Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Huu muungano upo kuwazubaisha hao jamaa wakiachwa "huru" wanaweza leta shida mbele ya safari.

Ila ndio unakera kweli, sasa tunawabembeleza kama watoto, pesa za sherehe ya muungano tugawane sawa, hizi pesa zilizotokana na walipa kodi wa bara, kwani huko Zanzibar hawana pesa kwa ajili ya hizo sherehe?
Ndiyo maana nasema ifike mahali tuwaachie wenyewe wajipangie mambo yao.

Maana wanadai Serikali ya Muungano inawadhibiti wakitaka kushirikiana na nchi za OIC ambazo ziko tayari kutoa mikopo ya uwekezaji isiyo na riba.
 
Leo tunasherekea miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi kabla ya 1964 na Muungano tuliokuwa nao ni "marriage of convenience" kwa wakati ule kwenye kipindi cha vita baridi (NATO/ Warsaw Pact).

Ni USA kupitia kachero wao Frank Carlucci aliyekuwa Balozi wao Tanganyika kisha Congo na baadaye akaja kuwa CEO wa CIA. Huyu Carlucci alianza kumshawishi kwanza Jomo Kenyatta kutaka kuiunganisha Zanzibar na Kenya. Jomo Kenyatta atakataa ndipo akamu approach J K Nyerere ambaye alikubali.

Nyerere aliweka muundo wa Serikali 2 ili kutoimeza Zanzibar kama nchi. Alikataa kabisa kuifanya Zanzibar kuwa Mkoa. Hata hivyo vita baridi ilikwisha mwaka 1989 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin. Ushahidi upo kwenye Rasimu ya Katiba ya Warioba uliotaka Serikali 3.

Sababu ya kuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sasa hazipo. Tunahitaji tu kuwa na ushirikiano kama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Yeyote anayetaka ridhaaa ya kura za Wazanzibari lazima aongelee "sovereignty ya Zanzibar" as a country.

Zanzibar ilikuwa tajiri sana kuliko Oman kabla ya mwaka 1960 na ndiyo sababu Sultan Seyyid Said alihamisha Makao makuu ya Sultanate of Oman kwenda Zanzibar mmamo 1840. Mwaka 1960 kwa mfano Zanzibar ilikuwa na kilometres 22 za barabara ya lami wakati Oman ilikuwa haina. Leo hii Oman ni nchi tajiri sana baada ya kugundua raslimali za mafuta mpaka imekuwa nchi mfadhili.

Mimi ni Mtanganyika naamini kuwa muda wa kuendelea kuishikilia Zanzibar umekwisha. Tuwaache wapate maendeleo kipitia OIC na waanzishe bandari huru kama ilivyo Singapore na Dubai.

Zanzibar imecheleweshwa mno kiuchumi kwa kuwa ndani ya Tanganyika.
Umenena na una pwenti mwanangu.
 
Mkuu kwa mfano, muungano uvunjike leo, tugawane rasilimali! Wazenji wanachukua rais wa jamuhuri ya muungano, Sisi tutabaki na Nani, Mpango?!
Mpaka tu-adopt Serikali 3 kama zilivyo kwenye Rasimu ya Katiba ya Warioba. Kwa mfumo wa Serikali 2 ni Dr Hussein Mwinyi tu wa ZNZ ndiyo anauhakika na nafasi yake.
 
Acha ujinga wewe, hujui kuwa muungano ukivunjika sasa hivi Wazanzibari wanamchukua Rais wetu?
Huu muungano uendelee kudumu tu.
 
Leo tunasherekea miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi kabla ya 1964 na Muungano tuliokuwa nao ni "marriage of convenience" kwa wakati ule kwenye kipindi cha vita baridi (NATO/ Warsaw Pact).

Ni USA kupitia kachero wao Frank Carlucci aliyekuwa Balozi wao Tanganyika kisha Congo na baadaye akaja kuwa CEO wa CIA. Huyu Carlucci alianza kumshawishi kwanza Jomo Kenyatta kutaka kuiunganisha Zanzibar na Kenya. Jomo Kenyatta atakataa ndipo akamu approach J K Nyerere ambaye alikubali.

