Muwaache wanafunzi waliorudi likizo, msiwarubuni kimapenzi

Muwaache wanafunzi waliorudi likizo, msiwarubuni kimapenzi

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Wakuu poleni na majukumu ya siku ya leo. Nimekuwa nikifatilia mienendo ya wanafunzi wetu pindi wanapokuwa likizo nikajiridhisha kuwa watoto wengi wanaingizwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume wasio waadilifu. Kipindi hiki kuna wanafunzi waliomaliza Kidato cha Sita mtaani, wapo waliomaliza kidato cha nne (Pre-form five).

Lipo pia kundi lingne kuanzia chekechea mpka kidato cha tano wanakuja mtaani (likizo ndefu). Nawaomba sana hasa wanaume kuwatunza vema wanafunzi wetu hasa mabinti, kumbukeni sheria kali zilizopo. Usikubali kwenda jela kwa raha ya mda mchache maana JAIL IS REAL.

Akina mama pia wamekuwa na hulka ya kuwarubuni watoto wa kiume na kufanya nao mapenzi (kuwaharibu kisaikolojia) naomba mbadilike term hii jamani mnaharibu Taifa la Kesho. Kwa kufanya hivyo mnawapa kazi kubwa sana walimu pindi shule zinapofungulia.

Mara kusolve kesi za mimba, mara kesi za mahusiano n.k. Kumbukeni mtoto analelewa na jamii nzma, future yake ipo mikononi mwa kila mmoja wetu. Unapowatongoza unahalilisha kuja kuwa na Taifa la WADANGAJI, MALAYA WALIOKUBUHU ambao hawawezi kujenga hoja za kutatua changamoto hata za familia.

Nipo kwenye hatua za mwisho kuandika barua kwenda kwa Rais kuhusu kuongeza adhabu kwa wazinzi, washenzi wote wanaotembea na wanafunzi either wa kiume au wa kike. Pia, nitamshauri Rais aweke gereza maalumu la washenzi wa aina hiyo ili wawe wanateswa vizuri vizuri.

JAIL IS REAL, TAKE CARE.

1622792835599.png

Wakuu poleni na majukumu ya siku ya leo.Nimekuwa nikifatilia mienendo ya wanafunzi wetu pindi wanapokuwa likizo nikajiridhisha kuwa watoto wengi wanaingizwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume wasio waadilifu.Kipindi hiki kuna wanafunzi waliomaliza kidato cha Sita mtaani,wapo

JAIL IS REAL,TAKE CARE.
Sawa tumekuelewa ila tusitishane tafadhali.
 
Uzinzi na umalaya ni kipaji kama ilivo kucheza mpira au basket ball na inaonekana mapema kama vipaji vingine tu toka udogoni ndio maana mkiambiwa mchague wa kuzaa naye mnakuwa na jazba na hasira,serikali hawezi kuingilia vipaji vya watu its in human nature.

WHERE THERE IS A WHEEL, THERE IS A WAY!!
 
Mda mwingne tatizo ni vibint vyenyewe, ukikitana nako kwenye daladala mavazi kaliyovaa na style ya nywele kichwan kalioweka vinapokuwa likizo uwez jua kama ni mwanafunzi.
 
Mda mwingne tatizo ni vibint vyenyewe, ukikitana nako kwenye daladala mavazi kaliyovaa na style ya nywele kichwan kalioweka vinapokuwa likizo uwez jua kama ni mwanafunzi.
Unatakiwa kuvielimisha vivae vizuri mkuu
 
Nipo safarini peke yangu kwenye gari, kuna sehemu muda si mrefu nimesimama kunywa chai, kanipita mtoto wa Form 4 au Form 5 hivi akanisalimia "MAMBO".

Bado ninaitafakari sana hio salamu ya mambo huyo mtoto alionipa wadau. Najiuliza, ndio tuseme anapima maji, au amekubali flag, au alijaribu kuniseti anivunje goti (Anipige mzinga) au ndio zarau za kurudi mtaani.
 
Hapo miaka 60 inapiga hodi kwako mzee stuka😂😂😂😂
 
Unatakiwa kuvielimisha vivae vizuri mkuu
Unataka matusi na kudharirishwa hapo sasa. Kwanza uwezi jua kama ni mwanafunzi pili yeye vinajidai kubehave kama viwatu vizima, salamu utasikia "mambo" au "mambo we kaka" wakat ukikaangalia umekapita age kama miaka 10
 
Duuuh hapo ongozwa na Mungu wako kwa imani yako uipuke hicho kikombe
 
Uzinzi na umalaya ni kipaji kama ilivo kucheza mpira au basket ball na inaonekana mapema kama vipaji vingine tu toka udogoni ndio maana mkiambiwa mchague wa kuzaa naye mnakuwa na jazba na hasira,serikali hawezi kuingilia vipaji vya watu its in human nature.

WHERE THERE IS A WHEEL, THERE IS A WAY!!
Mmmmmmmh
 
Back
Top Bottom