Mvutano Mirathi ya Mengi wapamba moto. Abdiel & Benjamin wapinga kutupwa maombi yao na Mahakama ya Rufani

Jack naye awe na aibu sasa, binafsi namuona kama mtu mwenye tamaa na ujinga mwingi.

Yaani jitu limepambana na mke wake miaka yote mpaka wanafikisha over 60yrs pamoja na mitoto mikubwa na mihangaiko yao yote ya kuutafuta utajiri wewe umeingia tu una miaka haifiki hata mitatu kwenye ndoa mtu akiwa na utajiri wake unataka mirathi mali zote....DUNIA INA MAMBO SANA.... hapa Jack anataka kudhulumu jasho la watu bure kabisa.

Anachostahili ni kusomeshewa watoto na matunzo ya watoto ikiwa pamoja na kuishi nyumba nzuri watoto, budget ya kula siku, shule five stars vyote vikilipwa na IPP group... watoto wawe na shares kidogo baafa ya majibu ya DNA....

Yeye aende akafanye kazi ikiwezekana apewe offer ya Kazi IPP group....otherwise atakuwa anasumbuliwa na njaa tu aka anatafuta mteremko..
 
Yule Mzee alichoharibu kama kweli ni yeye mwenyewe ndiye kaandika ule wosia ni kuwabagua wale watoto wake wakubwa kwamba wasipate chochote kwenye urithi wake, yeye kama alitaka kuwanyima angeweza kusema tu warithi nguo au kitu kingine chochote kisichokuwa na thamani kubwa basi.

Lakini kuwanyima kabisa ndipo alipokosea.
 
Wenzetu waasia mambo ya urithi wamejitahidi kuyaweka vizur

Mengi uhusiano wake na familia sijui ulikuaje ila kwa umri wake watt wake ndio walitakiwa wawe ndio wasimamizi wakuu yy akiwa pemben kama mshauri

Ila cha kuhuzunisha na miaka yake ile huku akitetemeka alikua akionekana kwenye tv akipambania co utadhani watt hana
 
Waarabu/Wahindi pia hawaoi ngozi pendwa kwa kadhia Kama hizi
 
Bila kumsahau the late bilionea Mrema wa Ngurdoto, Naura Spring, na Impala hotels Arusha.
 
Naona huyo Jack anajitahidi apelekwe kuzimu, hio ni dhuluma ya wazi...yaani kukata viuno kidogo tu kwa mzee kwa vi miaka vichache basi anataka urithi wote.

Wakimpeleleka kuzimu ni haki yake sio kwa dhuluma hio.
 
Watu wanaogopa kufa kwa kuweka wosia wazi, limtu linajua kitarithi mali kinakutanguliza na cynide
 


Watoto wake walikua wanasimamia hizo Company miaka yote bila Mzee kuwepo na wao ndio walikua signatories

Walikua wana uwezo wa kumpa hela Mzee au kumyima baada ya kumuona anapotea na kuwaongezea madeni kwa sababu ya michepuko

Mdangaji hakua na taarifa nyingi za maisha ya hiyo familia anaenda kudondokea pua tena hii ni rufaa ya Mia mbili kyln anakata🤓🤓🤓🤓
 
Sio kama naupendelea Uislamu ila Uislamu umeeleza vzr sana mambo ya mirathi na ukifuata sheria hasaa hakuna atakaelalamika.
kwenye Uislamu ni jambo dogo sana hilo
 
Sio kama naupendelea Uislamu ila Uislamu umeeleza vzr sana mambo ya mirathi na ukifuata sheria hasaa hakuna atakaelalamika.
kwenye Uislamu ni jambo dogo sana hilo
Lakini sasa cha kushangaza sasa, wengi wa wanufaika wa mali za marehemu aliyekua muislamu, yaani watoto wa marehemu huwa hawataki mirathi itoke kwa sheria ya kiislamu, wanataka itoke kwa sheria ya mirathi (PAEA Cap 352)
 
Utajiri autafute mwingine kuminyana wafanye wengine.....

Ama kweli BURE NA MAISHA KITONGA ni mtihani sana.....

#Tafuta Pesa Ya Halali Na Uitumie Kwa Kujitanguliza binafsi halafu ndio wafuatie wengine
 
Lakini sasa cha kushangaza sasa, wengi wa wanufaika wa mali za marehemu aliyekua muislamu, yaani watoto wa marehemu huwa hawataki mirathi itoke kwa sheria ya kiislamu, wanataka itoke kwa sheria ya mirathi (PAEA Cap 352)
Maelekezo na utekelezaji ni vitu viwili tofauti.....

Hata wasipotekeleza ,sheria ya dini itabaki palepale kwani wako wanaoitekeleza iwe wanaishi Luanda ,Syria ,Germany ama Mauritius!
 
Kwangu Mimi jambo kubwa la kujifunza hapa ni kuishi na mwanamke. Ukipata Hela ukiwa umeshaoa, jitahidi Sana kumu upgrade mkeo awe na ka exposure Fulani hivi.

Na kama unataka kumbato mwanamke yeyote na unajua una Hela tafuta mwanamke ambaye level yake inaendana na wewe.

Hakuna kitu kibaya kama unakuwa na hela halafu unazaa na vilaza case study nzuri ni yule Bilionea wa Arusha mwenye mahotel.
 
Sasa ilitakiwa iwe wazi kwenye umiliki
Yaani nani ana miliki kipi na kipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…