Mvua zinazonyesha haziingizi Maji kwenye Mabwawa ya Umeme, acheni kulaumu kuhusu Mgawo
R.I.P Magufuli

Kwenye kipindi chako hatukuwahi kusikia huu upuuzi
Huyo aliyewaambia Wapiga kura wasichanganye betri na magunzi tochi haitawaka. Mbona tochi yenyewe ndiyo hii mwanga hafifu???

Tatizo hapa siyo Kiongozi wa Juu bali ni mfumo wa CCM wa kulindana.
 
Tuwaulize walio karibu na hayo mabwawa Kama mvua zinanyesha ama la. Ni kweli Kama mvua zinanyesha Dar na bwawa lipo Dodoma maji hayataingia
 
Huyu Mkurugenzi wa TANESCO, Eng. Gissima Nyamo-Hanga Muongo hafai kuwaMkurugenz waTanesko anasema uongo mchana kweupe. Siyo Rais Mama Samia suluhusu anawapata wapi hawa wasanii?Sihuwi Mama Rais anapangiwa na mtu kuwateuwa Wasanii kama huyu?Hii nchi tunako kwenda kubaya sana nchi haina Umeme wa kutosha nchi haina Maji safi eti kutakuwa kweli na maendeleo? tunaongozwa na viongozi wetu kam vile sisi ni wanyama wao.Wanatuongoza vile wanavyotaka wao wenyewe .Ewe Mwenyeezi Mungu tuokoe na haya matatizo amin.




View attachment 2824097
Tutakukumbuka Baba siku zote Ulale salama.
Utamkumbuka wewe usiyeelewa mbumbumbu
 
Huyu Mkurugenzi wa TANESCO, Eng. Gissima Nyamo-Hanga Muongo hafai kuwaMkurugenz waTanesko anasema uongo mchana kweupe. Siyo Rais Mama Samia suluhusu anawapata wapi hawa wasanii?Sihuwi Mama Rais anapangiwa na mtu kuwateuwa Wasanii kama huyu?Hii nchi tunako kwenda kubaya sana nchi haina Umeme wa kutosha nchi haina Maji safi eti kutakuwa kweli na maendeleo? tunaongozwa na viongozi wetu kam vile sisi ni wanyama wao.Wanatuongoza vile wanavyotaka wao wenyewe .Ewe Mwenyeezi Mungu tuokoe na haya matatizo amin.




View attachment 2824097
Tutakukumbuka Baba siku zote Ulale salama.
Kwani 2020 haijafika au ni upikaji wa takwimu
 
Wasitudanganye sisi siyo watoto wadogo. Wenyewe ndo walitoa tamko kuwa ukosefu wa umeme chanzo kikuu ni hali ya ukame. Sasa mvua inayesha wanaleta sababu za uongo uongo.
 
Alichosema ni kweli kwasababu mikoa yenye mabwawa haina mvua. Sema na yeye angekaa tu kimya kuliko kusema alichosema.
 
Hii ndio Taarifa mpya kutoka Tanesco , kwamba hizo mvua mnazoona zinanyesha haziwezi kupunguza mgawo wa umeme kwa vile maji ya mvua hizo hayaingii kwenye mabwawa hayo , haijulikani kama mabwawa hayo yamepigwa Bati juu yake au La

Na mnaambiwa zaidi mvua hizo zinaharibu miundo mbinu na kuongeza matatizo .

TANESCO imesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini hususani katika ukanda wa Pwani na ukanda wa Ziwa Victoria, mtiririko wa maji yake hauelekei viliko vyanzo vya uzalishaji wa umeme vya Mtera, Kihanzi na Kidatu.

Mkurugenzi wa TANESCO, Eng. Gissima Nyamo-Hanga amesema mvua hizo zimeleta athari katika miundombinu ya shirika katika baadhi ya maeneo, hivyo kuongeza changamoto katika upatikanaji wa umeme.
Nimemdharau sana huyu jamaa..hivi kwa akili yake anafikiri watu hawazioni hizo mvua...
Anachekesha sana
 
Ile porojo ya kuwa Bomba la gas ikifika Dar mgao wa umeme utakuwa ni historia mmeisahau? Au gas nayo inataka mvua?!
Walidhani hilo bomba litakuwa linazalisha na kusafirisha umeme wa gesi. Uhalisia ni kwamba hilo bomba linasafirisha gesi kidogo sana, chini ya asilimia 20% ya uwezo wake (installed capacity yake) kwa sababu gesi inayozalishwa huko Lindi na Mtwara ni kidogo sana.

Halafu gesi hiyo ilishakuwa si yetu tena kwa sababu ya mkataba mbovu tulioingia nao hao wawekezaji wa kuchimba hiyo gesi. Wawekezaji hao tuliwamilikisha hiyo gesi na hivyo sisi inabidi kuinunua kutoka kwao kwa bei mbaya waitakayo. Kuvunja mkataba huo gharama yake ni kama mbingu au dunia.

Pili mitambo yetu ya kuzalisha umeme hapo Kinyerezi uwezo wake hauzidi MW 600. Halafu mingi ya mitambo hii huwa haifanyi kazi kwani gharama ya maintenance ya hii mitambo nayo ni mbingu na dunia ukilinganisha na mitambo ya umeme wa maji ya mvua huko Kidato na Mtera.

Kazi ipo kweli kweli anayo huyu mpambanaji Dotto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati. Anapambana, hana porojo na nafuu ya mgao imeanza kuonekana ndani ya mwezi mmoja tu tangia aanze kazi. Tumeambiwa mwanzoni mwa mwezi January, mgawo huu utakuwa historia baada ya kuwashwa generator moja kati ya majenereta tisa yaliyoko bwawa la Nyerere.
 
Back
Top Bottom