Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Hebu eleza utaratibu wa kulipa deni la nje ukoje,, je huwa tunaguatwa mmoja mmoja kulipa au ni vipi, wanzanzibar hawalipi kodi?,
Zanzibar walijitoa kuomba mkopo chini ya Tanzania wakiongozwa na Masoud VP wa Zanzibar sasa akiwa mwanasheria mkuu
Z'bar awamu ya kikwete.
Kodi wanalipa kwa Serikali yao ambayo ni bil 400 ukiweka na ruzuku ya bara na wahisani.
Kama walishindwa kulipa deni la 60bil. watewazeje kulipa hili?
Kenya ilijimilikisha mali za EAC baada ya kuvunjika muungano na ndio Zanzibar wanachotaka kufanya.
Wanakuja na nyimbo zao wametatua kero za Muungano na hawaziweki wazi ni kero zipi
na zimetatuliwa vipi, akili kumkichwa.
 
kwanini usimalizie ni Nani atalilipa Deni hilo?
Juzi tu Magufuli alikaa na Dr Sheni kufuta Deni la Tanesco, Zanzibar alilokataa kukulipa na alitumia halali.
Mnachotaka huyu Mama Muungano uvunjikie mikononi mwake, ni lazima mlipe madeni yote kwanza maana mnategemea Utalii km Tanganyika hakuna Utalii
Maswali ya kijinga, madeni mengine huwa analipa nani?
 
Nadhani amejibu bila kuelewa mantiki ya hoja. Hoja ni kuwa Mtanganyika akiwa Zanzibar kwenye masuala ya Ajira, kumiliki ardhi na nafasi za kisiasa anatambulika kama mgeni kutoka Kenya, Uganda, Somali, China, Usa, nk. Lakini mzanzibar anapokuja bara kwenye masuala hayo hayo ya Ajira, kumiliki ardhi na fursa za kisiasa anatambulika kama mwenyeji kutoka Kigoma, Dar, Iringa, Arusha nk. Kwanini hili jambo liwe hivyo wakati tuna muungano? Kwanini kuna double standard?

Suluhisho ni nini?
KATIBA MPYA.
Narudia tena sio sahihi ikiwa Ali Hassan Mwinyi, Aboud Jumbe Mwinyi na sasa hivi Hussein Mwinyi wameweza kuwa Rais Zanzibar hoja hiyo haina mashiko mimi nawajuwa watanganyika (Wazanzibara) wengi wameajiriwa Serikalini bila ya taabu na wengine kuwa mawaziri. Suala la Katiba Mpya undeni tuu hiyo ni hiyari yenu suala langu ni uongo kufanywa ndio jambo sahihi kwangu sikubaliani nayo.
 
Hesabu zibadilike sasa kwakuwa tunafanya sensa mwakahuu mgao uchakatwe kwaidadi ya watu yaani uwe hivi ;

Bara
=(wabara ÷ watz) × mkopo/msaada

Zenji
=(wazenji ÷ watz) × mkopo/msaada

Mkopo unalipwa nawatu kwahivyo kilamtizii ahusike kwenye calculation!!
'Wabunye' yetu hayawezi kulisemea hili 'bunyeni' maana kiladakika wanawaza wamfurahishaje 'bibiye' ili waukwae uwaziri au unaibu uwaziri wanaouota kilaiitwapo Leo!!!
Kaziyao nikumsifu 'bibiye' kuliko hata yanavyomsifu Muumba wao...damnittt!!
 
Upo sahihi sana na je..?
usilolijua ni bora uulize masoko yote hayo ni PPP ambapo wawekezaji binafsi wanafanya. Miradi ya bandari Mamngapwani na Malindi pia inajengwa kwa PPP na Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman. Mradi wa Darajani ni uwekezaji wa Kampuni ya AFRICAB ya wazawa. Ni kweli kwa sasa Zanzibar kuna miradi mingi ipo katika Planning Stage lakini asilimia kubwa ni ya uwekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi. Miradi hiyo mchango wa Serikali ni mdogo sana
Una evidence yoyote kuwa masoko yanajengwa kwa wawekezaji binafsi na si wakati ule ila kwa sasa ndipo serikali inawekeza kwa nguvu zote?.

Hapa i wrote issue ya masoko not bandari ( about bandari we'll discuss in next article)

Either wewe ndiye hujui, hata wakati wa madaraja na ununuzi wa mandege huko bara wengi mlipiga mayowe kuhusu serikali kutumia pesa nyingi za ndani ila, baadaye mkaanza ooh mikopo nk.
 
Weka hapa huo mkataba wa Muungano.Pili unaelewa maana ya kero za Muungano? Na je mkataba ni biblia au msahafu?

