Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Wabara kupata ajira kwenye mahoteli visiwani sio faida? Vipi kupata nafasi kusoma chuo kikuu Zbar? Vifaa used vya kielektroniki vinapatikana kwa bei chee Zbar.
Mbona walioko Kagera wanafanya biashara na waganda tena kubwa kuliko ya huko kwa akina Mamidebwedo. Hata aliyeko Mtwara anafanya biashara vizuri na Msumbiji na ajira kule zipo pia undugu wa damu kabisa kuliko huu wa kulazimisha. Ukienda Mbeya ndo usiseme ni wana ndugu pande zote na biashara ukienda Kasumulu na Tunduma mambo mswano bila kuhitaji hata boti.
 
Maoni yalishatolewa kama hukutoa umechelewa maana sio muda wake sasa bunge liniafanya kazi yake iwe ya hovyo au ya kweli litafanya kaziz yake; mhimu nachukulia kama maoni yako tena ya mtu aliyechelewa so useless labda kama kutakuwa na katiba mpya ingine kama hii ikishindikana kwa jinsi inavyoonekana

Laiti ungelijua kuna kura ya maoni....
 
sitaki wawauwe wakristo na sijasema hivyo bali elewa kuwa nchi ya z ilishauzwa siku nying hivyo wale hawana chao kabisa

hao waznz ndio hawataki muungano. unataka waendelee kuuwa wakristo huko viziwani? na viongozi wa uamsho kuwatukana watanganyika?
 
labda sababu wengi hatujazaliwa kabla ya muungano na tanganyika tunaisoma kwenye vitabu tu....
Wale wajuvi wa historia naomba mtueleze ni nini tanganyika ilipungukiwa kabla ya muungano na nini kiliongezeka cha faida baada ya muungano!!!
Tumesomasoma juu juu kuwa moja ya sababu ni usalama kutoka pande hii ya bahari ila kwa technolojia ya sasa sioni hilo tishiO....
Tukasomasoma zaidi tukaambiwa ni mambo ya vita baridi katika kuizima cuba ya afrika.....

Je ni nini faida ya muungano kwa tanganyika???
Kule naona wanapata vingi vya chee tu, je huku??

Au ndio kizuri kula na mwenzio....
 
Ungekuwa precisely kwa ku re-phrase swali lako liwe. Nini Faida ya muungano wa SERIKALI 2 kwa Tanganyika? Because miungano ipo ya aina nyingi kama ule uliofanya USA, UK, USSR (Enzi hizo) China (Hong Kong &Taiwan), Germany (west & East)
 
Unaweza kulinda mipaka ya Bahari ya Tanzania Bara bila kuwepo kwenye hivyo visiwa?
 
Chanzo cha muungano hakikuwa ushirikiano wa kiuchumi, kijamii wala wa kisiasa wakati nchi hizi zikipata uhuru kwa Tanganyika na mapinduzi kwa Zanzibar. Hazikuwa na mtawala mmoja.

Sababu kubwa ya muungano ilikuwa ni ya kiusalama na ilikusudiwa kuinufaisha zaidi Zanzibar kuliko Tanganyika. Mapinduzi ya 1963 yalikuwa na wasiwasi wa kudumu kutokana na nguvu ya Sultan. Kutokana na falsafa ya Nyerere kutaka Afrika kuwa huru, Nyerere alihakikisha anaifanya Zanzibar kuwa sehemu ya Tanzania ili kujibu mapinduzi ya Sultani ambayo yangeweza kutokea. Tabia ya kupenda uhuru kwa Afrika iliifanya Tanzania kushiriki katika vita Msumbiji, Zimbabwe na Namibia.

Hakukuwa na tishio la Sultan kwa Tanganyika hivo Muungano haukulenga kuletea manufaa kwa Tanganyika bali Zanzibar. Wazanzibari sasa wana uwezo wa kujilinda wenyewe na ndio maana hawaoni tena faida za muungano ambazo hazihusiani na usalama. Kwa ukweli ni kuwa muungano kwa jinsi ulivoongezeka umri uligeuka kuwa shida kwa uchumi wao!!
 
NewOrder,

Nimekuelewa fika mkuu..kuwa sababu ni usalama wa zanzibar tu hamna kingine...
Kwa sasa kwa nini twaung'ang'ania??
1. Je tutaonekana tumeshindwa katika kuiunga Afrika??
2. Je ni kuwa hamna kiongozi anayetaka kuwekwa katika historia kwa muungano huu kuvunjikia mkononi mwake???
3. Kama hauna faida kiuchumi, kisiasa, kiusalama kwa tanganyika kwa nini twautaka tu!!!
 
Ungekuwa precisely kwa ku re-phrase swali lako liwe. Nini Faida ya muungano wa SERIKALI 2 kwa Tanganyika? Because miungano ipo ya aina nyingi kama ule uliofanya USA, UK, USSR (Enzi hizo) China (Hong Kong &Taiwan), Germany (west & East)

Hapana mkuu huko ni kufichaficha tu swali!!! Me nataka kujua faida ya muungano kwa tanganyika iwe serikali moja mbili tatu au hata tano zina faida gani kwa tanganyikA?
 
Hamna faida yoyote zaidi ya sababu zilizopitwa na wakati
 
Mkuu, maswali yako ni murua kabisa!!! Ndio maswali tunayotakiwa kujiuliza na kupata majawabu.

