SoC02 Mvuta sigara anavyotumia wastani wa kiasi cha Tsh milioni 16.9 hadi Tsh 42.3 kununua sigara karibu kipindi chote cha maisha yake

SoC02 Mvuta sigara anavyotumia wastani wa kiasi cha Tsh milioni 16.9 hadi Tsh 42.3 kununua sigara karibu kipindi chote cha maisha yake

Stories of Change - 2022 Competition

Mrope11

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
13
Reaction score
3
Bei za baadhi ya sigara nchini Tanzania kutokana na majibu ya wauzaji wa Sigara mnamo mwezi July 2021 wilayani Pangani Mkoani Tanga.

BAADHI YA SIGARABEI ZA SIGARA HIZO KWA SASA
BEI YA PAKTI MOJABEI YA SIGARA MOJA
Winston & Master ClubTsh1600/=Tsh 100/=
Sports Club & Sm ClubTsh 3000/=Tsh 150/=
Portsman (Sports Kawaida)Tsh 3400/=Tsh 200/=
EmbasyTsh 4500/=Tsh 250/=

NB: Kwa mujibu wa maoni ya wauzaji wasigara kwenye maduka ni kwamba kiwango cha chini cha mvutaji wa sigara ni wastani wa sigara 10 kwa siku na pia wanunuaji wengi hununua kwa bei ya reja reja.


Matumizi kwa Siku,Mwezi na Mwaka.
Mchanganuo wa kiasi cha Pesa anchotumia mtu mtu kununua sigara kwa siku,mwezi hadi mwaka kutokana na bei zilizooneshwa kwenye jedwali hapo juu.

1.Winston & Master Club.
Sigara 10 X 100 hivyo ni sawa na Tsh 1000/= kwa siku.

Tsh 1000 X 30 hivyo ni swan a Tsh 30,000/= kwa mwezi.

Tsh 30,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 360,000 kwa mwaka.

2.Sports Club & Sm Club.

Sigara 10 X 15O hivyo kwa siku sawa na Tsh 1500.

Tsh 1500 X 30 hivyo ni sawa na Tsh 45,000/- kwa mwezi.

Tsh 45,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 540,000 kwa mwaka.

3.Portsman (Sports Kawaida).

Sigara 10 X 200 hivyo kwa siku ni sawa na Tsh 2000/=

Tsh 2000 X 30 hivyo kwa mwezi ni sawa na Tsh 60,000/=

Tsh 60,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 720,000/=

4.Embassy.
Sigara 10 X 250 hivyo ni sawa na Tsh 2500 kwa siku.

Tsh 2500 X 30 hivyo ni sawa na Tsh 75,000 kwa mwezi.

Tsh 75,000 X 12 hivyo ni sawa na Tsh 900,000/= kwa mwaka.

Madhara ya Sigara kiuchumi.
NB:- Kwa takwimu za hapo juu mvuta sigara hutumia kiasi cha Tsh 360,000/= hadi Tsh 900,000/= kwa mwaka kununua sigara.

Ripoti ya Makadirio ya Idadi ya Watu kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2035, iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa, amesema Umri wa kuishi kwa Watanzania umeongezeka kutoka miaka 37 mwaka 1978 na kufikia miaka 65 mwaka 2018.

Kijana nchini Tanzania huanza kuwa na maamuzi akifikia miaka 18 na kama akianza shule na miaka 7 hadi anafikisha miaka 18 tayari atakuwa amemaliza kidato cha nne hivyo hapo atakuwa mtu mzima na mimi kama muandaaji wa makala hii nachukulia kama mtu ataanza kuvuta sigara akiwa na miaka 18.

Ukokotozi.
Makadiri ya maisha ya mtanzania kwa sasa ni miaka 65

Kama mtu akianza kuvuta sigara na miaka 18(Hapa tunamuhesabu kama mtu mzima)

Soln 65-18=maana yake maisha yake yote atakuwa na wastani wa miaka 47 ya kuvuta sigara.

Fanya, Kwa takwimu za jedwali hapo juu mvuta sigara hupoteza kiasi cha chini cha Tsh 360,000/= na cha juu hadi Tsh 900,000/= kwa mwaka kununua sigara.

Tafuta kiasi maisha yake yote.

Sawa na 1. Tsh 360,000 X 47=Tsh 16,920,000/=

2. Tsh 900,000 X 47=Tsh 42,300,000/=

HIVYO:- Mvuta sigara Tanzania hutumia kiasi cha Tsh 16,920,000/= hadi Tsh 42,300,000/= kununua sigara kipindi chote cha maisha yake

Uvutaji wa Sigara hupingwa?

NDIO:-Tarehe 31 Mei ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku.

8 Disemba 2020 Shirika la Afya Duniani,WHO lilizindua kampeni ya mwaka mzima kwa jina "Jitolee kuacha kuvuta." Walipokuwa wanaelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutovuta tumbaku kwa mwaka 2021.

Madhara ya kiafya ya Uvutaji wa Sigara.
Ripoti ya shirika la afya Duniani,WHO ya mwaka 2018 inaonesha, “kila mwaka watu wapatao milioni 8 hufariki dunia kutokana na tumbaku. Mamilioni ya wengine wanaishi na magonjwa sugu kama vile saratani, Kifua Kikuu, pumu au magonjwa sugu ya njia ya hewa yanayosababishwa na matumizi ya tumbaku.” Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema matumizi ya tumbaku hayajaacha watoto salama kwa kuwa, “zaidi ya watoto 60,000 wenye umri wa chini ya miaka 5 hufariki dunia kutokana na kuvuta moshi watu wavutao sigara.

NB: HAINA MAANA YA KUHARIBU BIASHARA ZA WAUZA SIGARA BALI NI KAMA INAVYOANDIKWA ONYO UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO.

USISAHAU KWAMBA SERIKALI PIA INAPATA MAPATO KWA KILIMO CHA TUMBAKU ILA MLINZI WA AFYA YAKO NI WEWE MWENYEWE
 
Upvote 2
Kwa maana hiyo ni kwamba anatumia gharama kubwa kuharibu afya yake mwenyewe
 
Mimi binafsi, huwa sipendi kuwapangia watu namna ya kuishi.

Watakuja hapa wavuta sigara wakuulize "wewe ambae huvuti, iko wapi milioni 16 yako?"
 
Nineipenda sana,na inaonekana bajeti ya sigara kwa maisha ya mwanadamu ni kubwa kuliko ya mnywa pombe
 
Mwagilia moyo wewe hizo pesa utakufa utaziacha hata usipovuta fegi. Ambao hawavuti wana nini cha kuonyesha kwa pesa walizosave?
 
Back
Top Bottom