Nyerere aliweka muundo wa Serikali 2 ili kutoimeza Zanzibar kama nchi. Alikataa kabisa kuifanya Zanzibar kuwa Mkoa. Hata hivyo vita baridi ilikwisha mwaka 1989 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin. Ushahidi upo kwenye Rasimu ya Katiba ya Warioba uliotaka Serikali 3.

Sababu ya kuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sasa hazipo. Tunahitaji tu kuwa na ushirikiano kama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Yeyote anayetaka ridhaaa ya kura za Wazanzibari lazima aongelee "sovereignty ya Zanzibar" as a country.

Zanzibar ilikuwa tajiri sana kuliko Oman kabla ya mwaka 1960 na ndiyo sababu Sultan Seyyid Said alihamisha Makao makuu ya Sultanate of Oman kwenda Zanzibar mmamo 1840. Mwaka 1960 kwa mfano Zanzibar ilikuwa na kilometres 22 za barabara ya lami wakati Oman ilikuwa haina. Leo hii Oman ni nchi tajiri sana baada ya kugundua raslimali za mafuta mpaka imekuwa nchi mfadhili.

Mimi ni Mtanganyika naamini kuwa muda wa kuendelea kuishikilia Zanzibar umekwisha. Tuwaache wapate maendeleo kipitia OIC na waanzishe bandari huru kama ilivyo Singapore na Dubai.

Zanzibar imecheleweshwa mno kiuchumi kwa kuwa ndani ya Tanganyika.
Hawataweza kuanzisha Bandar huru kama Singapore au Dubai. Watamuuzia Nani mizigo Yao wataipeleka wapi mbona kuna nchi kama Madagascar, Seychelles au Comoros na Mauritius au Cape Verde hazijawa kama Singapore au Dubai.
 
Mwenye kufahamu historia ya G55 watupe mtazamo wa watu hawa kuhusu muungano.
Katika kikao cha Bunge la Bajeti cha mwaka 1993, aliyekuwa Mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Njelu Kasaka aliwasilisha hoja binafsi bungeni ya kudai Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. Wabunge 55 waliokuja kufahamika kama G55, wakiongozwa na mtoa hoja, Njelu Kasaka, waliiunga mkono hoja hiyo na pia ikapata baraka za Waziri Mkuu wa wakati huo, John Samwel Malecela 'Cigwiyemisi' na kupitishwa na Spika wa Bunge , marehemu Chifu Adam Sapi Mkwawa ili ijadiliwe. Baadaye walikuja kuongezeka na kufikia 65 (G65?)

Hii hapa ni orodha ninayoamini ilikuwa ya G55 ingawa natanguliza samahani kuwa sina hakika na majina mawili matatu na wapo niliowasahau ila kwa msisitizo; Jaji Sinde Joseph Warioba hakuwa moja wao. Kwamba Jaji alikuwa kwenye G55 ni habari ambayo chanzo chake ni CCM katika jitihada za kujaribu kuinusuru CCM kwa kumpaka matope huyo shujaa wa Watanzania.

