Somoche
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 6,795
- 9,143
Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane.
Hii mvua itasaidia kupunguza vumbi kwa muda mrefu Jiji hili halikua na mvua.
Lakini pia Mvua hutuonyesha kwamba Mji wa Dar na miji mingine Mikubwa inatakiwa ipangwe hata kama Sio mji mzima lakini Maeneo yotr ya Miji hii Mikubwa Yanatakiwa kuwa Na water ways..Maji Mvua Yapite vizuri na maji taka yawe na Mifumo mizuri ya kuyabeba.
Inasikitisha sana kuona kila Open space katika Miji hii imevamiwa na kuuzwa au kujengwa .
Kila eneo la maji kupita Yamevamiwa Na kujazwa mavifusi na hatimae nyumba au biashara Kufunguliwa hapo Kuna kipindi alikuepo mtu pale Nemc akajaribu kuzuia nadhani alikwamba na hatimae alionja joto maana aligusa maslahi ya watu.
Mamlaka Za Maji zilinde vyanzo vyake..Nemc itumie sheria zake..Ardhi na Mipango miji nao watimize wajibu wao bila hivyo miaka nenda rudi shida hii haiishi.