Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Mvua Kubwa inanyesha Dar tangu usiku wa manane

Wanabodi, imekuwa siku mbaya sana kwangu na wengi ninaowashuhudia katika barabara ya Ally Mwinyi. Kupigana pasi, kuzimika magari, bodaboda kuanguka-kuinuka-kuanguka tena, misafara isiyofuata taratibu, maandamano yasiyo na kibali toka kila pande za mjini kati nk. Kifupi mvua imetukomesha wengi.
 
Hii ya foleni ya Banana majumba sita ni ya hovyo kiwahi kutokea.Naona serikali imeamua kutuachia wenyewe tupambane na hali zetu.Yaan toka saa kumi bado hata mataa ya majumba sita sikafika.wala hakuna dalili kama tutatoka hapa
 
Poleni.

Nilikua nasoma Kibasila A Level siku hiyo mvua ilinyesha kuanzia asubuhi mpaka mida ya kutoka shule.

Kigogo na Jangwani ni maeneo sugu kwa kujaa maji mvua ya hivi husababisha aliyeko Boma kwenda huko Mbagala na Temeke ni wa huko na aliyeko Kigogo kuja Magomeni ni wa huku.
Ukisema uende Kkoo unajikuta Jangwani hapapitiki.

Ile siku nilitembea kwa mguu kutoka Temeke mpaka Makumbusho. Nafika Kigogo nakuta nyumba zote zimefunikwa na maji watu wapo juu ya mapaa ya nyumba.

Wiki mbele baada ya mvua kukata na jua kuwaka watu wanarudi makazi yao kama kawaida. Same routine miaka nenda miaka rudi.
 
Hii ya foleni ya Banana majumba sita ni ya hovyo kiwahi kutokea.Naona serikali imeamua kutuachia wenyewe tupambane na hali zetu.Yaan toka saa kumi bado hata mataa ya majumba sita sikafika.wala hakuna dalili kama tutatoka hapa
Mkuu nimeamua kuzima Gari kabisa. Foleni imesimama kabusa saa 8 na dk17 muda huu
 
Foleni ya leo balaa. Ninapoandika thread hii bado niko kwenye foleni Airport
Leo ni balaa for sure. Naona Traffic wamesusa leo.
Pole kwa mvua! Naona imekuchanganya, sielewi kichwa cha uzi na ulichoandika bila ya kusema umetumia muda gani, unatokea na unakwenda wapi, haiwezekani kujua madhali yanayokukuta.
 
Pole kwa mvua! Naona imekuchanganya, sielewi kichwa cha uzi na ulichoandika bila ya kusema umetumia muda gani, unatokea na unakwenda wapi, haiwezekani kujua madhali yanayokukuta.
Kutoka Samora str to Pugu. Unatumia saa 13 self Drive.
 
Mimi tangu saa kumi nimetoka chang'ombe naelekea kinondoni,hapa ndio nipo maktaba na watu wengine wameamua kupaki magari yao petrol station wanalala hapo,hamna namna
 
Foleni ya leo balaa. Ninapoandika thread hii bado niko kwenye foleni Airport
Leo ni balaa for sure. Naona Traffic wamesusa leo.
Kazi ya Traffic ni kukamata magari yenye vikosa vya kijinga ambavyo vinastahili elimu ndio kazi yao kubwa wale wash%%$$$$.Ila issue critical kama hii wanagwaya wao wanajua kushika tochi tu.
Tukutane tr 28 Ict
 
Hapa kunawahindi wanafanya kitendo cha kiungwana sana,yaani wameamua kugawa maji ya kunywa kwa kila aliyepo kwenye gari,maana ni njaa na kiu tangu saa kumi jioni mpaka sasa watu wapo barabarani,foleni za kipuuzi hata chanzo hakijulikani,daah alafu tunaambiwa miundo mbinu safi,naona Mungu ameamua kutufunulia
 
Lakini leo imekuwaje na hii foleni? Kimsingi tumelala nje ya Nyumba zetu. Barabara nyingi zimezidiwa na Magari.
 
Back
Top Bottom