Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Hilo ndio suluhisho Katiba mpya na serikali ziwe Tatu, Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania hizi chokochoko tunazifukia baharini[emoji3][emoji3]
Sawa kabisa,, JMT iwe symbolic,
Zanzibar wawe na Mamlaka kamili jeshi na polisi wao,, pia wawe na kiti UN
 
Zanzibar acha waitumue vyema fursa waliyo ipata. Inaweza isijirudie tena. Na baada ya miaka 20 tukiendelea hivi zanzibar haitakamatika. Kuna uwezekano mkubwa wananchi wa kule wakapata benefits nyingi na bora sana.

Jiulize deni tunalo wadai la umeme wamesha lilipa? Au wanatulalia tu
Mnawadai shilingi ngapi deni la umeme?
Weka mchanganuo wake hapa, uonyeshe ni la mwaka gani na gani, mliwauzia units ngapi kwa shilingi ngapi na wamelipa au hawakulipa ngapi.

GT wanataka kujua vitu kama hivyo, sio uongo uongo tu na umbeya mwingi kama wanawake wa Kiswahili.
 
Kwa nini hamtaki kuungana na Burundi mpate hizo serikali 3 mnazotaka? 1964 Zanzibar ilikosa silaha za kupambana na genge la akina Okello na wenzake waliovamia Zanzibar. Zingekuwepo ingetokea kama kinavyotokea Ukraine.
Jenga Hoja mkuu Zanzibar kuwa km mwanzo sahau aliyeiunga ni karume ndo mtu pekee aliekuwa na uwezo wa kuvunja Muungano na kuifanya Zanj iwe huru wapili ni Aboud Jumbe likamkuta lakumkuta hakuna mwengine anaeweza na kudhubutu. [emoji3][emoji3][emoji1787] Issue ni katiba mpya na hizo serikali 3.
 
Mngelalamika na Magufuli alivyokuwa anaipendelea chato,

Simlikuwa mnasema Chato nayo Ni Tanzania hakuna ubaya eti!!!
Kijana.

Kama kweli unataka kumsaidia Rais.

Mshauri aangalie swala la uchumi ukosefu wa fedha na ajira ni mkubwa.

Usimdanganye kwa kumsifia tu.

Mwambie ukweli.
 
Mnawadai shilingi ngapi deni la umeme?
Weka mchanganuo wake hapa, uonyeshe ni la mwaka gani na gani, mliwauzia units ngapi kwa shilingi ngapi na wamelipa au hawakulipa ngapi.

GT wanataka kujua vitu kama hivyo, sio uongo uongo tu na umbeya mwingi kama wanawake wa Kiswahili.
Unadhani kwanini raisi msitaafu alisema mngewasha kibatari endapo umeme ungekatwa? Na tena akaongeza kuwa hilo swala linatambulika tangu awamu zilizo pita. deni la zaidi ya miaka 20. Sasa wewe una taarifa zaidi ya raisi wako?
 
Jenga Hoja mkuu Zanzibar kuwa km mwanzo sahau aliyeiunga ni karume ndo mtu pekee aliekuwa na uwezo wa kuvunja Muungano na kuifanya Zanj iwe huru wapili ni Aboud Jumbe likamkuta lakumkuta hakuna mwengine anaeweza na kudhubutu. [emoji3][emoji3][emoji1787] Issue ni katiba mpya na hizo serikali 3.
Karume ni mtu wa Malawi, mambo ya Zanzibar hayamhusu. Swali bado lipo, kwa nini hamtaki kuungana na Burundi au hata Msumbiji mpate hizo serikali 3 mnazotaka kila siku?
 
Miaka yote mikopo ikitoka inatumika bara tu, na wazenji hawakuruhusiwa kukopa kama wao,, watu wa bar tuna ubinafsi sana[emoji28]
Nahuu uwazi na ukweli ndo shida ilipo yaani wa Tz wakifichwa mambo ndo wanatulia wacha wale bata bana.
 
Kuna madai kuwa BOT ilianzishwa kwa fedha za pamoja zanzibar na bara n a share ni asilimia 25.
Wanzeji wanalijua hili na hata ujenzi wa bwawa la umeme fedha ilitoka zanzibar na umeme wa upepo ulipigwa chini.
 
