R.I.P Magufuli

Kwenye kipindi chako hatukuwahi kusikia huu upuuzi
Huyo aliyewaambia Wapiga kura wasichanganye betri na magunzi tochi haitawaka. Mbona tochi yenyewe ndiyo hii mwanga hafifu???

Tatizo hapa siyo Kiongozi wa Juu bali ni mfumo wa CCM wa kulindana.
 
Hii nchi wananchi wake kama misukule. Watanzania wanaweza kuongozwa hata na mijusi. Kila sehemu ni uozo tu, alafu tunajiita eti tuna viongozi.
 
Tuwaulize walio karibu na hayo mabwawa Kama mvua zinanyesha ama la. Ni kweli Kama mvua zinanyesha Dar na bwawa lipo Dodoma maji hayataingia
 
Utamkumbuka wewe usiyeelewa mbumbumbu
 
Kwani 2020 haijafika au ni upikaji wa takwimu
 
Wasitudanganye sisi siyo watoto wadogo. Wenyewe ndo walitoa tamko kuwa ukosefu wa umeme chanzo kikuu ni hali ya ukame. Sasa mvua inayesha wanaleta sababu za uongo uongo.
 
Alichosema ni kweli kwasababu mikoa yenye mabwawa haina mvua. Sema na yeye angekaa tu kimya kuliko kusema alichosema.
 
Nimemdharau sana huyu jamaa..hivi kwa akili yake anafikiri watu hawazioni hizo mvua...
Anachekesha sana
 
Ile porojo ya kuwa Bomba la gas ikifika Dar mgao wa umeme utakuwa ni historia mmeisahau? Au gas nayo inataka mvua?!
Walidhani hilo bomba litakuwa linazalisha na kusafirisha umeme wa gesi. Uhalisia ni kwamba hilo bomba linasafirisha gesi kidogo sana, chini ya asilimia 20% ya uwezo wake (installed capacity yake) kwa sababu gesi inayozalishwa huko Lindi na Mtwara ni kidogo sana.

Halafu gesi hiyo ilishakuwa si yetu tena kwa sababu ya mkataba mbovu tulioingia nao hao wawekezaji wa kuchimba hiyo gesi. Wawekezaji hao tuliwamilikisha hiyo gesi na hivyo sisi inabidi kuinunua kutoka kwao kwa bei mbaya waitakayo. Kuvunja mkataba huo gharama yake ni kama mbingu au dunia.

Pili mitambo yetu ya kuzalisha umeme hapo Kinyerezi uwezo wake hauzidi MW 600. Halafu mingi ya mitambo hii huwa haifanyi kazi kwani gharama ya maintenance ya hii mitambo nayo ni mbingu na dunia ukilinganisha na mitambo ya umeme wa maji ya mvua huko Kidato na Mtera.

Kazi ipo kweli kweli anayo huyu mpambanaji Dotto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati. Anapambana, hana porojo na nafuu ya mgao imeanza kuonekana ndani ya mwezi mmoja tu tangia aanze kazi. Tumeambiwa mwanzoni mwa mwezi January, mgawo huu utakuwa historia baada ya kuwashwa generator moja kati ya majenereta tisa yaliyoko bwawa la Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…