Habari zenu wakuu?
Kama nitamkwaza mtu naomba nisamehewe lakini siwezi kukaa kimya.
Serikali imetoa mpangilio wa matumizi ya mkopo wa IMF , Tsh Trillion 1.3 za kitanzania.
Kama ifuatavyo;
(i). Sekta ya maji- Billion 139.4
(ii). Elimu -Billion 368.9
(iii). Afya - Billion 90.2
(iv).Jamii yenye maisha duni - Billion 5.5
(v). Makundi maalum - Billion 5
(vi). Shughuli za uratibu - billion 5
(vii). SERIKALI YA ZANZIBAR - BILLION 231
********************************************
* Yani Tanzania bara tupo zaidi ya million 55 ila jamii yenye mazingira magumu inapewa billion 5 wakati kwa takwimu za harakaharaka nadhani inakadiriwa waTz wenye maisha duni ni zaidi ya million 7. ni dhahiri hiyo hela haitoshi kbsa maana hata watu wa tasafu wanalipwa kiduchuuuuuu.
*Zanzibar ina wakazi zaidi ya 1 million kwanini fedha zote hizi ziende kwao ilihali serikali ingepunguza walau billion 100 na kuzijaza kwenye yafuatayo...
-mikopo ya vijana yenye riba nafuu au 0% riba
-kuongeza hela kwenye hiyo bajeti ya afya ili hospitali za wilaya na zahanati za kata vijijini vikapata vifaa pungukiwa.
-basi jamani hata walimu kadhaa wajengeeni nyumba za kukaa hata mbili tatu za kuzuga na hyo bilion 100
HAYO NI BAADHI AMBAYO YAPO KICHWANI KWANGU ILA NAJUA KILA MTU ANA YAKE AKILINI.
Ni nini faida ya muungano kwa Tanzania bara?
mzalendo wa kweli.
Hapa kwetu lita ya mafuta ya kula imefika 9000
mkate- 1300
soda -700
mchele wa kawaida 1kg-2200
Chanzo ya picha ya budget -TBC
maoni yaliongezewa - Mzalendo wa kweli
Nawasilisha.