1. Waasisi wa mawazo mengi Afrika, Lumumba, Nyerere, Nkrumah nk walikuwa na maono ya uhuru na umoja. Na walifanya mengi kuleta umoja afrika. Kizazi cha viongozi kilichofuata kilikuwa ni utajiri, madaraka na ubinafsi. (kuvunjika kwa Sudan, mapinduzi ya kijeshi, vita vya wenyewe kwa wenyewe nk).

2. Ndicho kinachofanyika. Hakuna mtu anataka kuwa ndiye wa "kulaumiwa" na historia. Kila mtu anampitishia mwenzake. Mabadiliko ya kwanza yalikuwa ni 1984 kwa upande wa Zanzibar. Toka kipindi hicho kasi ya mabadiliko kwenye muungano ilishika kasi na kusiwe na hata mamlaka ya kuhoji. Hakuna aliyetaka kutoa maelezo, hata wale waliokuwa sahihi nao walinyamaza!! Nao pia hawakutaka kuwa historia, kila mtu alikuwa mwoga. Maoni ya Kamati ya SMZ imesema kwa Warioba kuwa wanataka dola kamili mbili lakini je umekwishasikia CCM kutoka Zanzibar wakisema hilo kwa mdomo?? Je umeelewa sasa kwanini hakuna makubaliano kwenye kamati za bunge ambako misimamo hasa ya CCM Zanzibar hatupati kuyasikia lakini changes kwenye rasimu zinashindwa kupitishwa kwa kukosa au theluth mbili upande wa Zanzibar au na Tanzania Bara pia?? The truth is nobody wants to take responsibility. Hata Kinana anasema "tujilaumu wenyewe kwa katiba ya Zanzibar 2010". Kwani CCM au JMT hawakujua na kuona katiba hiyo mpya kabla haijapitishwa?? We are reactive and not proactive!!

3. Nasema tena, hakuna faida za kiuchumi au kisiasa wala kiusalama kwa Tanganyika. Kama ni swala la usalama, Kenya has the longest porous border with Tanzania. Threat zingetoka zaidi huko kuliko Zanzibar. Kuna mwingiliano wa kijamii na Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, Kenya na Msumbiji kuliko uliopo na Zanzibar. Faida pekee ni ya kisiasa ambayo ilianza kwa kuunganisha TANU na ASP. So kwa CCM wanaogopa kuharibu historia yao ya kisiasa. Wanaogopa kupoteza ideologies zao na wanaogopa kupoteza madaraka na influence katika sehemu moja coz kwa mifano ya UNIP Zambia, KANU Kenya, inamaanisha kuwa inaweza kuwa ndio mwisho wa CCM kama chama baada ya muda mchache!! Kwa CCM, it is a survival battle and they will fight to the last drop of their blood. This fact is understandable!!! Toka Uchaguzi wa kwanza wa 1995, seats za CCM katika uwakilishi wa mawazo ya wananchi katika mabunge na serikali za mitaa zimekuwa zikipungua progressively. CCM has been notified and they want to put a halt to the downfall.
 
Kwa miaka mingi tangu kutikiswa kiberiti 1984 na mitikisiko iliyofuatia mpaka leo hii ya Rasimu ya Katiba, suala la Kero la Muungano linaongelewa.

Najiuliza hasa kero za Muungano ni zipi? Je wanaokereka wamefikisha wapi vilio vyao?

Je waliopokea vilio hivi, wamefanya nini mpaka leo hii ambapo ni miaka 30 tangu kiberiti cha kwanza kilipotikiswa?
 
Kwa miaka mingi tangu kutikiswa kiberiti 1984 na mitikisiko iliyofuatia mpaka leo hii ya Rasimu ya Katiba, suala la Kero la Muungano linaongelewa.

Najiuliza hasa kero za Muungano ni zipi? Je wanaokereka wamefikisha wapi vilio vyao?

Je waliopokea vilio hivi, wamefanya nini mpaka leo hii ambapo ni miaka 30 tangu kiberiti cha kwanza kilipotikiswa?
Kishoka , ni miaka zaidi ya 40. Zimeundwa tume na tume hakuna jibu.
Kero za muungano kwa tafsiri rahisi ni znz kusikilizwa wanataka nini. Hilo limefanya Watanganyika wajiulize, Tanganyika yao ipo wapi? Na kinachoendelea ni kuidai. Huwezi kuwa na znz huru halafu znz ndani ya muungano na hewa!
 
Kwa miaka mingi tangu kutikiswa kiberiti 1984 na mitikisiko iliyofuatia mpaka leo hii ya Rasimu ya Katiba, suala la Kero la Muungano linaongelewa.

Najiuliza hasa kero za Muungano ni zipi? Je wanaokereka wamefikisha wapi vilio vyao?

Je waliopokea vilio hivi, wamefanya nini mpaka leo hii ambapo ni miaka 30 tangu kiberiti cha kwanza kilipotikiswa?
Mkuu Rev Kishoka, hakuna kero za muungano!, kuna changamoto tuu zinazoukabili Muungano!.

Jaji Warioba alizitaja zote alipohutubia Bunge Maalum!.
Pasco
 
Back
Top Bottom