Muungano wa Tanzania uko katika hatua ya kwanza kuelekea kuvunjwa

Tuwe na serikali tatu na tuwe na nia ya kuwa na muungano sio kulaghaiana!

Very good words je katiba ya zanzibar wataifanyaje maana iko juu ya katiba ya muungano.

Alafu muungano asili yake ni watu wa maeneo yanayoungana mwanzoni hakukuwa na shida mpaka hivi karibuni lakini viongozi wa zanzibar walipotaka na wao wawe wanaenda umoja wa mataifa na kutembelea nchi mbalimbali dunian kama anavyofanya kikwete wakaanza kuwashawishi wazanzibar na wakashawishika.

maana ukiangalia kwa makini wazenji hawabughudhiwi hapa tanganyika wanafanya kila kitu wanavyotaka ila sio watanganyika zanzibar wanatunyanyasa na hii imekuja baada ya kuaminishwa na viongozi kwamba hao ndio waliotusababishia umaskini.Ebu Angalia wanapanga bajeti yao wenyewe hakuna anayewaingilia wana bunge lao hakuna anayewaingilia je umaskini wao sisi watanganyika tunausababishaje?

Yaani ikifika hapo utajua kwamba madai yao hayana mashiko kama kuna lingine ebu mtufumbue sisi watanganyika tunawasabishaje maskini wa wazenji?
 
Si nishakwambia kuwa lengo sasa ni kulinda maslahi ya wachache? Hawa ndio tatizo kiasi kuwa wanapinga wanayoyataka wananchi!
hawaezi kupambana na umma inagawa mfa maji haachi kutapatapa
 

Hapana ndugu yangu kama wewe ni mhehe utakuwa mhehe je alishashambuliwa mtu huku tanganyika eti ni mluguru au mchaga au mpemba ila ukienda zanzibar wao wako wazi hawatupendi mpaka wanasema mwislamu wa tanganyika si mwislamu kamili umeshaona comred hao wazenj wana mambo ya ajabu sana
 
huu muungo wa tanganyika. na zanzibar uvunjwe na kama kutakuwa na ulazima wa kuungana hapo baadae iitishwe kura ya maoni wananchi wa pande zote waulizwe kama wanataka kuungana au hawataki

siku hiyo itafika tu usijali
 

Dullyhami;
Hivi kweli unayoyasema yanatoka moyoni au akili yako tuu ulivyo uelewa huo Muungano na chokochoko zake? Mbona unawakingia kifua hao Wazenj kuwa sio wao walio anzisha chokochoko?
Wamejiandikia katiba yao ilokuwa imepotezwa na Muasisi wa huo Muungano, kama hilo halitoshi wakajitungia wimbo wa Taifa huru, ka hilo halitoshi wakajiundia majeshi yao na Mkuu wao wa Majeshi. Weye upo hapo? Ka hiyo haitoshi, wakasema, Twataka Dola yetu, Benki Kuu yetu na Sarafu yetu. Ni nchi moja tu duniani inatumia Fedha yake yenyewe ila ina value 2 tofauti. Tanzania. Umeona wapi, Fedha halali ya JMT na Fedha halali ya BMZ. Jamani, mambo mengine tuyaangalie. Haya yoote yanatendeka, Rais wa JMT yupo hai tena anasema yupo Ikulu ya JMT.
Kivumbi ni pale bunge lilipo mpindua Rais wa JMT na kumfanya sawa na rais wa BMZ. Ati, akitaka kufanya lolote, awasiliane na huyo wa BMZ. Na yule wa Tanganyika yupo wapi hapo???? Wazenj, kubalini msikubali, hakuna Muungano. Hata hiyo katiba mpya inayo andikwa, sijui Zanziba wanakaa na wanani. Kwa nini wajiandikie katiba mbili???? Kama haki ipo hiyo unayoisema, waanze kwanza kuiunda Tanganyika kwani Zanziba ipo, kwa nembo zao kuu walizojianzishia kama Taifa.
Hivyo Zanziba wamesha onesha wazi kuwa, Hawajajiunga na ushirika wowote ila wapo watu wanaojibalagaza kuwataka ushirika nao hao Wazenj hawawajui hao watu wanaojiita Tanzania Bara. Hilo ni Taifa gani? Tanzania Bara???!!! Ni wanani hao?
Nasema, Wajumbe wa hilo Bunge la katiba kama wana moyo mzuri na Taifa hili, waache kuendelea na hiyo Katiba. Ni kama Mama kwenda labour Ward na kulala huko akingojea mtoto kuzaliwa huku hamjui mume wala hana ujauzito. Ni maajab haya duniani. Wanajadili Katiba Mpya ya nchi gani?
Zanzibar waliuvunja muungano tangu 2010 walipoandika katiba yao.
 
maganjwa,

Kwani ukivunjika muungano Zanzibar haitaweza kufanya uhusiano na mataifa mengine au haitaweza kujinunulia chakula chake? Zanzibar kabla Muungano ilikuwa ni miongoni mwa nchi tajiri duniani. Kylikuwa na supermarkets za serikali vyakula vilikuwa rahisi tu. Kenyan products including vyakula kama sembe la packets na mafuta ya kupikia siagi, vitunguu na hata vitu vya na sanitary kama sabuni za kuogea na.dawa za meno zilitoka Kenya, UK, India na China.
Nakuona uko katika majanga ya ufaham mdogo wangu majangwa. Nahisi Tanganyika itapata tabu kiuchumi, maana kila upande majirani wanaangalia kwa jicho la waswasi, Kaskazini (Kenya & Uganda) Magharibi Ruwanda na Kusini Malawi. Hawa wote ndio wa kufanya zaidi biashara na Tanganyika. Zanzibar population ya watu milioni 1 wakiagiza tani alfu 20 za mchele kutoka India au Thailand inatosha chakula cha miaka miwili.
Vitunguu vya India ni rahisi sana na juu ya gharama za usafirishaji kuliko vya Iringa.

