Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Hata UBELGIJI kuna MAFURIKO Jamani[emoji16][emoji16][emoji16]
15278646799030251892.jpg
 
Jiji la makonda aliahidi kujenga daraja la mita 100 kwenda juu jangwani...mkamuombea afkuzwe ona sasa leo mnahaha kama kuku mtagaji.. Njooni huku mikoani
 
Yaani ikaja kutokea mgombea mmoja akaja na sera ya kutokomeza mafuriko Dar es Salaam kwa kujenga drainage system ya maana niaminini mimi atavuna kura na kushinda ukizingatia wapiga kura wengi wapo Dar. Hili jiji jamani mvua ni kero kuubwaa japo ni baraka.

Wagombea njooni ya huo mkakati 2025 maana saa hizi mshachelewa. Kila mkazi wa Dar mvua zinamuathiri pakubwa bila kujali anaishi Oysterbay au Tandale kwa Mfuga Umbwa.
 
Umehamia shamba eh! Hongera sana
🙊🙊🙊
Mi inanichoshaga tu inavyonyesha kwa mafungu kwani sisi huku shamba 😎 imenyesha hii alfajir tena ile ya kiasi tu na usiku kucha kulikuwa na vimanyunyu tu vya hapa na pale.
 
Leo usafiri hapa dsm umezingua sana, kutokana na hizi mvua

Mimi nipo Posta, nipo blocked, jangwani gari hazipiti. Kama upo posta nichek tupeane kampani ya kutembea mpka kimara
Jinsia yako tafadhali
 
Mbona sioni mkisema kuhusu daraja la matumbi, kuna tetesi kuwa hatunalo tena, ni maneno tunayoyasikia huku kwenye daladala tukiwa hapa Mfugale kwenye foleni kwa masaa 3 taslimu sasa.

Mwenye taarifa sahihi tafadhali anijuze, kama ni kweli nianze tu marathon yangu.
 
No daraja lipo sema limefunikwa nimepita hapo saa 12 nimevuka maji ya mapaja bora ushuke utembee tu kuna wanajeshi lakini wanashangaa tu pale hakufai kwa gari hamuwezi kupita sasa hivi.

Sent from my A37f using JamiiForums mobile app
 
Asante.
Kumbe na sisi tulikuwa tumesimamishwa hapa mfugale masaa nenda rudi ili kumpisha mzee baba apite, maana kule ghorofani pia kumefunga, amepita tayari, ngoja tuone.
 
Wa mikoani tunashangaa tu mambo yalivyo huko Dar[emoji134]
 
Serious chige[emoji26]
Kwahiyo kwa hizo hesabu, kwa mwezi utakuwa unakunywa pipa mbili za maji, kwa mwaka unapiga kama pipa 25 hivi!!

Ungeanzisha kilimo cha umwagiliaji basi, manake unaamka zako saa 11 alfajiri, unapiga ndoo ya kwanza, ikifika saa 12 unapiga ndoo ya pili, kisha huyooo shambani; na ukifika huko unajitapishia kwenye nyanya zako!
 
Back
Top Bottom