Karume ni mtu wa Malawi, mambo ya Zanzibar hayamhusu. Swali bado lipo, kwa nini hamtaki kuungana na Burundi au hata Msumbiji mpate hizo serikali 3 mnazotaka kila siku?
Hakuna muenyeji Zanzibar wote wakuja umeona wapi kisiwa kikawa kina uzawa wasili hata ww usikute babu yako wa baba yako kwao Congo au Muscat huko.
 
Kilo moja ya sukari Zanzibar ni sh 1900 je ni wapi bara sukari inauzwa hivyo na je Zanzibar wana viwanda vingapi vya sukari?? Hawa jamaa wanatukamua kweli na siajabu ukakuta umeme wa sh 2000 zanzibar mtu anapata unit 75
Niko Zanzibar 2000 napata unit 4.8, japo sifurahii kabisa huu muungano wa kinyonyaji.
 
Habari zenu wakuu?
Kama nitamkwaza mtu naomba nisamehewe lakini siwezi kukaa kimya.

Serikali imetoa mpangilio wa matumizi ya mkopo wa IMF , Tsh Trillion 1.3 za kitanzania.

Kama ifuatavyo;

(i). Sekta ya maji- Billion 139.4
(ii). Elimu -Billion 368.9
(iii). Afya - Billion 90.2
(iv).Jamii yenye maisha duni - Billion 5.5
(v). Makundi maalum - Billion 5
(vi). Shughuli za uratibu - billion 5

(vii). SERIKALI YA ZANZIBAR - BILLION 231

********************************************

* Yani Tanzania bara tupo zaidi ya million 55 ila jamii yenye mazingira magumu inapewa billion 5 wakati kwa takwimu za harakaharaka nadhani inakadiriwa waTz wenye maisha duni ni zaidi ya million 7. ni dhahiri hiyo hela haitoshi kbsa maana hata watu wa tasafu wanalipwa kiduchuuuuuu.

*Zanzibar ina wakazi zaidi ya 1 million kwanini fedha zote hizi ziende kwao ilihali serikali ingepunguza walau billion 100 na kuzijaza kwenye yafuatayo...

-mikopo ya vijana yenye riba nafuu au 0% riba

-kuongeza hela kwenye hiyo bajeti ya afya ili hospitali za wilaya na zahanati za kata vijijini vikapata vifaa pungukiwa.

-basi jamani hata walimu kadhaa wajengeeni nyumba za kukaa hata mbili tatu za kuzuga na hyo bilion 100

HAYO NI BAADHI AMBAYO YAPO KICHWANI KWANGU ILA NAJUA KILA MTU ANA YAKE AKILINI.

Ni nini faida ya muungano kwa Tanzania bara?


mzalendo wa kweli.
Hapa kwetu lita ya mafuta ya kula imefika 9000
mkate- 1300
soda -700
mchele wa kawaida 1kg-2200


Chanzo ya picha ya budget -TBC
maoni yaliongezewa - Mzalendo wa kweli

Nawasilisha.

Mkuu. mimi sijui na wala sina jibu la mambo haya, lakini inanisukuma nichangie mjadala huu, kwani ni muhimu zaidi kuliko kukaa kimya na maumivu ndani kwa ndani.

Binafsi ningetegemea kuwa kuna utaratibu maalum unaoeleweka wa mambo kama haya kufanyika. Kama utaratibu huo upo, na ulishajadiliwa na kukubaliwa, basi, tutafute jibu huko. Na kama bado hairidhishi, kwa maana kwamba utaratibu uliopo siyo sahihi, ufumuliwe na uwekwe wenye uwiano unaostahili.

Lakini kama mambo haya sasa hivi yanafanyika kama mazoea tu, kwa vile mkuu ni wa kutokea huko, basi haifai hata kidogo kuyanyamazia.
Nadhani litakuwa ni jambo muhimu la kutumia ule utaratibu ambao mara nyingi umetumiwa na sehemu moja ya muungano, utaratibu unaoitwa 'KERO ZA MUUNGANO"..., sasa Kero zitakuwa zinaelekezwa upande wa pili (Tanganyika), badala ya kulivyozoeleka kuwa zinaelekezwa Visiwani.

