choza choza
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 2,081
- 3,831
England, Scotland, Wales, ni muungano ila kila mmoja anaMi jana nimebaki mdomo wazi. Nilidhani naujua huu muungano ila kiukweli bado kuna vingi si vijui ila nadhani ni kwa kuwa pia havieleweki hata uwe mfuatiliaji kiasi gani.
Hivi ni muungano gani ambao upande mmoja una bendera, wimbo wa taifa na rais?
Hawa wachezaji waliozaliwa ughaibuni wanaoshawishiwa kuja kucheza huku kwa siku za karibuni ni kigezo au sheria gani inawafanya wachezee huku na sio Zanzibar heroes. Mfano michuano ambayo Zanzibar heroes wanaenda independently from Tanzania je hawa kina Kawawa wanaruhusiwa kucheza upamde wa Zanzibar heroes au Kilimanjaro stars?
Hili bango wangelishika Kilimanjaro stars wakihitaji Tanganyika itambuliwe hali ingekuwaje?
Hivi huu ni muungano kweli au ni nchi moja ina ilea nchi nyingine hadi hapo nchi inayolelewa itakapo kuwa na uwezo wa kujitawala itapewa uhuru wake kama ilivokuwa Tanganyika na Waingereza?
Hivi huu ndo muungano aliouunda Nyerere au kuna mambo yalikuja badilishwa yeye akiwa hajui, mbona kama alikuwa vizuri upstairs ila hii kazi ya mikono yake haieleweki kabisa?
Bendera yake
Wimbo wake wa taifa
Timu yake ya taifa
Ila ligi wales na England ni ligi moja
Waziri mkuu ni mmoja kwote
Na bunge la muungano ni moja kama huku