Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Meli ya MV LIEMBA, inayotoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo katika Ziwa Tanganyika, inatarajiwa kurejea katika huduma hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ukarabati mkubwa ulioanza Julai 2024.
Ukarabati huo umehusisha mabadiliko makubwa ya mifumo na miundombinu ya meli, ikiwemo kubadilishwa kwa mashine, viti na vitanda, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa meli, usalama na kuboresha mazingira ya safari kwa abiria.
MV LIEMBA ina uwezo wa kubeba hadi abiria 600 na tani 200 za mizigo kwa safari moja, hivyo kurejea kwake kunatarajiwa kuimarisha usafirishaji wa watu na bidhaa katika maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika.