Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

*Kwa kadri siku zinavyokwenda muungano wa Tanzania umeendelea kuwa ni mzigo mzito sana kwa nchi yetu sababu kuu ikielezwa kuwa pia ni muundo wa muungano uliopo sasa wa serikali mbili umekuwa ni kiini ama kichocheo cha kudumaza muungano wetu.

*Wazanzibar walio wengi wanaufahamu muungano wetu kwa kina zaidi na wao wako tayari hata sasa muungano huu uvunjike kama muundo wake hautarekebishwa lakini kikwazo kikuu kimekuwa ni Tanzania bara(Tanganyika)

*Swali kuu la kujiuliza ni faida gani ambazo Tanzania bara(Tanganyika) inaipata kutokana na muundo wa sasa wa muungano?
 
Hakuna faida yoyote kwa Watu wa Tanganyika, mie nadhani Muungano huu una faida zaidi kwa ccm na utawala ulioko madarakani kwani siku zote ndio wana utetea hadi kujaza mate midomoni. ila kwa uzoefu wangu sijawahi kuona Mwanachi wa kawaida akiutetea Muungano huu.
 
Wazanzibari wanafaidi zaidi kuliko wabara, angalia hatawakitangaza nafasi za kazi lazima waweke sharti kuwa muombaji awe mzanzibari ilihali bara hatuweki sharti kama hilo.
 
Zanzibar wanafaidika katika Ulinzi, na ndomana wazanzibar wengi hawataki uvunjike kabisa juu ya Ulinzi Nchi hii ni ya Kimapinduzi so Nje Ya Muungano Ni Rahisi Kuwa Na Mapinduzi Ya Mara Kwa Mara Sababu Aliyepinduliwa 64 atajipanga na kupindua kisha naye Aliyepinduliwa atajipanga atapindua na kama unavyojua hapa zanzibar kumegawanyika makundi ya wapemba na waunguja ni rahisi kwa mapinduzi, hii ndomana hata zinapotokea vurugu wakija askari utaskia hawa hawana masikhara wabara hawa, znz n ndogo na ivyo n rahisi kuwatambua askari na kwenda kuwafanyia jambo baya kwenye muungano hii imesaidia sana.

Free Movemnt Hii Ni faida ya Muungano sina haja ya Visa Kuja Tanganyika wala siulizwi unaenda kufanya nn na unafikia wapi, na hata nikifa huko nafanya chochote ntakacho kufanya biashara bila kufata taratbu anazofata asiye Raia wa TZ

Muungano Umetanua wigo wa Biashara wabara wanafanya huku na waznz nao pia

Muungano umeongeza Pato la Taifa juu ya ukusanywaji wa Kodi Za Serikali ya Muungano Na Znz

mengne baadae ati
 
Wakati Watanzania wanajiandaa kuipeleka mbele rasimu ya Katiba Mpya kwenye mabaraza ya Katiba ningependa sana kufahamishwa faida na hasara za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa upande wa Tanganyika.

...tafadhali usiingize faida na hasara za Muungano kwa upande wa Zanzibar.
 
Katika kuelekea miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar kuna mengi tunayasikia hasa ya kuvunja muungano na ikionekana kuwa Zanzibar wananyonywa kuliko wabara aka Watanganyika.

Na mara zote watanganyika hawajawahi kulalamika kama wananyo lalamika Wazanzibari juu ya Muungano.

Sasa napenda kama raifa tufanye mjadala wa wazi faida na hasara ya muungano huu na nani anafaidika zaidi ya mwenzake na nini kifanyike kuwe na usawa?
 
........... nini kifanyike kuwe na usawa?
.
Hakuna sababu za msingi za kuwepo muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Kama zilikuwapo (I doubt that) basi ni miaka hio ya 60's, hivyo kizazi kipya hakiefahamu tena kwanini kinapoteza muda kujadili na kurekebisha muungano usio na maana.

Ukizingatia kuna Afrika Mashariki, kama ni mashirikiano yatafanyika kwa kupitia shirikisho hilo ambalo kila nchi huingia kwa hiari.Naamini huenda Zanzibar kama itakuwa huru itauliza wananchi kwa kura ya maoni kama wanahitaji kuwemo ndani ya shierikisho hilo la EAC.Binafsi pia huenda nikapiga kura ya HAPANA!
 
Ndugu zanguni.

Nawaomba niwaulize tu, si kwa shari bali heri.

Hivi huu muungano wa tembo na sisimizi una manufaa kwa nani?

Watanganyika tunautaka wa nini?

Wazanzibari tunajua hawautaki , sasa tatizo ni nini?

Inakuwaje sisimizi ale mlo sawa na Tembo?

Kwa nini kila mtu asichukue taim yake kero ziishe?

Tuna mapori mengi, milima mingi, ardhi kubwa mara alfu kumi ya zanzibar lakini bado tunapoteza muda kuubembeleza huu muungano?

Leo hii mtanganyika haruhusiwi kununua ardhi Zanzibar lakini ruksa mzanzibari kununua tanganyika

Leo hii umeme Tanganyika tunalipa mara dufu ya Zanzibar

Leo hii mimi kama Mtanganyika siwezi tembea kwa amani na uhuru huko visiwani wakati wao wanatembea matumbo mbele huku wakibeua kwetu na kutupigia kelel juu kuwa hawatutaki.

LIWALO NA LIWE

HUU MUUNGANO WA TEMBO NA SISIMIZI UFE.

MUNGU IBARIKI TANGANYIKA.
tz-tng61.gif
 
ulishawahi kujiuliza hivi ktk mwili na ukubwa wake huo, nyusi zinakazi gani???
 
Tumekaririshwa shuleni.1 ulinzi na usalama wa tz.2.undugu wakuona na mengine mengi.pia ni mtaji wa ccm.
 
Chris Lukosi you are right hawa jamaa zetu wamemwaga sana damu hadi wengine kupata kilema,wamefungua kesi nyingi sana,hadi wakaanzisha uasi kama wa UAMSHO kwa ajili ya kuudai Zanzibar taifa huru(wajitoe kwenye muungano) ,this time sio busara tuwaachie tusiwabane mbavu kwa ajili ya masilahi ya baadhi yao wachache(wanzanzibar waroho wa madaraka)
 
Last edited by a moderator:
aisee katika makosa yote, watanganyika tusifanye kosa la kuwaachia hawa wazanzibar, kitakuwa kituo kikuu cha magaidi!.
 
Kaka mbona kama unataka kuongeza sikukuu za nchi..?kutakua sikuu hapo..siku ya muungano na sikukuu ingine itazaliwa siku ya mvunjiko hafu zote tutazienzi we si unatujua wabongo hatupendi kazi kiasi gani...mi naombea iwe mwezi wa 6..daaah mwezi gan hauna sikukuu zaid ya j2 tu..
 
Mkuu, mambo ya katiba na muungano sio ya CCM wala Chadema
Mimi naongelea utanganyika wangu, kama vile tulivyozoea kuwasikia wazanzibari wakiongelea uzanzibari wao bila kuogopa wala kuficha.

Nasema hivyo coz huko uliko hawataki kusikia kitu kama hicho, ni kama unapingana na chama chako. Na siku zote uungwana kama upo kwanye kundi ambalo unadhani haliendani na unacho amini ni vizuri ni vizuri ukajiuzuru basi
 
Back
Top Bottom