hayo hatutafanikiwa kwenda kwenda kwenye neema.
 
Nadhani kura ya maoni ndio suluhisho na si kubishan nani yuko sahihi.
 
Muswada wa Maboresho ya Katiba umeibua mambo mengi. Muswada huo umepingwa vikali na watu mbalimbali. Muswada huo umekuwa ukijadiliwa kwa hisia kali.

Kubwa kuliko yote mpaka sasa ni pale ambapo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipoamua kupingana na kutofautiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mawaziri wa SMZ, wabunge nk wamekuwa baridi kuhusu Muswada huo. Mwanasheria Mkuu wa Smz amesema wazi kwamba hakushirikishwa.

Serikali hizi zinaongozwa na CCM. Natambua CUF pia wana nafasi katika uongozi wa SMZ.

Mpaka sasa inaonekana CCM kama chama hakijakaa kujadili au kukubaliana kuhusu mchakato wa Katiba mpya. Tatizo lililopo CCM wamekurupuka na kudandia hoja ya Katiba bila kuwa na maandalizi kama chama. Endapo maandalizi yangekuwapo basi serikali hizi mbili zisingepingana na kulaumiana hadharani.

Kitendo cha Muswada huo kupingwa kwa nguvu ni wazi kabisa safari ya kuelekea kwenye katiba mpya haitakuwa rahisi. Ila naamini tutafika hata kama tutakuwa tumechoka.
 
Mimi nashangaa wanaoshangaa Kulingana na marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010 inasema kuwa Zanzibar ni nchi, kama ni nchi si ajabu serikali ya nchi moja kupingana na serikali ya nchi nyingine.
 
Only83,

Hiyo nchi nyingine ni ipi? Mipaka yake? Raisi wake? Mawaziri wake? Wabunge wake? Lakini, zaidi KATIBA yake iko wapi?

Kama Zanzibar ni basi Tanganyika ni nchi.
 
Nyumba inayojibomoa dhidi yake haiwezi kudumu,ccm inajibomoa yenyewe kamwe haitadumu
 
kwanza ukivunjika itakuwa vizuri-then watu wataishi pale wanapopenda-ni sawa na wakenya wanaoishi humu nchini-
 
ni sawa upeleke mswada wa katiba kenya-then wakugomee-wakat wao ni nchi nyingine na wanautaratibu wao na katiba yao tofauti-
 
Viza ya kuja Tanganyika itakuwa dola 3000 na kuapply lazima uchukue miezi 3 ndio upate.
 
Hakuna la ajabu SMZ kuipinga serikali ya muungano. Muasisi wa muungano Bw. Nassoro Moyo ametamka wazi na kumwambia Bw. Sitta kuwa "IT'S OVER". ama hamukusikia?. Mbona munajifanya hamuelewi?. Yamekwisha masuala ya muungano. zilioko sasa hivi ni babaisha tu.
 
Falconer, anaebabaisha ni nani? Kwanini SMZ wasiwe wazi na kusema wamejitoa kwenye Muungano? Je CCM kama chama wanalitambua hili? Wazanzibari wanawalaumu Watanganyika na kuwaacha viongozi wao. Huo uonevu viongozi wao hawauoni? Kwa nini viongozi wao wasichukue hatua?
 
Viza ya kuja Tanganyika itakuwa dola 3000 na kuapply lazima uchukue miezi 3 ndio upate.
AHAA sasa zanzbar ukija lazima owombe visa tena iyambatane na barua ya mualiko ya mzawa wa zanzibar akupatie,na visa itakuwa dola 100,ila lazima uwe na bank statement inayoonyesha una kiwango cha dola kuanzia elfu40,tutakusumbua kama ubalozi wa america na uk,suala la barua sijui mzanzibari gani atakupatia.
 
Swali langu ni hili aliua muungano ni nani? Isije tukaanza kusikia kama kawaida yao hili shirika la sisiem kuanza kutambaza maneno kwamba cdm wameua muungano. Tatizo la muungano lilikuwepo tangu hapo Nyerere alipokuja na hii idea na mpaka alipoondoka madarakani alishindwa ku-fix problems za huu muungano na kibaya zaidi hivi visiwa haviza sources za revenues na Mwinyi, Mkapa na sasa huyu fisadi kikwete ndio kabisa hajui analofanya yeye ana-worry about the wealth and bling bling.
 
tatizo lako husomi alama za nyakati JK NI RAISI WA KWANZA AFRICA KUTOA UHURU WA KUJIELEZA NA KUTOA MAONI ,KINACHOFANYIKA WATU WANATOA MAONI MBALI MBALI SI LAZIMA YAFANANE HIZI SIO ZAMA ZA MZEE KIFIMBO ,MWINYI &MKAPA,acha woga CCM inaimarika
 
muungano udumu bwana..hatutakawia kuingia zanzibar na viza..hivi ukivunjika tanzania bara itaitwajea?tanganyika tena?
 
Falconer, anaebabaisha ni nani? Kwanini SMZ wasiwe wazi na kusema wamejitoa kwenye Muungano? Je CCM kama chama wanalitambua hili? Wazanzibari wanawalaumu Watanganyika na kuwaacha viongozi wao. Huo uonevu viongozi wao hawauoni? Kwa nini viongozi wao wasichukue hatua?
Viongozi wepi unaowataka wewetena, Mwanasheria Mkuu, Wawakilishi na Mawaziri wameshapinga sasa unataka viongozi wepi?

Zanzibar haitaki kuwa sawa na wenzao kujiamulia mambo bila kushirikishana na ndio maana wanasema Tanganyika ije ili jambo hili lizungumzwe. Tanganyika hamtaki kujitowa kwenye ngozi mliyojivika ya Muungano sasa Zanzibar itazungumza na nani? Wale wanaoufananisha huu muungano kama ndowa inapotokea mume nae anavaa upande wa kanga hali inakuwaje?
 
Swali langu ni hili aliua muungano ni nani? Isije tukaanza kusikia kama kawaida yao hili shirika la sisiem kuanza kutambaza maneno kwamba cdm wameua muungano. Tatizo la muungano lilikuwepo tangu hapo Nyerere alipokuja na hii idea na mpaka alipoondoka madarakani alishindwa ku-fix problems za huu muungano na kibaya zaidi hivi visiwa haviza sources za revenues na Mwinyi, Mkapa na sasa huyu fisadi kikwete ndio kabisa hajui analofanya yeye ana-worry about the wealth and bling bling.


Naungana nawe kwa hili CDM hawamo mpaka sasa, sijui wanaogopa au wao kwa hili wako pamoja na CCM kungangania?
 
Back
Top Bottom