Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Pamoja na haki zote hata ingekuepo ni nchi huru haingeweza kupewa hela nyingi kiasi hicho kwasababu pesa hutolewa kulingana na GDP ya mkoa husika. Kwahiyo Znz isingeweza kupewa kiasi chote hicho cha pesa kwasababu haina uwezo wa kuzilipa
Mlaumu aliyekujaza huu ujinga
 
Mgao wa zanzibar unatakiwa kuwa proportionate na mikoa mingine ya Tanzania, kimsingi ukubwa na idadi ya watu ya zanzibar ni sawa na mikoa mingine iliyopo Tanganyika. Sasa chukulia bil. 700 uigawe kwenye mikoa 20 ya Tanganyika utapata wastani wa bil. 35 kwa kila mkoa. Halafu linganisha na bil. 242 iliyopewa zanzibar hapo ndo utagundua namna Tanganyika inavyotumika kuipaisha zenj..........
 
Kichekesho nyinyi watu wa maajabu sana. kitu usichokijuwa ni bora kufanya uchunguzi ili kuwa na uhakika na unachokisema. Mmeimbishwa uongo na nyinyi mmekuwa mkiurudia mpaka mnauamini kuwa ni ukweli. Zanzibar ardhi yote ni ya Serikali. Mzanzibari anapatiwa hati ya matumizi ya ardhi ya kulima, kujenga na shughuli za uzalishaji wa kawaida. Uwekezaji mkubwa inabidi aombe kukodishwa ardhi ambayo atalipa kodi kila mwaka Serikalini. Hivyo hivyo kwa mgeni anaekuja kuwekeza nakodishwa ardhi kwa malipo kwa muda aliokubaliwa kwa kujibu wa sheria zilizopo. Halafu mnajiwa kuwa Mtanzania yoyete anaweza kuwa Mzanzibar akiamua kufanya hivyo? anachotakiwa aishi Zanzibar miaka 5 na kuomba ndio maana Mhe. Ali Hassan Mwinyi amekuwa Mzanizbari na Rais wa Zanzibar. Kwa hiyo kama hoja ni ardhi nenda kaishi Zanzibar ili upate hiyo ardhi inayokutoa roho.
Hata Tanzania umiliki wa ardhi ni Kwa miaka 99!Ardhi inabaki kuwa chini ya umiliki wa Rais Kwa muda Huo!Sasa jiulize,Je, mzanzibar akija bara masharti ni hayo hayo?Au hujui wewe ukiwa mdanganyika Kwa Zanzibar unahesabika kama mgeni yeyote kutoka ughaibuni?Unajua huwezi kuajiriwa au kugombea Zanzibar kama si mzanzibar?Njoo Bara,wazanzibar wangapi Wana majimbo na Wana nafasi kwenye sekta hata zisizo za Muungano?Tafakari!
 
Ramani gani hiyo inaonyesha Tanganyika ndiyo Tanzania? Au ni wapi Tanganyika inatambulika kama Tanzania? Tanganyika siioni kwenye ramani popote pale.
Nini huwa kinatangulia! Inatangulia ramani au kilichowekwa kwenye ramani?

Tafuta articles of union uzisome, utaipata sehemu inayosema:

Nchi hizi mbili, Tanganyika na Zanzibar, zimeungana kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Zanzibar yatasimamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mambo yote yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika, yatasimamiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Usijifunge akili kwenye mambo madogo kama ramani. Tanganyika ipo, na ndiyo inayoibeba JMT. Ndiyo maana kuna mahakama kuu ya Tanganyika, kuna chama cha Wanasheria wa Tanganyika.
 
Hivi karibuni, kuna taarifa zilizowekwa wazi kwenye baadi ya vyombo vya habari, juu ya mgawanyo wa mikopo ya nje, kati ya Tanzania bara na Zanzibar.

Mkopo wa pesa ya Uviko 19, tunaambiwa Zanzibar ilipata 21%. Mkopo wa kutoka Japan, tunaambiwa Zanzibar imepata 30%.

Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, umeweka wazi kanuni ya mgawanyo wa mikopo na misaada kutoka nje, ambapo Zanzibar inastahili kupewa 4.5%.

Kama ni kweli Zanzibar ilipata 21% badala ya 4.5%, na pia ilipata 30% badala ya 4.5%, waliohusika wote, wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Katibu Mkuu Wizara ya fedha, walistahili wasimamishwe mara moja, na kama tungekuwa na Bunge, lilistahili kuunda kamati kuchunguza ukweli wa jambo hili, na kuchunguza uhusika wa Rais katika ukiukaji huu wa kanuni za Muungano.

Jambo la kujiuliza:

1) kwa hali hii ya sasa, ambapo nchi haina bunge linalowakilisha wananchi, nani ataihoji serikali?

2) kama trend itaendelea hivi, mpaka kufikia 2025, hali itakuwaje?

3) kama hiki ndicho kinachoendelea, hatuoni kuna njama za kuitumia Tanganyika kuijenga Zanzibar, na kuifanya Tanganyika kuwa 'kubwa jinga?'

4) Hali ikiendelea hivi, na bunge hatuna, nani ataweza kuhoji juu ya jambo hili?

5) Je, hatuoni kuwa kama hali hii ni kweli, mikopo hii inailenga Zanzibar, na Tanzania bara inatumika tu kama daraja, huku kisheria deni likiwa la kwake?

6) Japo hatuombei, kama kukiwa na njama ambazo zikafanya siku moja Muungano ufe, hatuoni hasara itakayokuwepo kwa Tanzania bara kwa sababu madeni haya yote mkopaji ni yeye, na hivyo ndiye atakayewajibika kulipa?
Mkuu, inaumiza kuona hamna mbunge hata mmoja akihoji mambo kama haya. WOTE ni WAOGA tu. Tunaambiwa wakati wa chama kimoja chini ya Mwalimu Nyerere bunge lilikuwa MOTO likilojaa SAUTI za kuhoji mambo bungeni. Na Nyerere nasikia alipenda sana. Mijadala yenye tija. Leo vyama ni vingi na CCM ndo wengi kwani hamna hata mbunge JASIRI wa kuuliza mambo kama haya? Kama jibu ni HAYUPO basi nchi yetu iko kwenye hatari ya FREE FALL!!!!
 
Kichekesho nyinyi watu wa maajabu sana. kitu usichokijuwa ni bora kufanya uchunguzi ili kuwa na uhakika na unachokisema. Mmeimbishwa uongo na nyinyi mmekuwa mkiurudia mpaka mnauamini kuwa ni ukweli. Zanzibar ardhi yote ni ya Serikali. Mzanzibari anapatiwa hati ya matumizi ya ardhi ya kulima, kujenga na shughuli za uzalishaji wa kawaida. Uwekezaji mkubwa inabidi aombe kukodishwa ardhi ambayo atalipa kodi kila mwaka Serikalini. Hivyo hivyo kwa mgeni anaekuja kuwekeza nakodishwa ardhi kwa malipo kwa muda aliokubaliwa kwa kujibu wa sheria zilizopo. Halafu mnajiwa kuwa Mtanzania yoyete anaweza kuwa Mzanzibar akiamua kufanya hivyo? anachotakiwa aishi Zanzibar miaka 5 na kuomba ndio maana Mhe. Ali Hassan Mwinyi amekuwa Mzanizbari na Rais wa Zanzibar. Kwa hiyo kama hoja ni ardhi nenda kaishi Zanzibar ili upate hiyo ardhi inayokutoa roho.
Nadhani amejibu bila kuelewa mantiki ya hoja. Hoja ni kuwa Mtanganyika akiwa Zanzibar kwenye masuala ya Ajira, kumiliki ardhi na nafasi za kisiasa anatambulika kama mgeni kutoka Kenya, Uganda, Somali, China, Usa, nk. Lakini mzanzibar anapokuja bara kwenye masuala hayo hayo ya Ajira, kumiliki ardhi na fursa za kisiasa anatambulika kama mwenyeji kutoka Kigoma, Dar, Iringa, Arusha nk. Kwanini hili jambo liwe hivyo wakati tuna muungano? Kwanini kuna double standard?

