Muungano wetu: Ujumbe huu kwenye bango la Timu ya Taifa Zanzibar unamaanisha nini?

Muungano wetu: Ujumbe huu kwenye bango la Timu ya Taifa Zanzibar unamaanisha nini?

Mi jana nimebaki mdomo wazi. Nilidhani naujua huu muungano ila kiukweli bado kuna vingi si vijui ila nadhani ni kwa kuwa pia havieleweki hata uwe mfuatiliaji kiasi gani.

Hivi ni muungano gani ambao upande mmoja una bendera, wimbo wa taifa na rais?

Hawa wachezaji waliozaliwa ughaibuni wanaoshawishiwa kuja kucheza huku kwa siku za karibuni ni kigezo au sheria gani inawafanya wachezee huku na sio Zanzibar heroes. Mfano michuano ambayo Zanzibar heroes wanaenda independently from Tanzania je hawa kina Kawawa wanaruhusiwa kucheza upamde wa Zanzibar heroes au Kilimanjaro stars?

Hili bango wangelishika Kilimanjaro stars wakihitaji Tanganyika itambuliwe hali ingekuwaje?

Hivi huu ni muungano kweli au ni nchi moja ina ilea nchi nyingine hadi hapo nchi inayolelewa itakapo kuwa na uwezo wa kujitawala itapewa uhuru wake kama ilivokuwa Tanganyika na Waingereza?

Hivi huu ndo muungano aliouunda Nyerere au kuna mambo yalikuja badilishwa yeye akiwa hajui, mbona kama alikuwa vizuri upstairs ila hii kazi ya mikono yake haieleweki kabisa?
England, Scotland, Wales, ni muungano ila kila mmoja ana
Bendera yake
Wimbo wake wa taifa
Timu yake ya taifa

Ila ligi wales na England ni ligi moja


Waziri mkuu ni mmoja kwote

Na bunge la muungano ni moja kama huku
 
Kwa kuwa huu ujumbe umo katika nembo ya CAF na wala sio nembo ya Umoja wa Afrika, iko wazi kuwa Zanzibar Heroes au Timu ya Taifa ya Zanzibar, inachoomba hapa ni uanachama wa CAF. Mimi badala ya kuutafsiri ujumbe huu kuwa ni "uhaini" kama mmoja alivyodai huko chini, ninaona kama ni "uchochezi uchwara" kwa kupindisha lengo la ujumbe kutoka kwenye mpira hadi shutuma za kutaka kuvunja Muungano.
Naomba hapa tujadili iwapo Zanzibar ina haki ya kuwa mwanachama wa CAF au la. Ikiwa Wana haki au hawana, ni kwa nini na kwa maslahi ya nani.
Anhaa angalau umetuelewesha,Sasa kama hawatambuliki na Caf wamewezaje kuwa na mchezo dhidi ya Kilimanjaro stars
 
Timu ya Taifa ya Zanzibar maarufu kwa jina la Zanzibar Heroes imebeba bango lenye logo ya CAF likiwa na ujumbe huu;

"Zanzibar should be restored as the 55th member state. Its time now to take us seriously" ~ "Zanzibar inapaswa kurudishwa kama mwanachama wa 55. Ni wakati sasa wa kutuchukua kwa uzito"

Ujumbe huu unamaanisha nini?

Yaani waondoke tu. Yaani mi naitamani sana Tanganyika yetu. Kushirikiana kumerudisha maendeleo nyuma
 
Mimi nipo karibu sana na wakenya na ninaishi nao vizuri tu ingawa huwa tunabishana mambo ya uchumi na utalii. Wakenya ukiishi nao nje ya Africa wanakuwa karibu sana na watanzania kuliko hata waganda na waafrica wengine.
Tunacheza nao mpaka upatu, na pia wakenya wa jinsia nyingine ni mteremko sana kwa waTz.

Sasa kuhusu experience yako, hapo siwezi kukubishia but from my experience, tukiwa nje ya nchi zetu huwa tunahesabiana kama tupo karibu ukilinganisha na watu kutoka mataifa mengine.
Mkuu ahsante kwa maelezo mazuri,na hapa Sina chakukubishia maana Sina experience ya kuish nao ila maoni yangu yalitegemea vyanzo fulani tu vya habari, ahsante kwa masahihisho.
 
Mimi badala ya kuutafsiri ujumbe huu kuwa ni "uhaini" kama mmoja alivyodai huko chini, ninaona kama ni "uchochezi uchwara" kwa kupindisha lengo la ujumbe kutoka kwenye mpira hadi shutuma za kutaka kuvunja Muungano.
Tafuta makala moja Aljazeera inaitwa Football rebels uone namna mpira wa miguu unavoweza kuwa na athari mbaya kwenye siasa. Mfano moja ya sababu kuu ya kujitenga kwa Croatia kutoka Yugoslavia ni mechi moja kati ya Red Star Belgrade dhidi ya Dynamo Zagreb
 
Wawapatie tu uhuru wa kispoti angalau maana kisiasa mmmh kuna kazi Brigedi ya Nyuki TPDF Ipo kule kwa kazi maalum,asilimia 70 ya wanajeshi ni wabara kule kisiwani
 
Mimi nipo karibu sana na wakenya na ninaishi nao vizuri tu ingawa huwa tunabishana mambo ya uchumi na utalii. Wakenya ukiishi nao nje ya Africa wanakuwa karibu sana na watanzania kuliko hata waganda na waafrica wengine.
Tunacheza nao mpaka upatu, na pia wakenya wa jinsia nyingine ni mteremko sana kwa waTz.

Sasa kuhusu experience yako, hapo siwezi kukubishia but from my experience, tukiwa nje ya nchi zetu huwa tunahesabiana kama tupo karibu ukilinganisha na watu kutoka mataifa mengine.
Mkiwa nje ya East Africa, Wakenya na Watanganyika wanakuwa karibu zaidi kuliko hata Mtanganyika na Mzanzibar. Wanzanzibari wengi wanaiweka mbele sana Dini hata kwenye mambo ya kawaida kinyume na Watanganyika na wakenya kiasi kwamba wao wanatembea na Ile slogan ya Islam ndugu yake muislam na wao pekee ndiyo wanajiona waislamu zaidi. Lakini pia Kwa sababu ya udogo wa Zanzibar kunawafanya wakose Ile kujichanganya na wenzao.
Hata utamaduni wa Kenya na Tanganyika ni kama unafanana including chakula kinacholiwa Kwa pande hizi zinafanana sana kuliko hata Tanganyika na Zanzibar.
 
Back
Top Bottom