Mvua ya Jumapili huko Durban Afrika Kusini yaleta madhara kwenye makaburi

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Tunaweza kuwa ni mipango ya Mungu ila haitoshi kuondoa imani kuwa huu ni wakati mgumu sana kwa ndugu wa marehemu ambao waliwapumzisha wapendwa wao katika makaburi ndani ya Durban, Afrika Kusini.


Mvua kubwa ilinyesha jana Jumapili na ni mvua ambayo inadaiwa kuwa ni level 5 imeleta madhara makubwa sana kwenye miundombinu kwenye mitaa ya Lamontville na hii sio mara ya kwanza kwani mwaka 2022 napo pia mvua kubwa ilibeba miili ya Marehemu na kuleta taharuki.


Poleni wanaafrika wenzetu! Hili nalo litapita, kwa sasa mtafute namna bora ya uzikaji kwani sio picha bora kuona masalia ya marehemu yakiwa kwenye mafuriko.
 
Duh,Hilo kaburi lenye majina matatu,walizikwa watu watatu nyakati tofauti au?
 
Halafu mbona inaonekana wanazika juu juu sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…