Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Live kutoka mbeya dr kitila mkumbo yuko anaongea na wananchi ukumbi wa mtenda sun set,ameanza kwa kuwapongeza waandaji na namna walivyo andaa na kwa kueleza namna muungano wa serikali yetu ilivyo.toa maoni yako
 
Kwa maoni yangu muungano hauna faida yoyote kwani sababu zilizotolewa kwa kuunganisha muungano hazipo tena na ziko irrelevant,kimsingi muungano ulianzishwa kama taadhari ya cold war ya wakati ule,ndio maana suala la maadui wa nje linazungumziwa sana katika uanzilishi,cold war illisha siku nyingi na nchi zilizokuwa na miungano ya aina hiyo mfano USSR tayari waliisha ivunja.Niliwahi kumuomba msomi mmoja aliyebobea mambo ya siasa anieleze faida 10 za muungano,lakini alishindwa hata kunitajia moja[KWA ILI ANAYEJUA ANGALAU FAIDA 5 ZA MUUNGANO AJITOKEZE NA KUZITAJA].Watu wa Zanzibar ndio wanafaidika zaidi na mfumo wa muungano uliopo,kwa bara hakuna faida yoyote,wabunge wote waliopo kwenye bunge la muungano,mawaziri,watumishi wa umma etc kama tukivunja muungano hawana pa kwenda na kwa ukumbwa wa Zanzibar haiwezi kuwa accomodate,wazanzibar waliopo bara nadhani ni idadi sawa na walioko visiwani,tukivunja Muungano wataenda wapi,hakuna wakunishawishi kuwa muungano una faida yoyote kwa watu wa bara
 
Napata shida sana kuendelea kupiga debe muungano muungano. Kwa mtanzania wa kawaida kuna faida gani za muungano? au tunapigia debe ili kuwanufaisha viongozi walafi haswa wakati wa kujitengea mapesa wakati wa sherehe kama za leo?

Kwa wewe mtanzania raia kuna lipi la kujivunia kwenye muungano huu. Ningepenga huu muungano uwe wa wananchi kwa ridhaa yao na siyo kama tunavyokaririshwa kuwa waasisi wa muungano walikuwa karume na nyerere na siyo watanzania. Huu ni upuuzi na pengine unahitajika ama kupiga kura au kufanya mchakato wa kuona faida za kuendelea kuwepo muungano.

kwa mimi wa bara naona unaleta ulaji wa wazanzibari kwa kutenga bajeti kubwa kwa nchi ya zanzibar eneo ambalo ni sawa tu na mkoa wa kilimanjaro.
 
Ukitaka kujua upande gani hautaki muungano tuamuae kuwa na serikali moja hapo ndipo ukweli utakapodhihirika na unafiki wa watu fulani utawekwa hadharani, muungano wa kweli na thabiti ni ule wa serikali moja tu na sio serikali mbili wala tatu, mfano mwanamke na mwanaume wanafunga ndoa halafu kila mtu anaenda kuishi kwa wazazi wake baada ya ndoa, je hiyo itakuwa ndoa imara na yenye hadhi!?
 
Jamani Wadau mimi bado sijajua ukweli.
Nasikia tu Watu wanabishana kuhusu Muungano, wakisema hauna tija, Hivi Kero kuu ya Muungano zinazo sababisha mabishano hayo ni nini?
Na Wakati nchi mbili zinaamua kuungana, kulikuwa na Makubaliano yepi?
Je yaliwekwa kwenye file, yaani Memorandam of Understanding?
Nini kunacho kusababisha wewe uone Muungano hauna tija au unatija?
Je Mtu kutoka Zanzibar anahaki ya kuwa Raisi wa Jamuhuli ya Muungano wa Tanzania? Kwa kufuata makubaliano hayo yaliyo fikiwa?
Naomba Muni tatulie kidogo maana natatanika kuhusu hilo.
 
kero za muungano ni muungano wenyewe.
Ivi kaka mimi na wewe tukikubaliana kuwa marafiki tukaishi hivo kwa muda mara mie nikaamua nisiwe rafiki yako kwanini wewe ung'ang'anie kuwa rafiki yangu? I mean kwa nini Bara tunang'ang'ania kuwa na muungano na wakati upande wa pili hawautaki?
 
