Mvua inayoendea Dar ni hatari sana, wale waliokuwa wanawabeza TMA wapo?

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa moja,

Katika kipindi cha miaka 7 Dar sijawahi kushuhudia mvua kama iliyopiga siku mbili hizi haswa ya leo ndio bab kubwa sehemu nyingi maji yamejaa sana.

Tukirudi nyuma wakati tahadhari zinatolewa na TMA wabongo wengi mitandaoni na mitaani walikuwa wanabeza sana na wengine kuleta dhihaka, sasa kwa hali inayondelea bado wale waliokuwa wanabeza na kudharau wanashikilia misimamo yao?







Wabongo tupende kuamini vya kwetu..

#UziTayari
 
Watu hupenda kutoa lawama bila kufikiria hata ni kwa namna gani TMA inakusanya data zake.

Watu wanajua TMA ni kama taasisi inayohusika na mambo ya time travelling.

Wanafikiria kuwa TMA wanapotoa data wanakuwa wameenda kesho kutwa wamekaa huko siku nzima wakaona kila kitu kilichojiri huko kisha wakaja leo kutupa taarifa ya tahadhari.
 
Ni mvua kubwa ila sio Elnino mkuu..
 
Wazee tuwe makini kuna bonge la mvua linakuja wajomba kama uko Mabondeni bora uhame au uende mkoani kaa muda LEO hii tahadhari imektoka tena kutoka EAST AFRICAN HAZARDOUS WATCH Wazee sio poa..



Hii ni hali ya ANGA ILIVYOKUWA WIKI MBILI ZILIZOPITA MVUA KUBWA ILIKUWA SOMALIA,.. ETHIOPIA KIDOGO NA KENYA







WAZEE CHUKUENI TAHADHALI LILE WINGU JEUSI LOTE LIMEANZA KUMOVE KUJA UPANDE WA KUSINI MAGHARIBI YAANI TANZANIA hii ni picha ya satelite leo kuweni makini sana
 
Daraja karibu na mitaa ya Kuelekea Buza miaka nenda rudi halijawahi kupatwa na hali kama ya leo ,sasa inabidi Raia wakanyage maji ya karibu na magoti kisha walifikie daraja kuvuka na kuelekea Buza kwa Lulenge..

 
Hiyo mvua imekuja na neema huku mikoani. Imesababisha Dar wakate umeme na huku watuwashie. Leo ilikuwa siku ya kukatiwa umeme nashangaa tumewashiwa. Ila ujinga unaweza kuta kenge hawa wakatukatia kesho ili kufidia.
Kwangu tofauti ,tokea mvua zianze kunyesha mtaa ninapoishi hapajakatwa umeme hovyo kama kipindi cha nyuma hadi nimeshangaa
 
Hii mvua ni nouma , biashara za online haziend kabisa , mvua haikatiki sku ya pili mfululizo mpak sasa wingu zito , soon itabonda tena
mkiambiwa msevu hela kwa dharula kama hii ili msilale njaa hamsikii na badala yake mnakula hovyo bata na zikiisha mnaanza kutusumbua kwa milawana yenu hii isiyo na kichwa wala miguu
 
Duh! kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kuja second version ya mvua tofauti na hii inayopiga siku hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…