Muziki kutoka nchini Zaire (sasa ni D.R.C) uliwezaje kutamalaki na kupendwa sana hapa Tanzania ilhali tumepakana na jirani wengine takribani 6?

Muziki kutoka nchini Zaire (sasa ni D.R.C) uliwezaje kutamalaki na kupendwa sana hapa Tanzania ilhali tumepakana na jirani wengine takribani 6?

Huyo wa job fununu eti kapigwa kipapai

Huyu wa kuzima anajiandaa kwenda church ( ndo rafiki yangu kuliko wote hao) eti alidhulumu mtu shamba kigamboni akalambwa albadili[emoji848][emoji848][emoji848][emoji26]

Huyo wa baruti eti aliwazingua watoto wa kihindi (alikwangua gari yao then akaleta ubabe) wakaamua kumlipua

Hizo zote ni fununu jamani si unajua kitaa, ila nimeogopa balaa, nimejikuta leo nimekuwa mtakatifu gabriel, natamani kumpigia kila mtu goti[emoji1751][emoji1751]
Hivi baruti nayo kumbe ni silaha inayoua?mimi nilikuwa nafikiri kazi ya baruti ni kitishia watu mitaani kwa ule mlio wake ikipigwa sikujua kama inatumika kama silaha
 
Tuendeleeni na madhumuni ya huu Uzi jamani. Mambo mengine binafsi mwende Inbox. Kila mtu akianza hapa kujielezea yeye na issue zake hata hatutafanikiwa lengo la uzi. Tuleteane hbr za Music wa Congo.
 
DRC, batoto ba Congo.......Mobutu ama (Kuku mbengu wa Zabanga), ni kweli alichukia sana mambo ya kuiga umangaribi, lakini hapo hapo akawa anatamani sana maisha ya Kifaransa!...baada ya kuwaambia bana ba congo kuacha majina ya kikoloni kama vile Franco ama Rochereau...ambao wakati huo ndio walikua wakali wa muziki, Majina ya kabakia Luambo Luanzo Makiadi na Tabu Ley.

Mobutu kapiga kampeini kubwa sana ya kuondoa Ukoloni mambo leo , ndio mpaka sasa Congo Drc kuna Dini na kanisa la ki itikadi ya Kiafrika inayoitwa 'Kimbangiste'..... Makanisa yalibaki kufunza vijana kupiga muziki.....vile vile kwa vile walitawaliwa na Wafransa, kuna kitu kinaitwa ''Assimilation" yaani kuigiza aliekuteka mpaka ufanane nae...ilibidi watafute vyombo na machine za kurecodi za hali ya juu sana, ndipo unaona ngoma zao nyingi ni kali mpaka kesho...rekoding either Paris , belgium ama Us!
 
DRC, batoto ba Congo.......Mobutu ama (Kuku mbengu wa Zabanga), ni kweli alichukia sana mambo ya kuiga umangaribi, lakini hapo hapo akawa anatamani sana maisha ya Kifaransa!...baada ya kuwaambia bana ba congo kuacha majina ya kikoloni kama vile Franco ama Rochereau...ambao wakati huo ndio walikua wakali wa muziki, Majina ya kabakia Luambo Luanzo Makiadi na Tabu Ley.
Franco anajua sana kupiga Gitaa mzee baba...
 
Huyu ni mwamba haswa... Ndio maana Franco alikuwa anampenda sana although alikuwa back vocal kwenye band yake ya T.P.O.K but baadae aliimprove... Na baada ya kufa kwa Franco 1989 band ilisitisha kufanya muziki kwa mwaka mzima na waliporudi Madilu ndio alikuwa kiongozi wa band hiyo.

Hiyo Faute ya Visa to cut story short...unakutana na mtu katika nchi ambayo unahitaji visa kabla ya kwenda. Mtu ambaye unakutana naye au mtu anayekabiliana nawe hataweza kukutana nawe tena nyumbani. Mtindo wa maisha unayoishi na mahali unakokwenda sio ya viwango vyake. Watu ambao walimpa visa hawajui kwamba atakuwa akisababisha shida huko alikoenda. Madilu unaposema Faute Ya Visa, analaumu ukweli kwamba mtu huyu asiyejali pia alipewa visa. Madilu anajikuta katika nchi ambayo hawezi kufanya mengi.

Sent from my SM-G970U1 using JamiiForums mobile app
Excelent
 
makambo maana yake “Tabu/matatizo” sasa hapo wanasema kinshasa makambo ngai mwana moto (kinshasa ina matatizo ,mimi mtoto wa mtu)
katika huo wimbo “Ngugi” Franco anawafananisha watu wa kinshasa na mbu wa jinsi wanavyoongea kwa kumsema anasema , hii ni True story maana watu wa kinshasa walimsema mno mara mchawi nk sasa akawa analalamika kwenye nyimbo zake nyingi mfano kuna moja inaitwa kimpa kisangameni anasema “swela obota ngai, ngai makila mabe mama” akimaanisha kwamba (swela umenizaa na damu mbaya)
Kimpa kimsangameni nyimbo tamu mno ya mwaka 1976
 
Back
Top Bottom