Muundano????
Waacheni jamani wanaoitaka nchi yao waichukue
 
Swali hili Nape na Magamba wengine wangeweza kutujibu vizuri sana.
 
Hamna Muungano wa kuvunjika, Zanzibar itaweza kulipa gharama za damu, jasho, pesa na watu wa Tanganyika walipokuwa wanakombolea na Mwalimu?
 
Jamani watu mmeambiwa faida na hasara mnaanza porojo....shit.............
Hasara ni kwa wa Tanganyika ni kubebeshwa mzigo wa wazanzibar kama kuwalipa msharaha, umeme....... mjitu kutoka zanzibar......
 
Hamna Muungano wa kuvunjika, Zanzibar itaweza kulipa gharama za damu, jasho, pesa na watu wa Tanganyika walipokuwa wanakombolea na Mwalimu?
Kwa hiyo malipo ya watanganyika walio kufa ni kuendelea na muungano.....yaani umenikumbusha na jaama mmoja alimosomesha demu tangu akiwa sekondari mpaka chuo lakini jamaa akaja akapiga kibuti mpaka leo anauguza maumivu...
 
Asnte sana kwa link hiyo umenifanya nijue mambo mengi sana ya waznz acha niya fatilie....


Crashwise tumegee hata kwa ufupi sisi wenye vimeo aka simu.
 
Last edited by a moderator:
Faida nyingi wanapata wazanzibar. Yaani waruhusiwa kumiliki ardhi bara na unguja.wanaruhusiwa kugombea uongozi bara au zanzibar. Wana bunge lao, rais wao, bendera yao, wimbo wao. Nk. Lakini bado wanalalamika tu. Hawatosheki tu labda mji mku uwe zanzibar!
 
Faida nyingi wanapata wazanzibar. Yaani waruhusiwa kumiliki ardhi bara na unguja.wanaruhusiwa kugombea uongozi bara au zanzibar. Wana bunge lao, rais wao, bendera yao, wimbo wao. Nk. Lakini bado wanalalamika tu. Hawatosheki tu labda mji mku uwe zanzibar!
Wazanzibari ni wezi na ni wanyang'anyi bila hata huruma, hebu tafuteni stori za Watanganyika wanavyonyanyaswa kwao, na isingekuwa uoga wa umma wa tanganyika kujibu (sio serikali) bunge lao lilikuwa lipitishe muswada wa kurudisha wabara wote kama wakimbizi, walisahau hao wabara wachache wameenda juzi tu na ni kwa sekta moja ya Utalii tu, na wale walioenda kupindua mwa 64, nusu yao wazanzibari pamoja na viongozi wapo bara na Mungu atunusuru kwani ni maadui wakubwa hawa, hasa hawa walioko serikalini.
 
Mwenzenu ninapata kigugumizi juu ya MUUNGANO. Hivi Huu muungano ambao aka yake JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Je, ni mali ya nani? Ni watanzania?, Wazanzibar? Watanganyika? ama rais JK? Hii katiba ambayo watanzania wanaenda kuijadili, haihusishi Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania? Kama inahusu, kwa nini mambo ya MUUNGANO yasipate kujadiliwa? Hivi anyekataa MUUNGANO kujadiliwa yeye ana agenda gani ambayo watanzania haturuhusiwi kuifahamu? Maswali ni mengi lakini majibu sipati, naishia kusema Kama MUUNGANO ni mali ya UMMA basi umma uachwe ujadili mali yake, na kama MUUNGANO ni mali ya MTU binafsi Nawaomba Watanzania tusiuguse katu.
 
Back
Top Bottom