Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Hongera awamu ya tano kwa kuleta mvua sasa ni kuomba tu iende kule moshi ikazime kale ka moto.
Kama tumeweza ma flyover hilo halishindikani.😇
 
Leo meseji zinasomeka.....

Umefika wapi..?
.
.
.
.
Nakaribia.....!
 
Hivi wataalamu wa jiji na Serikali kwa ujumla wana mikakati yoyote ya kuweza KUVUNA MAJI YA MVUA? maana naskia huko dar maji changamoto sugu
Wanna bahar pale..WATAKUFAJE NA KIU huo ni uzembe
 
Sisi wa huku bushi ndio tunaandaa mashamba ya mihogo, tunapanda mbogamboga ila sasa tope la huku, dadeq!!!
 
Hizo serikali zilikuwa zinaongozwa na chama gani? Ukoo wa wavuta bangi ni wavuta bangi tu huwezi kubadilika. Tangu 1961 kinachohubiriwa ni kile kile tu maji, umeme, elimu, na afya. Ukienda huko vijijini hali ni mbaya mpaka sasa maji ni ya shida.
Tukitaka maendeleo tubadili mifumo mpaka vyama ndiyo maana Marekani wanachagua raisi kutoka republic au democratic na wamepiga hatua sana kwenye maendeleo. Huku miaka nenda rudi ni chama cha mboga mboga halafu wanaaminishwa ukichagua chama tofauti na mboga mboga inauzwa nchi au kutakuwa na machafuko. Hiyo changamoto ya madawati imeisha?
Tupo kwenye serekali ambayo inajinadi kutatua changamoto za wananchi kuliko serekali zote zilizopita halafu unasema kuwa Dar maji ni changamoto sugu?Una akili timamu kweli wewe mtu?!
 
Kama video inavyoonyesha, maji yamezidi kiwango hadi yanapita juu ya Daraja, na hivyo magari hayawezi kupita kwa sasa, si salama.

Ila nimeona kuna jamaa mbisho mwenye hilux kapakiza watu nyuma na kuvuka kibishi bishi.
 
Back
Top Bottom