  1. John Samwel Malecela, (Mtera, Waziri Mkuu)
  2. Horace Kolimba?
  3. Njelu Kasaka (Lupa)
  4. Mateo Tluway Qaresi (Babati)
  5. Jenerali Twaha Khalfani Ulimwengu (Taifa/Jumuiya ya Vijana)
  6. Ahmed A. Mpakani (Iringa Magharibi)
  7. Paschal K. Mabiti (Mwanza)
  8. Luteni Lepilal Ole Moloimet (Monduli)
  9. Lumuli Alipipi Kasyupa (Kyela)
  10. Profesa Aaron Masawe (Hai)
  11. Arcado Ntagazwa (Kibondo).
  12. Phineas Nnko (Arumeru Mashariki)
  13. Paschal Degera (Kondoa Kusini)
  14. Mussa Nkhangaa (Singida Mjini)
  15. Halimenshi Kahema Mayonga (Kigoma Kaskazini)
  16. Said Abdallah Nakuwa (Lindi Mjini)
  17. Mosi Tambwe (Taifa/Wanawake).
  18. Luteni Kanali John Mhina (Muheza)
  19. Charles Kagonji (Mlalo),
  20. Kisyeri Werema Chambiri (Tarime)
  21. Tobi Tajiri Mweri (Pangani)
  22. William H. Mpiluka (Mufindi)
  23. Aidan Livigha (Ruangwa)
  24. Philip Sanka Marmo (Mbulu)
  25. Erasto K. Lossioki (Simanjiro)
  26. Shamim Khan (Morogoro Mjini)
  27. Raphael Shempemba (Lushoto)
  28. Pachal Degera (Kondoa)
  29. Tuntemeke Sanga [Makete]
  30. Mbwete Polile Hombee (Mbeya Vijijini)
  31. John Byeitima (Karagwe)
  32. Chediel Yohane Mgonja (same)
  33. Japhet Sichona (Mbozi),
  34. Benedict Losurutia (Kiteto)
  35. Dk. Mganga Kipuyo (Arumeru Magharibi)
  36. Stanley Kinuno (Nyang'hwale)
  37. Dk. Aaron Chiduo (Gairo)
  38. Edward Oyombe Ayila (Rorya)
  39. Shashu Lugeye (Solwa).
  40. John Mwanga (Moshi Mjini)
  41. Dk. Deogratius Mwita (Serengeti)
  42. Abel Mwanga (Musoma Mjini)
  43. Juma Jamaldin Akukweti (Tunduru)
  44. Patrick Silvanus Qorro (Karatu)
  45. Steven Mwaduma (Iringa Mashariki)
  46. Dk. Ndembwela Ngunangwa (Njombe Kusini),
  47. Richard Koillah (Ngorongoro),
  48. Leipilal Ole Molloimet [Monduli]
  49. Phares Kabuye (Biharamulo - alihamia CUF)
  50. Evarist Mwanansao (Nkasi)
  51. Mussa Masomo (Handeni)
  52. Jared Ghachocha (Ngara)
  53. Mariam Kamm (Taifa/Wanawake).
  54. Kuwayawaya Stephen
  55. Masoud Masoud (Temeke) ?
  56. Gerald Gachocha?
  57. John Elikana Byeitima?
  58. Mrs Tabitha Siwale ?
  59. Laipalal Ole Moiloitmet (Longido)
 
Leo tunasherekea miaka 56 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi kabla ya 1964 na Muungano tuliokuwa nao ni "marriage of convenience" kwa wakati ule kwenye kipindi cha vita baridi (NATO/ Warsaw Pact).

Ni USA kupitia kachero wao Frank Carlucci aliyekuwa Balozi wao Tanganyika kisha Congo na baadaye akaja kuwa CEO wa CIA. Huyu Carlucci alianza kumshawishi kwanza Jomo Kenyatta kutaka kuiunganisha Zanzibar na Kenya. Jomo Kenyatta atakataa ndipo akamu approach J K Nyerere ambaye alikubali.

Nyerere aliweka muundo wa Serikali 2 ili kutoimeza Zanzibar kama nchi. Alikataa kabisa kuifanya Zanzibar kuwa Mkoa. Hata hivyo vita baridi ilikwisha mwaka 1989 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin. Ushahidi upo kwenye Rasimu ya Katiba ya Warioba uliotaka Serikali 3.

Sababu ya kuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sasa hazipo. Tunahitaji tu kuwa na ushirikiano kama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Yeyote anayetaka ridhaaa ya kura za Wazanzibari lazima aongelee "sovereignty ya Zanzibar" as a country.

Zanzibar ilikuwa tajiri sana kuliko Oman kabla ya mwaka 1960 na ndiyo sababu Sultan Seyyid Said alihamisha Makao makuu ya Sultanate of Oman kwenda Zanzibar mmamo 1840. Mwaka 1960 kwa mfano Zanzibar ilikuwa na kilometres 22 za barabara ya lami wakati Oman ilikuwa haina. Leo hii Oman ni nchi tajiri sana baada ya kugundua raslimali za mafuta mpaka imekuwa nchi mfadhili.

