POTOSHI Mwabukusi awalipua haya kuhusu wanaharakati na CHADEMA

POTOSHI Mwabukusi awalipua haya kuhusu wanaharakati na CHADEMA

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Wakuu, nimekiona hiki kipeperushi je, kina ukweli kwa haya yaliyoandikwa kwa kurejelea mahojiano aliyoyafanya Mwabukusi na kituo cha Clouds TV?

Mwabukusi.jpg
 
Tunachokijua
Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) Boniphace Mwabukusi mnano Septemba 15, 2025 alifanyiwa mahojiano na kituo cha TV cha Clouds katika kipindi cha asubuhi kiitwacho Clouds 360. Akiwa hapo alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo yanayoendelea hivi sasa nchini.

Madai
Katika mitandao ya kijamii kinasambaa kijarida chenye muonekano wa gazeti kikiitwa Mlipuko wa Volcano ambacho kimechapisha taarifa kuwa Mwabukusi awalipua wanaharakati na CHADEMA.

Uhalisia wa kilichoandikwa kwenye kijarida hicho

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo inapotosha uhalisia.

Taarifa iliyoandikwa katika kijarida hicho inapotosha uhalisia wa kile alichokizungumza Mwabukusi katika mahojiano aliyofanyiwa na Clouds TV siku ya Septemba 15, 2025.

Katika mahojiano hayo Mwabukusi hakuitaja CHADEMA kuwa inafanya uhalifu kwa kivuli cha siasa kama kijarida hivyo kilivyoandika.

Aidha Mwabukusi hakusema kuwa CHADEMA imewachokoza ama iache kuwachokoza polisi mahakamani na badala yake alisisitiza kuwa Jeshi la polisi linapaswa kufanyiwa mabadiliko makubwa na lipunguziwe baadhi ya majukumu.
Back
Top Bottom