Muungano wetu: Ujumbe huu kwenye bango la Timu ya Taifa Zanzibar unamaanisha nini?

England, Scotland, Wales, ni muungano ila kila mmoja ana
Bendera yake
Wimbo wake wa taifa
Timu yake ya taifa

Ila ligi wales na England ni ligi moja


Waziri mkuu ni mmoja kwote

Na bunge la muungano ni moja kama huku
 
Anhaa angalau umetuelewesha,Sasa kama hawatambuliki na Caf wamewezaje kuwa na mchezo dhidi ya Kilimanjaro stars
 
Yaani waondoke tu. Yaani mi naitamani sana Tanganyika yetu. Kushirikiana kumerudisha maendeleo nyuma
 
Mkuu ahsante kwa maelezo mazuri,na hapa Sina chakukubishia maana Sina experience ya kuish nao ila maoni yangu yalitegemea vyanzo fulani tu vya habari, ahsante kwa masahihisho.
 
Mimi badala ya kuutafsiri ujumbe huu kuwa ni "uhaini" kama mmoja alivyodai huko chini, ninaona kama ni "uchochezi uchwara" kwa kupindisha lengo la ujumbe kutoka kwenye mpira hadi shutuma za kutaka kuvunja Muungano.
Tafuta makala moja Aljazeera inaitwa Football rebels uone namna mpira wa miguu unavoweza kuwa na athari mbaya kwenye siasa. Mfano moja ya sababu kuu ya kujitenga kwa Croatia kutoka Yugoslavia ni mechi moja kati ya Red Star Belgrade dhidi ya Dynamo Zagreb
 
Wawapatie tu uhuru wa kispoti angalau maana kisiasa mmmh kuna kazi Brigedi ya Nyuki TPDF Ipo kule kwa kazi maalum,asilimia 70 ya wanajeshi ni wabara kule kisiwani
 
Mkiwa nje ya East Africa, Wakenya na Watanganyika wanakuwa karibu zaidi kuliko hata Mtanganyika na Mzanzibar. Wanzanzibari wengi wanaiweka mbele sana Dini hata kwenye mambo ya kawaida kinyume na Watanganyika na wakenya kiasi kwamba wao wanatembea na Ile slogan ya Islam ndugu yake muislam na wao pekee ndiyo wanajiona waislamu zaidi. Lakini pia Kwa sababu ya udogo wa Zanzibar kunawafanya wakose Ile kujichanganya na wenzao.
Hata utamaduni wa Kenya na Tanganyika ni kama unafanana including chakula kinacholiwa Kwa pande hizi zinafanana sana kuliko hata Tanganyika na Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…