Mvua ya Jumapili huko Durban Afrika Kusini yaleta madhara kwenye makaburi

Mvua ya Jumapili huko Durban Afrika Kusini yaleta madhara kwenye makaburi

Pengine hayo makaburi yameingilia njia ya maji sasa mnategemea nn?

Haina tofauti na kujenga mabondeni kisha mvua ikija unaanza kutia huruma.
 
Tatizo lilitokea huko nyuma kwa mafuriko ila bado wakaendelea kuzika hapo hapo
Yaani kama sisi na msimbazi yetu kasoro makaburi
 
Tunaweza kuwa ni mipango ya Mungu ila haitoshi kuondoa imani kuwa huu ni wakati mgumu sana kwa ndugu wa marehemu ambao waliwapumzisha wapendwa wao katika makaburi ndani ya Durban, Afrika Kusini.
View attachment 3257479

Mvua kubwa ilinyesha jana Jumapili na ni mvua ambayo inadaiwa kuwa ni level 5 imeleta madhara makubwa sana kwenye miundombinu kwenye mitaa ya Lamontville na hii sio mara ya kwanza kwani mwaka 2022 napo pia mvua kubwa ilibeba miili ya Marehemu na kuleta taharuki.
View attachment 3257480

Poleni wanaafrika wenzetu! Hili nalo litapita, kwa sasa mtafute namna bora ya uzikaji kwani sio picha bora kuona masalia ya marehemu yakiwa kwenye mafuriko.
View attachment 3257481
Ndo hivyo
 
Dah misukosuko hadi kaburini.........unatakiwa u rest in peace ila hata huko nako vurugu tu hakuna peace
 
Back
Top Bottom