Mimi ni Mtanganyika naamini kuwa muda wa kuendelea kuishikilia Zanzibar umekwisha. Tuwaache wapate maendeleo kipitia OIC na waanzishe bandari huru kama ilivyo Singapore na Dubai.

Zanzibar imecheleweshwa mno kiuchumi kwa kuwa ndani ya Tanganyika.
Muungano ungekuwa muhimu kiasi hicho basi ungekuta leo hii dunia ni moja na hakuna mipaka ya ki nchi. lakini lazima ujue kila mipaka ina maana na umuhimu wake, hao waliotuwekea hii mipaka ya ki nchi walifikiri na kutizama mbali sana. Na ndio maana kila ukivuka mpaka wa taifa moja kwenda jingine hukutana na watu wa tofauti kabisa na wale wa taifa ulilotoka.

Bila Muungano wa kitaifa bado maisha yanawezekana maana cha muhimu si muungano bali ushirikiano. Taifa moja laweza kushirikiana na taifa jingine katika mambo flani flani bila kuungana na mifano tunayo kama SADC au EAC.

Tanganika na Zanzibar zaweza kuwa na ushirikano kwa mambo hayo tunayoyaita ya Muungano lakini Kila taifa likawa huru hivyo kusiwe na Rais wa Muungano. iwepo tu Commission ya shirikisho itakayoratibu na kusimamia hayo mambo ya shirikisho thats it.

Pemba kuwa na serikali yake na Unguja kuwa na yake bado si tatizo kama uwepo wake utakuwa ndio maedeleo kwa wapemba na waunguja.

Kwa jinsi serikali moja inaposimamia eneo kubwa ndivyo inavyokuwa taabu kwa serikali hiyo kuhudumia watu wa eneo hilo.

Kama inabidi hata hiyo tunayoitaka iwe Tanganyika inabidi iwe na sub governments ambazo zitachaguliwa na wananchi wa eneo husika.

Mwisho. Muungano ni mzuri lakini ni pale tu unapokuwa kwa faida ya wote na si kwa wachache
 
Huu muungano upo kuwazubaisha hao jamaa wakiachwa "huru" wanaweza leta shida mbele ya safari.

Ila ndio unakera kweli, sasa tunawabembeleza kama watoto, pesa za sherehe ya muungano tugawane sawa, hizi pesa zilizotokana na walipa kodi wa bara, kwani huko Zanzibar hawana pesa kwa ajili ya hizo sherehe?
Linalotakiwa ni kuwauliza watanzania ni aina gani ya muungano wanapenda au wanapendelea. Jibu la wengi ni kuwa na serikali tatu ingawa mwalimu Nyerere alitahadhalisha gharama ya kuendesha serikali tatu hatuwezi na mzigo mkubwa utaiangukia Tanganyika, kuwa na serikali moja kamwe visiwani hawatokubali. Kama itatokea tusielewane ni heri tuachane salama kila upande uwe na serikali yake ili tujenge nchi zetu. Tanganyika waijenge tanganyika yao na wazanzibari waijenge zanzibar yao. Tutashirikiana kiuchumi, kijamii na kisiasa. Iwapo hili likitokea, basi utanzania umeisha na hakutokuwa na taifa la Tanzania. Sasa basi, kama hutakiwi kuwa mtanganyika au mzanzibari basi jiandae kuwa raia wa nchi nyingine tofauti na hizo mbili tajwa hapo juu. Sijui utasafiria passport gani, utakuwa na kitambulisho gani, nadhani unayasema haya kwa kuwa hayajatokea, ikitokea huna pa kwenda ndugu yangu. Tusingependa kuona hayo yote yakitokea kwa kuwa na mimi mwenyewe naupenda muungano wetu. Serikali 2 ni mzigo kwa raia wote, tujadili la serikali 3
 
Leo tunasherekea miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar ilikuwa nchi kabla ya 1964 na Muungano tuliokuwa nao ni "marriage of convenience" kwa wakati ule kwenye kipindi cha vita baridi (NATO/ Warsaw Pact).