Mwisho Zanzibar sio Mkoa ni Nchi na pia ni sehemu ya JMT kwa hiyo ina haki zote na tena haki zaidi ya Mkoa.
Suala ni kwamba Zanzibar inapewa mgao mkubwa kuliko makubaliano rasm ya asilimia 4.5%. Si suala la kinchi wala kimkoa!! Wahusika wanaona malalamiko haya kila siku lakini wameziba masikio!! Kama kuna maelezo kuhusu ukiukwaji huu tuambiwe!! kama kuna utetezi wowote tuambiwe!! Au ndo utaratibu wa mbuzi kula kwa kulingana na urefu wa kamba yake?? Inakera!!
 
Hivi karibuni, kuna taarifa zilizowekwa wazi kwenye baadi ya vyombo vya habari, juu ya mgawanyo wa mikopo ya nje, kati ya Tanzania bara na Zanzibar.

Mkopo wa pesa ya Uviko 19, tunaambiwa Zanzibar ilipata 21%. Mkopo wa kutoka Japan, tunaambiwa Zanzibar imepata 30%.

Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, umeweka wazi kanuni ya mgawanyo wa mikopo na misaada kutoka nje, ambapo Zanzibar inastahili kupewa 4.5%.

Kama ni kweli Zanzibar ilipata 21% badala ya 4.5%, na pia ilipata 30% badala ya 4.5%, waliohusika wote, wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Katibu Mkuu Wizara ya fedha, walistahili wasimamishwe mara moja, na kama tungekuwa na Bunge, lilistahili kuunda kamati kuchunguza ukweli wa jambo hili, na kuchunguza uhusika wa Rais katika ukiukaji huu wa kanuni za Muungano.

Jambo la kujiuliza:

1) kwa hali hii ya sasa, ambapo nchi haina bunge linalowakilisha wananchi, nani ataihoji serikali?

2) kama trend itaendelea hivi, mpaka kufikia 2025, hali itakuwaje?

3) kama hiki ndicho kinachoendelea, hatuoni kuna njama za kuitumia Tanganyika kuijenga Zanzibar, na kuifanya Tanganyika kuwa 'kubwa jinga?'

4) Hali ikiendelea hivi, na bunge hatuna, nani ataweza kuhoji juu ya jambo hili?

5) Je, hatuoni kuwa kama hali hii ni kweli, mikopo hii inailenga Zanzibar, na Tanzania bara inatumika tu kama daraja, huku kisheria deni likiwa la kwake?

6) Japo hatuombei, kama kukiwa na njama ambazo zikafanya siku moja Muungano ufe, hatuoni hasara itakayokuwepo kwa Tanzania bara kwa sababu madeni haya yote mkopaji ni yeye, na hivyo ndiye atakayewajibika kulipa?

Watanzania tuna kazi zana kwa uelewa mdogo. Yaani unafikiri mikopo inatolewa kwa mgao! Mikopo ni tofauti na kodi!

Mikopo inatolewa kwa mahitaji na project sio mgao. Hivyo kama haipo kuwe na sheria nyingine ya mikopo. Unaongelea vitu viwili tofauti mikopo na kodi
 
Suala ni kwamba Zanzibar inapewa mgao mkubwa kuliko makubaliano rasm ya asilimia 4.5%. Si suala la kinchi wala kimkoa!! Wahusika wanaona malalamiko haya kila siku lakini wameziba masikio!! Kama kuna maelezo kuhusu ukiukwaji huu tuambiwe!! kama kuna utetezi wowote tuambiwe!! Au ndo utaratibu wa mbuzi kula kwa kulingana na urefu wa kamba yake?? Inakera!!
Tuwekee hayo makubaliano maana naona umekazania uzushi wenu wa 4.5%
 
Mkuu, inaumiza kuona hamna mbunge hata mmoja akihoji mambo kama haya. WOTE ni WAOGA tu. Tunaambiwa wakati wa chama kimoja chini ya Mwalimu Nyerere bunge lilikuwa MOTO likilojaa SAUTI za kuhoji mambo bungeni. Na Nyerere nasikia alipenda sana. Mijadala yenye tija. Leo vyama ni vingi na CCM ndo wengi kwani hamna hata mbunge JASIRI wa kuuliza mambo kama haya? Kama jibu ni HAYUPO basi nchi yetu iko kwenye hatari ya FREE FALL!!!!
Kwa ujumla sasa hivi tuna wabunge wa majina. Wamekosa weledi, wamekosa ujasiri, wamekosa maono. Kwa ujumla ni wabunge wa hovyo kabisa ambao hatujawahi kuwa nao katika historia ya nchi yetu.

