Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Kwakweli kiasi wanachopekea wenzetu wa Zanzibar ni kikubwa sana hakina uhalisia hata kama ni nchi ila idadi yao ni ndogo kiasi kwamba uwezo wa kurejesha hizo fedha ni mdogo sana.
 
Ulitaka kero za Muungano zichukue mda gani kutatuliwa?

Kwa nini Marais wa Bara walikuwa wanapuuza?
Mwinyi alikuwa wa bara?Kwanini hizo kero zimefanywa Siri namna zilivyotatuliwa?Usiri Huo una Nini ndani yake?

 
Naomba Mungu iendelee hivihivi ili 2025 akili zitukae vizuri! Bado 3 good years
 
Labda waendelee kupora kura, vinginevyo ili kuondokana na hali hii lazima kubadili chama cha kuongoza!
 
Mwinyi alikuwa wa bara?Kwanini hizo kero zimefanywa Siri namna zilivyotatuliwa?Usiri Huo una Nini ndani yake?

Wewe kabla ya kusema zimefanywa Siri ulikuwa unazifahamu?

Kwani Mwinyi ana asili ya Zanzibar au Bara?

Muulize PM na VP akupatie kero zilizotatuliwa sio kuhemka kwa nyege.
 
Nikiona mtu anaingiza matusi kwenye ujengaji wa hoja huwa namweka kapuni!Asubuhi njema!
Jibu hoja acha kuhemka kwa nyege

2738144_JamiiForums764709745.jpg
 
Tumeizulumu sana Zanzibar kwa miongo ming wakati we're equal partners kwenye Muungano 50/50.
 
Hivi karibuni, kuna taarifa zilizowekwa wazi kwenye baadi ya vyombo vya habari, juu ya mgawanyo wa mikopo ya nje, kati ya Tanzania bara na Zanzibar.

Mkopo wa pesa ya Uviko 19, tunaambiwa Zanzibar ilipata 21%. Mkopo wa kutoka Japan, tunaambiwa Zanzibar imepata 30%.
Kama ni hivyo basi zanziba itawajibika kulipa ili deni kisheria isipokuwa hiyo asilimia 4.5 tu ndiyo italipwa na muungano hivyo mama anaitia zanziba kwenye deni kubwa
 
Kiukweli hivi sasa zanzibar inajengeka asee tuache utani, mfano dr. Mwinyi ameamua waunguja wawe wafanyabiashara na anajenga masoko matatu makubwa yote kwa mkupuo tena yenye kiwango kama lile la Kisutu, magomeni au zaidi ya hayo.

Kuna soko linajengwa Mwanakwelekwe, Kwa nyanya na lingine Jumbi njia ya kwenda tunguu, ukiachilia mbali yale maduka pale darajani ukiangalia ujenzi huu wa mkupuo unaweza usielewe ila kwa ndani unawaza je, fedha za miradi hii inatoka wapi?.

Unaweza sema kuna bandari na ile peaa ya mrahaba wa wawekezaji wa mahoteli ila, kiukweli ile pesa ni tone tu katika maendeleo yoyote ya nchi inayoamua kujenga na kuwekeza miradi mikubwa kwa mara moja.

Pesa za uviko 19 je?.
 
Tumeizulumu sana Zanzibar kwa miongo ming wakati we're equal partners kwenye Muungano 50/50.
Ni bora tutengane tu,kwenye masuala ya ulinzi kama itakuwa lazima basi ndio tuwe na makubaliano!
50/50 wakati mdanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar na mzanzibar anaweza kumiliki ardhi Bara!
 
Ni bora tutengane tu,kwenye masuala ya ulinzi kama itakuwa lazima basi ndio tuwe na makubaliano!
50/50 wakati mdanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar na mzanzibar anaweza kumiliki ardhi Bara!
Kutengana kutalisaidia Taifa la Tanganyika lililofutwa na Wanasiasa wenye uchu wa Madaraka kurejea tena na Zanzibar kurejesha kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa.
 
Waziri na katibu mkuu unawaonea tu hawana ubavu wa kupitisha mambo makubwa hivyo bila amri kutoka juu
 
Kero za Muungano zimetatuliwa ndani ya miezi michache tangu SSH aingie madarakani!🤣🤣
Tumepigwaaaaaa!
Mabadiliko yote ya muungano yanatakiwa yapitishwe na theluthi mbili ya baraza la wawakilishi na theluthi mbili ya bunge la muungano
 
Mabadiliko yote ya muungano yanatakiwa yapitishwe na theluthi mbili ya baraza la wawakilishi na theluthi mbili ya bunge la muungano
Mkuu hizo ni kero na sio mabadiliko ya Muungano!Mabadiliko ya Muungano ni kama muundo wa serikali NK!Lakini mgawo na vitu vingine vidogo vidogo ni makubaliano tu!

 
Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, umeweka wazi kanuni ya mgawanyo wa mikopo na misaada kutoka nje, ambapo Zanzibar inastahili kupewa 4.5%.
Hakuna mkataba wa muungano uliozungumzia mgawanyo wa mapato ya nje. Swala la 4.5% lilikuja baada ya kuvunjika EAC mwaka 1977. Wakati wa kugawana mapato likaja swali sisi Tanzania tutagawanaje mapato baina ya Tanganyika na Zanzibar? Kumbuka Zanzibar ilikuwa imejiunga na EAC kama nchi kamili wakati wa kuanzishwa kwake. Ndipo akatafutwa mshauri elekezi kushauri mgawanyo. Huyo mshauri ndiye alipendekeza hiyo 4.5 na JMT ikakubali ushauri huo. Hivi ndivyo ilivyokuwa. Utaratibu huu, kwa bahati mbaya, ndio uliendelea kutumika hata kwenye misaada na hata hivyo mara zote Zanzibar ilikuwa ama haipati chochote au inapata chini ya 4.5
 
Back
Top Bottom