Ni USA kupitia kachero wao Frank Carlucci aliyekuwa Balozi wao Tanganyika kisha Congo na baadaye akaja kuwa CEO wa CIA. Huyu Carlucci alianza kumshawishi kwanza Jomo Kenyatta kutaka kuiunganisha Zanzibar na Kenya. Jomo Kenyatta atakataa ndipo akamu approach J K Nyerere ambaye alikubali.

Nyerere aliweka muundo wa Serikali 2 ili kutoimeza Zanzibar kama nchi. Alikataa kabisa kuifanya Zanzibar kuwa Mkoa. Hata hivyo vita baridi ilikwisha mwaka 1989 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin. Ushahidi upo kwenye Rasimu ya Katiba ya Warioba uliotaka Serikali 3.

Sababu ya kuwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sasa hazipo. Tunahitaji tu kuwa na ushirikiano kama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Yeyote anayetaka ridhaaa ya kura za Wazanzibari lazima aongelee "sovereignty ya Zanzibar" as a country.

Zanzibar ilikuwa tajiri sana kuliko Oman kabla ya mwaka 1960 na ndiyo sababu Sultan Seyyid Said alihamisha Makao makuu ya Sultanate of Oman kwenda Zanzibar mmamo 1840. Mwaka 1960 kwa mfano Zanzibar ilikuwa na kilometres 22 za barabara ya lami wakati Oman ilikuwa haina. Leo hii Oman ni nchi tajiri sana baada ya kugundua raslimali za mafuta mpaka imekuwa nchi mfadhili.

Mimi ni Mtanganyika naamini kuwa muda wa kuendelea kuishikilia Zanzibar umekwisha. Tuwaache wapate maendeleo kipitia OIC na waanzishe bandari huru kama ilivyo Singapore na Dubai.

Zanzibar imecheleweshwa mno kiuchumi kwa kuwa ndani ya Tanganyika.
Zanzibar ni kupe kwa Tanganyika
Wasepe tuu
Wakawe Singapore kama wanavyoota
 
Mkuu kwa mfano, muungano uvunjike leo, tugawane rasilimali! Wazenji wanachukua rais wa jamuhuri ya muungano, Sisi tutabaki na Nani, Mpango?!
Philip Mpango & Majaliwa Kasim Majaliwa

Zanzibar wasepeee
 
Huu muungano upo kuwazubaisha hao jamaa wakiachwa "huru" wanaweza leta shida mbele ya safari.

Ila ndio unakera kweli, sasa tunawabembeleza kama watoto, pesa za sherehe ya muungano tugawane sawa, hizi pesa zilizotokana na walipa kodi wa bara, kwani huko Zanzibar hawana pesa kwa ajili ya hizo sherehe?
Nini wanafanya TRA ndani ya Zanzibar??
 
Katika kipindi hiki ambacho tunaongoza huku Zanzibar na kule Bara ni wakati wa kuhakikisha kuwa tunajitahidi kuirudisha nchi yetu mikononi mwetu.

Tumekuwa chini ya Utawala wa Tanganyika kwa miaka mingi sana tukilazimishwa kuunganishwa kwa lazima. Binafsi sijawahi ona faida ya huu Muungano Uchwara zaidi ya Tanganyika kutunyonya na kufaidika nasi.

Zanzibar ni moja ya sehemu bora kabisa za Utalii. Ambayo inaweza endesha maisha yake kwa kutumia Utalii tu. Lakini pia kwa kutumia ndugu zetu na marafiki wa nchi kadhaa za Kiarabu hasa Oman ambako wamekuwa na nia ya dhati ya kutaka kutusaidia. Ila wamekwama kutokana na mfumo huu wa sasa wa kinyonyaji.

Tunahitaji kuwa Huru. Kwa nini mnataka kutulazimisha kuungana nanyi? Kama mke hakutaki si unamwacha?
 
Back
Top Bottom