Bunge la chama kimoja la akina Arcado Ntagazwa, Njelu Kasaka, na wengine nimewasahau, lilikuwa bunge hasa, siyo huu utopolo wa sasa hivi. Haieleweki hata huko Dodoma wanaenda kufanya nini. Ni aheri wangebakia majumbani kwao.

Kwa ujumla wabunge wa safari hii hawana msaada wowote kwa mtu yeyote zaidi ya familia zao.
 
Topic yako ina mislead the public, 4.5 inazungumzia misaada sio mikopo. Chanzo cha mkataba kikowapi ?
On top of that wazanzibari hawana haja na muungano kama unavyofikiria kuwa wanafaidika.
Ndugu yangu, sijampotosha yeyote. Kanuni hiyo ipo wazi, na inasema:

Misaada ya nje na mikopo ya nje, Zanzibar itapata 4.5%.
 
Ha ha ha eti Tanganyika ndio Tanzania,,
Uko wrong jina TANZANIA liko na zanzibar ndani yake,,,, tukubali tu, tulibugi,,
Tunaweza kurudisha serikalini ziwe tatu,
Lakini sasa inabidi zanzibar ipate kiti UN na kiti cha bara ndio kiwe cha sasa huko
Then iwe shirikisho,,,
Zanzibar wawe na bank kuu yao,jeshi lao na balozi zao nje ,,,
Ni suala la kukubaliana tu, mi sioni shida hapo [emoji23][emoji23]
Kama ulivyovitaja, vyote vikawa hivyo, ina maana Muungano utakuwa umekoma.

Tushirikiane katika yale tu tuliyokubaliana:

Ulinzi
Mambo ya nje
Mambo ya ndani
Sayansi na teknolojia
Elimu ya juu
Sarafu
Usafiri wa anga na majini
 
Sio kila mkopo unaopatikana hugawanywa kila mkoa, hii imetokea awamu hii tu kwenye pesa za uviko
Mikopo huwa inakuja kufanya specific project in a particular place,
Mfano zinaweza toka pesa UNDP bilion 500 kuja kutengeza barabara njombe,, au kujenga mabwawa simiyu, au kuvuta maji ya lake viktoria Tabora,,
Sasa haina maana hizo hela zikitoka, eti zanzibar nao wadai mgao. Au mwanza nao walalamike kwanini hawajapata, au kwanini wamepata kidogo kuliko simiyu, wakati wao wako wengi.
Mikopo inakuja na kufanya kazi kwenye specific project in a particular places,
Umetoa mfano mbaya. UNDP huwa haitoi mikopo wala misaada ya ujenzi wa barabara.

Mashirika ya musaada kama USAID wao wanapotoa msaada, wanautoa na kuupeleka ambako wao wanataka, na mlioukosa hamwezi kudai kwa sababu hawapangiwi na Serikali ya Tanzania.
 
Mama anaupiga mwingi
Labda Rais Samia, siyo muumini wa muundo wa Muungano wa sasa, hivyo anafanya mambo yatakayowaudhi Watanganyika ili ifikie mahali, pande zote waone umuhimu wa Serikali 3 au kuuvunja Muungano.
 
Hebu eleza utaratibu wa kulipa deni la nje ukoje,, je huwa tunaguatwa mmoja mmoja kulipa au ni vipi, wanzanzibar hawalipi kodi?,
Kodi ya Mzanzibari inalipwa kwa SMZ. Deni lilikopwa na JMT, SMZ haidaiwi na mkopeshaji bali JMT inatakiwa iidai SMZ.

Ni sawa na wewe uende bank ukope sh milioni 50, uwekee dhamana nyumba yako, halafu uchukue milioni 20 umpe binamu yako. Binamu yako hafamiki kwa benki na wala hadaiwi na benki, unadaiwa wewe uliyekopa. Huyu binamu yako asipokulipa, wewe ndiye utawajibika kwa benki.
 
Zanzibar walijitoa kuomba mkopo chini ya Tanzania wakiongozwa na Masoud VP wa Zanzibar sasa akiwa mwanasheria mkuu
Z'bar awamu ya kikwete.
Kodi wanalipa kwa Serikali yao ambayo ni bil 400 ukiweka na ruzuku ya bara na wahisani.
Kama walishindwa kulipa deni la 60bil. watewazeje kulipa hili?
Kenya ilijimilikisha mali za EAC baada ya kuvunjika muungano na ndio Zanzibar wanachotaka kufanya.
Wanakuja na nyimbo zao wametatua kero za Muungano na hawaziweki wazi ni kero zipi
na zimetatuliwa vipi, akili kumkichwa.
Hicho ndicho ninachokiona. Zanzibar, nadhani ina mpango wa muda mrefu wa kuvunja Muungano. Wanataka utakapovunjika, wawe wamefaidika kiasi cha kutosha.