Suluhisho ni nini?
KATIBA MPYA.
 
Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, umeweka wazi kanuni ya mgawanyo wa mikopo na misaada kutoka nje, ambapo Zanzibar inastahili kupewa 4.5%.
Topic yako ina mislead the public, 4.5 inazungumzia misaada sio mikopo. Chanzo cha mkataba kikowapi ?
On top of that wazanzibari hawana haja na muungano kama unavyofikiria kuwa wanafaidika.
 
  • Thanks
Reactions: lum
Topic yako ina mislead the public, 4.5 inazungumzia misaada sio mikopo. Chanzo cha mkataba kikowapi ?
On top of that wazanzibari hawana haja na muungano kama unavyofikiria kuwa wanafaidika.
Ni kweli wazanzibar hatuuhitaji huu muungano, maana unazika uhuru wetu kama taifa huru la Zanzibar, lakini hoja iliyopo mbele yetu ni kuhusu hii misaada na mikopo ya sasa ambayo Zanzibar tunavuna kati ya 20-30%, Je inakidhi hitaji la kikatiba na kisheria au una uhalali wa kimantiki?
 
Serikali iseme nini wazi? Anaeweka hii mikopo wazi ni baba yako? Kama kuna shida si wangefanya kwa kificho? Mna matatizo kichwani nyie.
kwanini usimalizie ni Nani atalilipa Deni hilo?
Juzi tu Magufuli alikaa na Dr Sheni kufuta Deni la Tanesco, Zanzibar alilokataa kukulipa na alitumia halali.
Mnachotaka huyu Mama Muungano uvunjikie mikononi mwake, ni lazima mlipe madeni yote kwanza maana mnategemea Utalii km Tanganyika hakuna Utalii
 
Wewe Ni mpumbavu.

Unachojaribu kukipambania hukijui.

Unataka watanganyika waungane kupambania haki yao na wakati huo huo uko busy kuhubiri utengano na kujiona wewe ndio Bora na mpambanaji kuliko yeyote.

Sasa pambana na mpaka utakufa na hakuna kitu chochote utafanikiwa.

Zanzibar itaendelea kuchukua mpaka asilimia 100 na hakuna kitu utafanyaje.

Endelea kununua vibando uweke, yingie mitandaoni ubweeeeke, halafu ukalale uendelee na kupiga miayo mboweeee mboweeee mboweeee.
Hawanaga akili hawa watu,,, tangu lini kila mkopo ukitoka unagawanywa?,.. miaka yote nyuma mikopo mingi inatumika bara tu, sijawahi sikia tangu nizaliwe mwaka 1938,eti sijui japan imetoa hela halafu zikapelejea na zenj,,
Kiufupi watu wa bara tuna roho za ajabu sana,
Leo bilion 200 zimejenga daraja la tanzanite,, je kwenye mgao wa mkopo wa kujenga hilo daraja, zanzibar walipewa bei gani?, Vipi kuhusu daraja za kigongo ferry, zanzibar wamepewa hela ngapi?
Vipi kuhusu kigamboni bridge,, je watumishi wa zanzibar hawakatwi NSSF?
[emoji23]
 
Kama Zanzibar ni nchi, ilistahili kukopa yenyewe na siyo kutumia mgongo wa nchi nyingine.

Siyo ikope Tanganyika, hela iende Zanzibar, idaiwe Tanganyika.
Walikuwa hawaruhusiwi wao kukopa kama nchi , si kiti chao UN walikiachia...
 
kwanini usimalizie ni Nani atalilipa Deni hilo?
Juzi tu Magufuli alikaa na Dr Sheni kufuta Deni la Tanesco, Zanzibar alilokataa kukulipa na alitumia halali.
Mnachotaka huyu Mama Muungano uvunjikie mikononi mwake, ni lazima mlipe madeni yote kwanza maana mnategemea Utalii km Tanganyika hakuna Utalii
Kazi iendeleee
 
Tanganyika ndiyo Tanzania. Na hilo limekuwa sababu mojawapo ya malalamiko ya Wazanzibari kuwa Tanganyika imevaa koti la Muungano.