Pili, hii ni hela ya mkopo, mkopo unaotolewa kwa serikali ya Tanzania, na ni hiyo hiyo itakayolipa mkopo huo. Kwa maana halisi ni kwamba sehemu kubwa sana italipwa na watu hao milioni 55 walioko sehemu moja ya Muungano, na wale milioni moja, uchangiaji wao katika kuulipa huo mkopo ni mdogo zaidi.

Baada ya kuyasema haya, nami naungana nawe katika kuuona huu utaratibu wa mgawanyo kama "KERO" hasa, kwa wale walioko Bara.
 
Hakuna muenyeji Zanzibar wote wakuja umeona wapi kisiwa kikawa kina uzawa wasili hata ww usikute babu yako wa baba yako kwao Congo au Muscat huko.
Waliohamia kwanza ndiyo wenjeji. Kama mnavyofanya huko bara. Wengi mna asili ya kwengine lakini waliohamia kwanza huko Sukuma land ndiyo wenyeji.
 
Tanganyika tunarudi nyuma kwa spidi ya mwanga huku Zanzibar ikichanja mbuga kuelekea kwenye neema.
Na ubaya zaidi ni kwamba huwezi ukasema na wewe utahamia huko ili ukafaidi keki; lakini yule aliyeko huko, akiona kuna unafuu upande wa pili, ana HAKI ya kufuata huo unafuu upande wa pili!

Lakini nasema hivi: Hali hii sasa ndiyo itakayozaa Muungano imara tunaoutafuta. Hawa wenye 'privilege' sasa, itafika mahala watakwamwa na ndoana wasiweze kuitema tena, watake wasitake.
 
kama kipindi cha jiwe zooote zilieklekezwa kule kitovuni kwani sasahivi zikienda kizimkazi mnakasirika, acheni nongwa wajameni kipindi kile mabakuli yooote mlifunga, sasahivi mnajifanya mnaropoka shikeni adabu mama aupigwe mwingi alaaaaaaaaaaaaaah
 
Siri ya mtungi aijue _____ Usikute haya hata mwanzo yalifanyika lkn kukawa na usiri.

Huu Muungano kuna haja yakurekebishwa zaidi kwa baadhi ya vipengele zaidi ni vyema kila upande ungejitegemea kwenye swala zima la mikopo kila mtu abebe msalaba wake lakini usikute mtoa mada unalalamika wakati hata hiyo Zanzibar haina mamlaka ya kukopa km nchi bila kibali cha Tanganyika.
Katika mambo waliyopigania sana ni kuweza kukopa. Rais JK akawapa fursa hiyo
Rais Shein amekopa katika ziara zake huko Uarabuni ni Malaysia .
Hivyo suala la kukopa si mjadala tena, wanaruhusiwa
Na usikute kuna mikopo inakuwa address kwa Zanzibar moja kwa moja lkn mtoaji kibali nani kuidhinisha hilo ni Tanganyika so unategemea nini wakati hayo yalikuwa yanafanyika nyuma sasa aliekuwepo ni Mzanzibari na moja yamambo yalikuwa yanapigiwa kelele ni haya niwakati wake kuwaliwaza WaZanzibar.
Hapana hawahitaji kukopa. Nitashangaa sana kama Zanzibar watataka kukopa halafu wazuiwe.
Tunachokataa ni kukukopa kwa dhamana ya Tanganyika kwasababu Wazanzibar wanatabia ya kukopa hawalipi. Walikopa Tanesco mabilioni waliolipa ni Watanganyika
 
Unadhani kwanini raisi msitaafu alisema mngewasha kibatari endapo umeme ungekatwa? Na tena akaongeza kuwa hilo swala linatambulika tangu awamu zilizo pita. deni la zaidi ya miaka 20. Sasa wewe una taarifa zaidi ya raisi wako?
Weka data kijana acha kuruka ruka.
Tangu muda huo mpaka leo imepita miaka mingapi. Unataka kuniambia,hakuna deni au sehemu ya deni lililolipwa, na hakuna mauziano mapya tangu kipindi hicho au mauziano yapo mnalipwa in full, isipokuwa hilo deni la wakati huo tu ndio bado kulipwa?

Kama sivyo basi mchanganua bado unahitajika.
 
Back
Top Bottom