Tanganyika ni kubwa jinga ambalo wakati wote linakula hasara. Wakati wa EAC lilipoteza ndege. Zote isipokuwa moja, zilibakia Kenya. Sasa tena kilichotokea EAC kinataka kutokea.
 
Kodi ya Mzanzibari inalipwa kwa SMZ. Deni lilikopwa na JMT, SMZ haidaiwi na mkopeshaji bali JMT inatakiwa iidai SMZ.

Ni sawa na wewe uende bank ukope sh milioni 50, uwekee dhamana nyumba yako, halafu uchukue milioni 20 umpe binamu yako. Binamu yako hafamiki kwa benki na wala hadaiwi na benki, unadaiwa wewe uliyekopa. Huyu binamu yako asipokulipa, wewe ndiye utawajibika kwa benki.
Bibi tozo anawafungisha ndoa ya mkeka wazanzibari..
Siamini kama ya Kenya kuhodhi mali za EAC yatajirudia tena kwa Zanzibar.
 
Hicho ndicho ninachokiona. Zanzibar, nadhani ina mpango wa muda mrefu wa kuvunja Muungano. Wanataka utakapovunjika, wawe wamefaidika kiasi cha kutosha.

Tanganyika ni kubwa jinga ambalo wajati wote linakula hasara. Wakati wa EAC lilipoteza ndege. Zote isipokuwa moja, zilibakia Kenya. Sasa tena kilichotokea EAC kinataka kutokea.
Ngoja tuone mwisho wa hizi ngonjera zao.
"ndani ya miezi sita bibi tozo katatua kero zote za muungano".
 
Watanzania tuna kazi zana kwa uelewa mdogo. Yaani unafikiri mikopo inatolewa kwa mgao! Mikopo ni tofauti na kodi!

Mikopo inatolewa kwa mahitaji na project sio mgao. Hivyo kama haipo kuwe na sheria nyingine ya mikopo. Unaongelea vitu viwili tofauti mikopo na kodi
Nakuonea huruma kwa sababu unachangia jambo usilo na uelewa nalo.

Huo mgawanyo wa Zanzibar kupata 4.5% imetamkwa wazi kuwa ni kwa misaada ya nje na mikopo toka nje.
 
Kwa ujumla sasa hivi tuna wabunge wa majina. Wamekosa weledi, wamekosa ujasiri, wamekosa maono. Kwa ujumla ni wabunge wa hovyo kabisa ambao hatujawahi kuwa nao katika historia ya nchi yetu.

Bunge la chama kimoja la akina Arcado Ntagazwa, Njelu Kasaka, na wengine nimewasahau, lilikuwa bunge hasa, siyo huu utopolo wa sasa hivi. Haieleweki hata huko Dodoma wanaenda kufanya nini. Ni aheri wangebakia majumbani kwao.

Kwa ujumla wabunge wa safari hii hawana msaada wowote kwa mtu yeyote zaidi ya familia zao.
Nakubaliana nawe kabisa. Wabunge wa zamani hawakutanguliza eti kungojea kuteuliwa kwenye uwaziri nk. Wao walikuwa na jukumu la kuwakilisha majimbo yao ya uchaguzi na zaidi ya majimbo yao hayo walihoji sana wakati kulikuwa na tatizo. Hata serikali waliiweka pn toes. Sasa hivi ni kuimba sifa tu. Inasikitisha. Hii elimu mbona haiwasaidii hawa wabunge wetu?
 
Mgao wa zanzibar unatakiwa kuwa proportionate na mikoa mingine ya Tanzania, kimsingi ukubwa na idadi ya watu ya zanzibar ni sawa na mikoa mingine iliyopo Tanganyika...
Hey stop!

Hakuna mkoa wa Tanganyika unaolingana na Zanzibar!

Zanzibar ni ndogo kuliko SIKONGE

ZANZIBAR, eneo la kilomita za mraba 2,462, inaingia Halmashauri ya Wilaya ya SIKONGE, eneo la kilomita za mraba 27,842, mara kumi na nne!

Kwa idadi ya watu, Zanzibar, Unguja na Pemba that is, watu mil 1.4 wanaingia Halmashauri ya Wilaya wa Kinondoni, watu 2.8 mil mara mbili!

Watu wa Zanzibar - kama watu wote wa Kinondoni wangehama wakapaacha wazi for 15 minute in a demographic experiment - Wazanzibar wasingeweza kujaza viwanja, majumba, mashamba, mashule, biashara na ajira za Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni!

Julius Nyerere's most catastrophic decision was indisputably the fat-headed blunder of subsuming out country in a union with the pea-sized Zanzibar archipelago.
 
Back
Top Bottom