Kiuhalisia, Tanganyika ndiyo Tanzania lakini ndani ya hiyo inayoitwa Tanzania, imetoa sehemu ya mamlaka yake kwa Zanzibar, na yenyewe kuendelea kusimamia yale ya Tanganyika.

Kwa ujumla, hata kwa logic ndogo kabisa, huu Mwungano ni utata mtupu. Hata tukichelewesha vipi, kuna siku ama utavunjika au utaboreshwa ili kuleta mantiki.
Ha ha ha eti Tanganyika ndio Tanzania,,
Uko wrong jina TANZANIA liko na zanzibar ndani yake,,,, tukubali tu, tulibugi,,
Tunaweza kurudisha serikalini ziwe tatu,
Lakini sasa inabidi zanzibar ipate kiti UN na kiti cha bara ndio kiwe cha sasa huko
Then iwe shirikisho,,,
Zanzibar wawe na bank kuu yao,jeshi lao na balozi zao nje ,,,
Ni suala la kukubaliana tu, mi sioni shida hapo [emoji23][emoji23]
 
Hawanaga akili hawa watu,,, tangu lini kila mkopo ukitoka unagawanywa?,.. miaka yote nyuma mikopo mingi inatumika bara tu, sijawahi sikia tangu nizaliwe mwaka 1938,eti sijui japan imetoa hela halafu zikapelejea na zenj,,
Kiufupi watu wa bara tuna roho za ajabu sana,
Leo bilion 200 zimejenga daraja la tanzanite,, je kwenye mgao wa mkopo wa kujenga hilo daraja, zanzibar walipewa bei gani?, Vipi kuhusu daraja za kigongo ferry, zanzibar wamepewa hela ngapi?
Vipi kuhusu kigamboni bridge,, je watumishi wa zanzibar hawakatwi NSSF?
[emoji23]
Mbona unaakili za usiku..
Wabara wanahoji hizo hela Zanzibari atarudisha kama mugao aliopewa au ni Tanganyika.
Mpaka sasa deni lake ni mara kumi zaidi ya bajeti kama atahusika kuzirudisha kwa miezi michache tu.
 
Mgao wa zanzibar unatakiwa kuwa proportionate na mikoa mingine ya Tanzania, kimsingi ukubwa na idadi ya watu ya zanzibar ni sawa na mikoa mingine iliyopo Tanganyika. Sasa chukulia bil. 700 uigawe kwenye mikoa 20 ya Tanganyika utapata wastani wa bil. 35 kwa kila mkoa. Halafu linganisha na bil. 242 iliyopewa zanzibar hapo ndo utagundua namna Tanganyika inavyotumika kuipaisha zenj..........
Sio kila mkopo unaopatikana hugawanywa kila mkoa, hii imetokea awamu hii tu kwenye pesa za uviko
Mikopo huwa inakuja kufanya specific project in a particular place,
Mfano zinaweza toka pesa UNDP bilion 500 kuja kutengeza barabara njombe,, au kujenga mabwawa simiyu, au kuvuta maji ya lake viktoria Tabora,,
Sasa haina maana hizo hela zikitoka, eti zanzibar nao wadai mgao. Au mwanza nao walalamike kwanini hawajapata, au kwanini wamepata kidogo kuliko simiyu, wakati wao wako wengi.
Mikopo inakuja na kufanya kazi kwenye specific project in a particular places,
 
Aliye anzisha mungano Nyerere hayupo, nyie mnaunga'ang'ania kwanini?
 
Mbona unaakili za usiku..
Wabara wanahoji hizo hela Zanzibari atarudisha kama mugao aliopewa au ni Tanganyika.
Mpaka sasa deni lake ni mara kumi zaidi ya bajeti kama atahusika kuzirudisha kwa miezi michache tu.
Hebu eleza utaratibu wa kulipa deni la nje ukoje,, je huwa tunaguatwa mmoja mmoja kulipa au ni vipi, wanzanzibar hawalipi kodi?,
 
Back
Top Bottom