Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Mke hakutaki na analalamika kuwa unampiga kila siku lakini cha ajabu hataki kuondoka! Zanzibar ina serikali yake na baraza lake la Mapinduzi. Zaidi ya hapo ina wabunge wengi tu ndani ya Bunge la JMT, wengine kutoka ACT na wengine CCM . Mnashindwa nini kuudai huo mnaoita uhuru?

Ukweli mnaujua. Katika mfumo uliopo mnapendelewa sana. Kuanzia idadi ya wabunge ambao hauendani na population yenu. Na hao wabunge wenu wana haki ya kuzuia bajeti za wizara ambazo si za Muungano.

Wabunge wenu wana haki ya kuwa mawaziri wa wizara ambazo si za Muungano. Mna haki ya kugombea nafasi yeyote ya kisiasa Tanganyika ingawa ni mzanzibari. Una haki ya uteuzi katika taasisi yeyote hata kama haina shughuli Zanzibar. Una haki ya kumiliki ardhi. Una haki ya kufanya biashara yeyote. Una haki ya kupata elimu Tanganyika hadi Chuo Kikuu.

Una haki ya kuuguzwa katika hospitali yeyote iliyopo bara bila bhughudha yeyote. Una haki ya kupiga kura katika uchaguzi wowote unaofanyika. Yote haya Mtanganyika hana haki nayo akiwa Zanzibar. Lakini ni nyie ndio hamuishi kulalamika. Mnasema hatuwapendi wakati nyie ndio mnaonyesha upendo wenu kwa kutuita machogo.

Kama kweli mnahisi mnaonewa, ondokeni tu. Tutasikitika kwa sababu ya mazaoea lakini maisha yataendelea.

Amandla...
 
Katika kipindi hiki ambacho tunaongoza huku Zanzibar na kule Bara ni wakati wa kuhakikisha kuwa tunajitahidi kuirudisha nchi yetu mikononi mwetu.

Tumekuwa chini ya Utawala wa Tanganyika kwa miaka mingi sana tukilazimishwa kuunganishwa kwa lazima. Binafsi sijawahi ona faida ya huu Muungano Uchwara zaidi ya Tanganyika kutunyonya na kufaidika nasi...
Mkuu acha ubinafsi na hadithi za kale.
Leo Duniani kote nchi zinahitaji kwenda kwa pamoja kukuza chumi zao, wewe unalilia kujitenga? Kweli kabisa?

Ungelisema ni wakati wa Zanzibar kujitangaza kimataifa kama mojawapo ya nchi yenye uvumilivu,umoja ,amani iliyodumu kwa miaka mingi uku Tanganyika akiwa ni sehemu ya utamaduni, ulinzi, nishati na ustawi wake.

Haitowezekana kujitenga,kutengwa au kujivika ukuu wa kujitenga. Nina imani na Mh. Rais wa Tanzania kamwe hatoweza kuruhusu fikra za namna hiyo.

Ndio maana ya "Nchi Moja ya "Jamhuri ya Muungano"
 
Toa sababu za wewe kutaka Muungano huu uendelee .
Kwa upande wangu nasema Muungano huu sio ule uliokubalika na umepoteza vigezo vingi na zaidi unatumiwa na kufaidisha chama kimoja tu na uwepo wake si kwa manufaa ya wananchi wa pande mbili za Muungano bali ni kwa sehemu ya kundi moja tu ndani ya CCM,yaani hata ndani ya CCM kuna kundi halitaki kwa sababu si wote wanaofaidika.

Zaidi watu hupoteza maisha kila unapokaribia uchaguzi mkuu sababu ni zilezile za lile kundi liwepo madarakani ufupi WaZanzibari wananyimwa haki yao ya kuchagua kiongozi au chama wananchokitaka, hili ni jambo moja ambalo limewafanya waZanzibari kuona wananyanyaswa na kunyimwa uhuru na hata utamaduni wao unaangamizwa kwa kasi kubwa mabaa wadangaji kutoka Tanganyika wamejaa .na ziko sababu za kisiasa kiuongozi kimaslahi ambazo zimetekwa na serikali ya Tanganyika iliyojificha chini ya kivuli cha inayojiita ya Muungano ambayo inamilikiwa na Chama cha CCM. Hujiulizi ni kwa nini CCM peke yao ndio wanaong'ang'ani Muungano ?

Vyama vingine vyote vinautathmini Muungano umuhimu wa kuwepo au kutokuwepo kwa CCM hilo halipo.
 
Mimi ni Mtanganyika ila muungano siupendi hata kidogo maana una kero nyingi sana ZANEXIT inahusika.
 
Hawa watu wa Zanzibar wana msimamo mkali sana si wadogo si wa kubwa utakaekutana nae mkizungumzia Muungano atakushinda tu.na sasa wanasema wanamchukua mwananchi wao ambae ni raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) ,tuone mtafanya nini,wazenji wananjaa lakini bado wana jeuri.
Na siku hizi wamekaa kimya kabisa kama hawapo. wanaweza kuuvunja Muungano kimya kimya,maana wanayaweza.
 
Hawa watu wa Zanzibar wana msimamo mkali sana si wadogo si wa kubwa utakaekutana nae mkizungumzia Muungano atakushinda tu.na sasa wanasema wanamchukua mwananchi wao ambae ni raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) ,tuone mtafanya nini,wazenji wananjaa lakini bado wana jeuri.
Na siku hizi wamekaa kimya kabisa kama hawapo. wanaweza kuuvunja Muungano kimya kimya,maana wanayaweza.
Wana chaguliwa Raisi kila mwaka arafu unasema wana jeuri, jeuri gani hiyo mtu anakutawala arafu anakuchangulia raisi kila awamu.
 
Naunga Mkono hoja.
Binafsi sijawahi ona faida ya Muungano na sijui kwanini sisi watanganyika twajipendekeza mno kwa wazanzibari.

Kwavile rais wa JMT ni Mzanzibari basi hii ni bahati ya pekee Kwao kuuvunja Muungano.

KILA LAKHERI WAZANZIBARI !!
 
Tuanzie hapa;
ZANZIBAR NI NCHI SIYO NCHI?
Unapojibu rejea Waziri mkuu mstaafu Pinda.
 
Kiukweli Zanzibar ni nchi kamili.

Wana Rais wao, Wana Katiba yao mpya, wana Jeshi (JKU), Pia wana Bunge

Jambo kubwa zaidi kwenye maoni ya katiba ya Jaji Warioba, zaidi ya asilimia 90 ya waliotoa maoni kuhusu Muungano walishasema Hawautaki. Hivyo kuna haja ya kuangalia namna mpya ya kuuboresha huu Muungano. Usiwe wa viongozi tu uwe na baraka za wananchi wengi.
 
Hawa watu wa Zanzibar wana msimamo mkali sana si wadogo si wa kubwa utakaekutana nae mkizungumzia Muungano atakushinda tu.na sasa wanasema wanamchukua mwananchi wao ambae ni raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) ,tuone mtafanya nini,wazenji wananjaa lakini bado wana jeuri.
Na siku hizi wamekaa kimya kabisa kama hawapo. wanaweza kuuvunja Muungano kimya kimya,maana wanayaweza.
Tunataka Muungano kama wa (UAE ) Other wise bora ujunjike .UAE ni nchi 7 na kila mmoja ana maendeleo yake bila ya kuingiliana akitaka kufanya maendeleo ya nchi yake hamshauri mwenzake .Tanganyika mungeungana na kenya au uganda ndio size yenu.Tuacheni tupumue amini watanganyika kila lenye mwanzo lina mwisho.
 
Back
Top Bottom