Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Pole sana mkuu lakini siku nyingine unatakiwa kujiongeza sio kukomaa na Gari. Ungeamua kwenda hapo airport ukapaki na kuondoka na boda kwenda home. Leo ungeenda asubuhi kuchukua gari. Ungelipishwa shs 2000 kwa saa. Ambayo si kubwa ukilinganisha na adha iliyopita barabarani.
Mgeni wa Gari hawezi kukubali kulipia gari yake ilale mbali na yeye,atakoma nayo hadi alfajiri!!
 
Foleni ya leo balaa. Ninapoandika thread hii bado niko kwenye foleni Airport
Leo ni balaa for sure. Naona Traffic wamesusa leo.
Sijawahi ona foleni kama ya jana. Nimetumia masaa 8 kutoka posta mpaka nyumbani.
Sijawahi ona foleni kama ya jana.
 
Kweli,wengi hupenda kulala gari akiliona .ila hiyo gridlock sababu ni watumiaji au ni hali ya hewa.
Mgeni wa Gari hawezi kukubali kulipia gari yake ilale mbali na yeye,atakoma nayo hadi alfajiri!!
 
Hii ya foleni ya Banana majumba sita ni ya hovyo kiwahi kutokea.Naona serikali imeamua kutuachia wenyewe tupambane na hali zetu.Yaan toka saa kumi bado hata mataa ya majumba sita sikafika.wala hakuna dalili kama tutatoka hapa
barabara ya bibi titi+mwinyi+bagamoyo jana nayo ilikua balaa...
 
Watu wazima madereva wenye leseni zenu,eti mmeshindwa kujioongoza kwenye Gridlock, mnataka kuilaumu Serekali,au mnazani hakuna Ma Afisa wa Serekali ambao nao walikwama kwa hiyo Gridlock!? Sasa huko driving school mlienda kusomea nini!? Next time ndiyo mjifunze uvumilivu inapotokea hali Kama hiyo,maana wengine walikua wanaforce hadi wanatumbukia Mitaroni huko!!
China watu walika siku 12 foleni yaan masaa kazaa tu watu washaaanza kulalamika
 
Pole sana mkuu lakini siku nyingine unatakiwa kujiongeza sio kukomaa na Gari. Ungeamua kwenda hapo airport ukapaki na kuondoka na boda kwenda home. Leo ungeenda asubuhi kuchukua gari. Ungelipishwa shs 2000 kwa saa. Ambayo si kubwa ukilinganisha na adha iliyopita barabarani.
Mkuu wazo lako zuri. Lakini msururu ule wa magari wote tungepata wazo hilo Airport pasingetosha
 
Serikli iache ujinga! Waache kujenga madaraja yasiyo na tija kama salenda, jana chanzo kikuu cha foleni ni
1. barabara kuu mbili kufungwa, jangwani na mkwajuni! Yanatakiwa madaraja marefu haya maeneo waache ujinga wa madaraja yasiyo na tija! Maana kwa foleni ya jana hata daraja la salenda lisingesaidia kitu...
2. Traffic kukimbia mvua na magari kuanza kujiongoza. Kila mtu ana haraka matokeo yake barabara za kwenda watu wanakuja na za kuja watu wanaenda...

Jana hadi CDF kakwama kwenye foleni ya bagamoyo road dadeki...piga king'ora weeee hamna gari inampisha ndio kwana zimezimwa utadhani zimepaki...wakajimix wakaingia kati kati, shughuli ikaisha hapo...cdf jana pale moroko fao kasimama karibu saa na zaidi. Tena ana bahati ndio foleni zilikua zinaanza kuachia kwa muda ule
 
Kweli,wengi hupenda kulala gari akiliona .ila hiyo gridlock sababu ni watumiaji au ni hali ya hewa.
Inachangiwa na vyote, Hali ya hewa na Watu pia!! Kwa mfano hapa DAR Madereva wengi hawajapita really shule ya driving japo leseni wanazo! Sasa Hali ya hewa ikibadilika ghafla barabarani nao wanapanic na kupoteza concentration!! Mwisho inakua jam coz the can't drive without a traffic Police on the Road!!
 
Poleni.

Nilikua nasoma Kibasila A Level siku hiyo mvua ilinyesha kuanzia asubuhi mpaka mida ya kutoka shule.

Kigogo na Jangwani ni maeneo sugu kwa kujaa maji mvua ya hivi husababisha aliyeko Boma kwenda huko Mbagala na Temeke ni wa huko na aliyeko Kigogo kuja Magomeni ni wa huku.
Ukisema uende Kkoo unajikuta Jangwani hapapitiki.

Ile siku nilitembea kwa mguu kutoka Temeke mpaka Makumbusho. Nafika Kigogo nakuta nyumba zote zimefunikwa na maji watu wapo juu ya mapaa ya nyumba.

Wiki mbele baada ya mvua kukata na jua kuwaka watu wanarudi makazi yao kama kawaida. Same routine miaka nenda miaka rudi.
Halafu unaambiwa nchi uchumi wa kati... Usengee huu
 
Lakini leo imekuwaje na hii foleni? Kimsingi tumelala nje ya Nyumba zetu. Barabara nyingi zimezidiwa na Magari.
Uzembe na kutokujia vipaumbele...jangwani pale na mkwajuni kufungwa ndio vyanzo. Gari zooote za huku ambazo kikawaida ni nyingi ilibidi zikajaze barabara nyingine. Pia polisi kugwaya. Trafiki polisi nimewatambua ni waoga sana. Wakizidiwa WANAKIMBIA sasa wakikimbia ndio kila mtu anaenda njia yoyote.
 
China watu walika siku 12 foleni yaan masaa kazaa tu watu washaaanza kulalamika
Wabongo ni shida! Tena mi naomba siku ya Uchaguzi Vua la Jana lishuke,na NEC hakuna kuhairisha Uchaguzi, mwenye uwezo wa kupiga Kura aendee akapige Kura,nakura zitakozopigwa ndiyo hizohizo zitakazo hesabiwa! Angalia Mziki hata Kura 50 hazitafika!! Alafu eti kuna watu Wanataka kinuke, wakati small Gridlock inawatowa jasho!!
 
Gwaji Fix acha usanii.......Kama umeshindwa kujenga kanisa waamini wako umewaweka kwenye mabanda yenye mabanzi na bati reject ndio utaweza kuondoa mafuriko?

Hiyo Noah kwa Warioba ilikuwaje akaiingiza mtaroni?

Kivule uelekeo wa Daraja na barabara iliyokatika kama havina ushirikiano.
 
Back
Top Bottom