Zanzibar ikitangaza kuwa bandari huru inatosha kwani haya yalifanywa huko nyuma wakati waingereza nq wajerumani walipotaka kuikwamiza Zanzibae kiuchumi.

Kuna, vyombo vingi vya kushiriki zanzibar kujiendelza kiuchumi. Kuna kama Indian Ocean Rim, SADEC, OIC, ASEAN, etc.

Badili ya Kudai Tanganyika nayo ikawa na mamlaka yake ili iingiane mikataba ya haki na usawa katika muungano mnashika kuking'ang'ania kanchi kadogo kwa nguvu mkitawale. Kwa mantiki gani na nini hasa mnachokitafuta Zanzibar?

Hebu boresheni utawala katika majimbo ya Tanganyika hasa ya Kusini amabako Mungu amejaalia kuna rasilmali za kutosha kuinyanyua nchi badala ya juendesja siasa chafu za kikoloni.
Ritz, gombesugu, THE BIG SHOW, mfumo

Zanzibar
 
Last edited by a moderator:

Tanganyika haiwezi kulalamika kwavile imebadili jina na kujiita Tanzania. Ukiangalia kiundani utaona Tanganyika inaikoloni Zanzinzibar.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 

Da kijana umenifurahisha sana
 

kila la heri ni mawazo yako kwa taarifa yako hako hakuna anayingangania zanzibar mchakato wa kuvunja muungano sio kichwa cha mada hii na waliofanikisha ni watanganyika wewe furahi tu utakuwa huru.
 
Tunapoteza muda hapa wa bure zanzibar hawataki muungano tena herufi kubwa.
 
Tanganyika haiwezi kulalamika kwavile imebadili jina na kujiita Tanzania. Ukiangalia kiundani utaona Tanganyika inaikoloni Zanzinzibar.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk

Kwani shida ni nini? mnakosa nini kwa sababu kama identity ipo mnaitwa wazanzibar lakini sis tumepoteza identity yetu mbona hatulalamiki. kila kitu mnajifanyia mnatulalamikia kwa sabab gani? bajeti mnapanga wenyewe ya maendeleo yenu sis tumewafanyia nini baya mpaka tustahihili kulaumiwa?

mlikuwa mpigane wenyewe kwa wenyewe baada ya muungano tukawasaidia mpaka mnaongea kama jamhuri ya watu wa zanzibar hivi jamhuri mlikaa katika jamhuri miaka mingap? acheni uchokozi usio na maana
 
Yaap umekuja kenye point. na suala muhim sana ilikuwa kuuliza watu je tuwe na muungano au tusiwe na muungano. hilo swali ni uhaini na kitu cha kuhioji ni je muungano uwe wa aina gani? umeona?
Maganjwa ndugu yangu kuna mengi nyuma ya Pazia la falsafa ya Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar mm nahisi sio matakwa binafsi ya waasisi wetu wa muungano tu nahisi pia kulikuwa na shinikizo la Mataifa ya nje.
Ipo kauli inasemwa kuwa Jkn aliwahi kusema anaichukia znz kuwa jirani ya Tanganyika anatamani visiwa vya znz vingesogea mbele zaidi ili visipakane na Tanganyika.sasa vipi Mtu huyu alietamka maneno hayo halafu arudi aungane na nchi anayo ichukia? Hapa ndio napata shaka kama Jkn alipewa shinikizo na Mataifa ya nje la kuunganisha hizi nchi. Ukiangalia Ujio wa Jkn ktk TANU kutoka uwalimu na jinsi alivyo pata umaarufu na madraka haraka haraka napata shaka kama ni pandikizi la Muengereza mtawala mkolonoi wa Tanganyika. Na hilo ndilo lililo pelekea Muungano usio isha manuguniko. Kwakuwa haukuwa Muungano wa wananchi wala wa nchi ulikuwa ni muungano wa watu wawili kwa masharti na muungozo wa nchi za nje.
 

nimekuelewa mkuu, ila yote uliyosema ni masikitiko ya kuzimwa kwa zile ndoto za kuimeza Zanzibar ambazo Watanganyika walikuwa wakiota na sasa wanaona kama ni ndoto za Alinacha!! maana kwa ulimweng wa sasa huwezi kulazimisha matakwa nje ya yale wananchi wanataka! Kwa Wazanzibar wanaonekanwa wanataka Uhuru zaidi wa kufany mambo yao ili kuwezesha uchumi wao kwa maslahi ya watu wao, hilo halina kificho wala sio haramu, lakin Uhuru huo wataupataje? Ni lazima kuwe na Muungano utaosimamia misingi ya hakki na usawa! hiyo ndio hoja kuu, sio issue ya Zanzibar kubadili katiba yao, Wazanzibar wana Uhuru wao wa kuifanyia watakavyo katiba yao maana ile ni Mali yao, sasa kama tuna uchu na Muungano huu tuifufue Tanganyika kisha tuone mambo yatavyoenda! Zanzibar ina wenyewe, Tujadili Tanganyika yet!
 
wlikuja wakongo kununuwa ijekuwa watu pori watanganyika let au goooo
 
Hicho chakula munatugaiya bure ? Mbona hoja za kitoto ? Nyie wenyewe munakufa na njaa
 
Hicho chakula munatugaiya bure ? Mbona hoja za kitoto ? Nyie wenyewe munakufa na njaa

kwanini mmevunja muungano na kujitungia katiba ndani ya muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…