Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano ulifanyika kumzuia Sultan kurudi Visiwani hata akipata msaada wa kijeshi kutoka Oman. Hili limefanikiwa lakini aliyelifanikisha amewaacha Wangazija na Wapemba umasikini mkubwa.

Kiuchumi Sultani angekuwepo sasa hivi Visiwa vingekua kama Dubai.
 
Tarehe 26 mwezi huu tunaadhimisha miaka 57 ya muungano. Miaka 57 ni umri wa mtu anayekwenda kustaafu, kama ni mtumishi.

Naomba wanaofahamu manufaa yaliyopatikana kwa Tanganyika, ambayo pengine bila kuungana yasingepatikana wanijulishe na mimi niweze kuyafahamu.
Faida kubwa. Samia kuwa rais.

Bila muungano angebakia kuwa mwakilishi wa Jimbo la Uzini
 
Muungano ulifanyika kumzuia Sultan kurudi Visiwani hata akipata msaada wa kijeshi kutoka Oman. Hili limefanikiwa lakini aliyelifanikisha amewaacha Wangazija na Wapemba umasikini mkubwa.

Kiuchumi Sultani angekuwepo sasa hivi Visiwa vingekua kama Dubai.
Sijaelewa. Tanganyika imepora utajiri wa Zanzibar? Au kinachozuia wasiwe kama Dubai ni kitu gani!
 
Hapana haikupora lakini Zanzibar haiko huru kufanya maamuzi na kuingia mikataba kama nchi.
If that is the case, urais wa Samia ni golden opportunity kwao. Waitumie miaka hii 4 ya Samia kurejesha uhuru wa kujiamulia mambo yao.
 
If that is the case, urais wa Samia ni golden opportunity kwao. Waitumie miaka hii 4 ya Samia kurejesha uhuru wa kujiamulia mambo yao.
Kumbuka kuna katiba, ni mpaka mambo haya yajadiliwe bungeni. Kama Mama ataruhusu mchakato wa katiba mpaya itasaidia sana.
 
Kumbuka kuna katiba, ni mpaka mambo haya yajadiliwe bungeni. Kama Mama ataruhusu mchakato wa katiba mpaya itasaidia sana.
Miaka 4 ni mingi sana kurekebisha vifungu vya katiba kandamizi kama vipo. Hii ni tofauti na mchakato wa kuandika katiba mpya ambao keshasema si kipaumbele chake.
 
Aiseeh. Humo mwenu akili zenu mnazijua ninyi wenyewe . Kwa hiyo tunawakalia ili tupate kodi zao ?!. Kwani hawawezi kutoa kodi kama wawekezaji wengine ambao ni foreigners wakiwa huru.

Foreigners hata sasa wanaruhusiwa kuwekeza lakini hawajawafikia wapemba

Hawawezi kuwafikia wapemba kwa uwingi na kuwekeza kila kona na kila sita

Pia kwao soko dogo na Ardhi ndogo. Nchi ina watu milioni moja tu na kitu .kibiashara hailipi kule kwao ndio.maana wanajazana Tanzania bara huku ndiko wanaibukia kuwa mabilione. Hivyo muungano una faida kubwa kwao kiuchumi.Wao wanatajirika kupitia sisi Tanzania bara na sisi tunanyanyuka kiuchumi kupitia kodi zao.Ni win win situation
 
Hizo ni choko choko,
Muuliza swali si mjenzi ila mbomoaji.
Watu tunahitaji kujenga uchumi mifukoni ,wewe unakuja na hila zako.
Tuache tupambane na hali zetu,wewe unatafuta wafuasi ili uibomoe nchi, hutafanikiwa.
 
Tarehe 26 mwezi huu tunaadhimisha miaka 57 ya muungano. Miaka 57 ni umri wa mtu anayekwenda kustaafu, kama ni mtumishi.

Naomba wanaofahamu manufaa yaliyopatikana kwa Tanganyika, ambayo pengine bila kuungana yasingepatikana wanijulishe na mimi niweze kuyafahamu.
Faida ziko nyingi wanasemaga wala keki ya taifa
Faida moja wapo ni watu wa Bara kwenye honeymoon Zanzibar[emoji1787][emoji1787]
 
Hizo ni choko choko,
Muuliza swali si mjenzi ila mbomoaji.
Watu tunahitaji kujenga uchumi mifukoni ,wewe unakuja na hila zako.
Tuache tupambane na hali zetu,wewe unatafuta wafuasi ili uibomoe nchi, hutafanikiwa.
Huna hoja.
 
Tanzania bara inafaidika kodi na ajira kutoka kwa wafanyabiashara wapemba wakiwemo akina bakhresa nk

Kwenye sekta binafsi wapemba ndio huongoza kuingizia Tanzania bara kodi
Wapemba wanachangia kodi kuliko Wahindi? Ile Kariakoo tukiondoka wahindi nani anabaki? Kwenye michezo tukiondoa wahindi na waarabu nani anabaki?
 
Back
Top Bottom